IPS Swahili

Mauritania: Hatua Ndogo za Kutokomeza Tohara kwa Wanawake
NOUAKCHOTT, Mei 8 (IPS) - Mkakati mkali wa kukomesha tohara kwa wanawake
nchini Mauritania unaleta mafanikio ya polepole, pamoja na kwamba
wanaharakati wanatambua bado kuna mambo mengi ya kufanyika katika
taifa ambalo theluthi mbili ya wasichana wamefanyiwa tohara.

GHANA: Akina Baba Wapambana Kuwaokoa Watoto Wao wa Kike Kutokana na Tohara
ACCRA, Mei 8 (IPS) - Wakati Jack Sabadgou alipoondoka nchini Ghana
kwenda Uswis miaka 10 iliyopita, aliacha mtoto mchanga wa kike
nyuma ili aweze kulelewa na mama yake. Sasa anahitaji kuishi na
mtoto wake, na mwanaume huyo anaona muda haumtoshi kumwokoa mtoto
wake kutumbukia kwenye mila zilizopigwa marufuku za tohara kwa
wanawake na watoto wa kike.

TANZANIA: Ufugaji Viumbe Bahari, Muhimu Kuongeza Kipato, Kutunza Mazingira
BAGAMOYO, Mei 7 (IPS) - Kwa miaka mingi wakazi wa pwani wamekuwa
wakitegemea zaidi kujipatia kipato na chakula kutokana na
kuendesha shughuli za uvuvi aidha katika mabwawa au kwenye Bahari
ya Hindi. "Lakini kutokana na kuongezeka kwa watu samaki
wamepungua kwa kiasi kikubwa katika bahari na katika mabwawa ya
asili na mahitaji yamezidi kuongezeka," alisema Mkurugenzi wa
Mradi wa Pwani wa Mpango wa Kusimamia Mazingira na Rasilimali za
Pwani (TCMP – Pwani), Baraka Kalangahe.

Kuokoa Maisha ya Akina Mama katika Sudan Kusini
JUBA, Mei 7 (IPS) - Martha Borete Angela ni mwanafunzi wa mwaka wa
kwanza katika programu ya wakunga wa jadi katika Taasisi ya
Mafunzo ya Afya ya Sudan Kusini.

Dharula Iliyosahauliwa katika Jimbo la Blue Nile Nchini Sudan
JAMAM, Sudan Kusini, Mei 7 (IPS) - Hamid Yussef Bashir alisema alitembea kwa siku 17
na mke wake na watoto watano ili kufika katika kambi ya wakimbizi
katika Sudan Kusini. Walipofika Jamam, waliungana na watu wengine
wapatao 37,000 ambao walikimbia vita na hivyo kuwafanya kuvuka
mpakani katika jimbo la Blue Nile nchini Sudan.
Mazingira ya
kambi ya wakimbizi hayafai, alisema. Kuna uhaba wa maji safi na
familia yake inabidi kuhamisha kibanda chao kabla mvua haijaanza
kunyesha na mafuriko kulikumba eneo waliloweka kambi. Lakini
walikuwa na bahati kuweza kusafiri salama hadi hapa.

Njaa Nchini Chad: Wanawake Wavunja Vichuguu Kutafuta Nafaka Zilizohifadhiwa na Mchwa
N’DJAMENA, Mei 7 (IPS) - "Ni Mungu tu anayejua nini kinatokea kwangu
mimi na watoto – kwa miezi miwili hatukuwa na kitu cha kula.
Tunaishi kama ombaomba," Henriette Sanglar, mama wa watoto
wanne katika majengo ya makazi ya Moursal kwenye mji mkuu wa
Chad, N’Djamena, aliiambia IPS.

Watoto wa Ivory Coast Waishi kwa Hofu
ABIDJAN, Aprili 23 (IPS) - Kundi la watoto wanaocheza katika eneo la wazi
kwenye mji maarufu kibiashara wa Ivory Coast wa Abidjan
wanaonekana kutokuwa na uangalizi. Lakini gari linapotoa ngurumo
mkali na kutoa moshi, wanatetemeka. Wakati askari wanapotembea
kupita eneo hilo, wanatetemeka. Na wanaonekana kuwa na hofu
wakati mtu mzima anapowasogelea.

Jukwaa la Maji Duniani Lasema Mabwawa Makubwa ‘Siyo Endelevu’
MARSEILLE, Ufaransa , Aprili 23 (IPS) - Mashirika kadhaa yasiyokuwa ya kiserikali yalitumia
Jukwaa la Maji Duniani (WWF) lililofanyika mjini Marseille wiki
iliyopita kama fursa ya kukumbusha jumuiya ya kimataifa kuhusu
madhara makubwa ya mabwawa makubwa duniani kote.

Maji Yanapokauka Katika Mabomba ya Mauritius
PORT-LOUIS, Apirili 23 (IPS) - Rani Murthy, mfanyakazi wa serikali anayeishi
Plaines Wilhems, katikati mwa Mauritius, anaamka saa tisa usiku
kusubiri maji ya gari kutoka Mamlaka ya Maji kuweza kupata maji
ya kupikia na shughuli nyingine za nyumbani.

Kuishi kwa Mlo Mmoja kwa Siku Nchini Swaziland
MBABANE, Aprili 23 (IPS) - Margaret Gamedze anaendesha maisha kwa kupiga pasi
katika jumuiya yake ya makazi duni ya Msunduza, ambayo
yanapatikana kilomita moja nje ya mji mkuu wa Swaziland wa
Mbabane. Tangu mgogoro wa kifedha nchini humo, hawezi tena
kuingiza fedha ya kuweza kulipia pango katika kijumba chake cha
tope cha chumba kimoja, ambacho anatumia pamoja na watoto wake
watano.

Kuokoa Mahindi Nchini Kenya
NAIROBI, Aprili 23 (IPS) - Wakati baadhi ya wakulima wa mahindi katika Jimbo
la Magharibi nchini Kenya wanaishi kwa kutegemea mavuno ya msimu
uliopita, Robert Oduor anahesabu hasara yake baada ya magugu
vamizi yanayojulikana kama Striga au Kayongo kushambulia hekta
yake moja ya mahindi.

Kudhalilisha Mazungumzo ya Kimataifa ya Biashara
GENEVA, Aprili 19 (IPS) - India, Brazili, na Afrika Kusini, kundi linalokuza
ushirikiano wa kimataifa miongoni mwa nchi hizo tatu unaojulikana
kama IBSA, pamoja na China na nchi kadhaa zinazoendelea,
wamekemea jitihada zinazoendelea za kujaribu kuandaa mikataba ya
kipekee ya biashara huria ya sekta ya huduma bila kukamilisha
mazungumzo ya biashara ya kimataifa ya Shirika la Biashara
Ulimwenguni.

Mto Limpopo Unapogeuka Kuwa Vumbi
BEITBRIDGE, Zimbabwe, Aprili 19 (IPS) - Chapita Ramovha anakumbuka siku ambazo Mto Limpopo
ulipozingira kijiji chake kusini mwa Zimbabwe. Anasema kuwa hapo
kabla wakazi wa kijiji cha Makakavhule ilibidi kujenga ukuta
mrefu kulinda makazi yao kutokana na mafuriko. "Mto Limpopo
ni kitu cha kushangaa, uzuri wa asili, chanzo cha chakula na
kipato kwa ajili yetu sisi ambao tunaishi kandokando ya mto
huo," anakumbuka mkulima huyo mdogo mdogo.

Bado Wanaume Nchini Ivory Coast Wana Maamuzi Katika Haki za Uzazi
ABIDJAN, Aprili 19 (IPS) - "Ningependa kutumia njia za uzazi wa mpango,
lakini mume wangu hataki," anasema Bintou Moussa*. Mama huyo
mwenye umri wa miaka 32 ndiyo tu anatoka kujifungua mtoto wake wa
sita katika Hospitali Kuu ya Abobo katika mji maarufu kibiashara
wa Ivory Coast, Abidjan.

Somo la Demokrasia Katika Mawimbi ya Utangazaji Sudan Kusini
JUBA, Aprili 19 (IPS) - Ni muda wa alasiri na kundi la wanaume na wanawake
wanaanza kukusanyika chini ya kivuli cha mwembe mkubwa katika mji
wa Yambio, mji mkuu wa jimbo la maghari mwa Ikweta. Kikundi hiki
hakipo hapa kwa ajili ya mkutano wa kikabila, kisiasa wala
masuala ya kidini. Wapo hapa kusikiliza redio.