Inter Press Service News Agency
Friday, February 15, 2019   21:06 GMT    
  Subscribe !
 

Enter your email and receive TerraViva Africa, our free weekly journal

   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions

UAE:
Dubai Yaahidi Kudhibiti Uchafuzi wa Mazingira Unaosababishwa na Kelele
Kwa Wahariri: Taarifa ifuatayo imetolewa na Shirika la Habari la Falme za Kiarabu (WAM)

DUBAI, Sep 29 (WAM) - Manisipaa ya Dubai katika Muungano wa Falme za Kiarabu (UAE) ina mpango wa kuchukua hatua za kisheria dhidi ya makampuni na taasisi ambazo zinatoa sauti zinazozidi kelele ambazo zinaruhusiwa kutolewa na taasisi zao, kwa mujibu wa Sheria ya Kiwizara Na. 12 ya mwaka 2006 katika kulinda uchafuzi wa hali ya hewa, alisema afisa mwandamizi wa Manisipaa hiyo.

"Wakati wa mwezi huu wa Oktoba, awamu ya kwanza ya mradi wa kufuatilia viwango vya kelele mjini Dubai unaanza, kwani utatekelezwa katika awamu mbili. Awamu ya kwanza ni pamoja na kuwepo kwa utafiti mpana wa viwango vya kelele katika Falme za Kiarabu utakaofanyika kwa kutumia teknolojia ya hali ya juu, ambapo takwimu za mawimbi ya sauti zinakusanywa na kuunganishwa na ramani za mipango miji na ujenzi Dubai. Baadaye takwimu hizi zitafanyiwa uchambuzi ili kubainisha maeneo yanayokumbwa na uchafuzi mkubwa wa mazingira kutokana na kelele," alisema Hussain Nasser Lootah, Mkurugenzi Mkuu wa Manisipaa ya Dubai.

"Baada ya hapo, Manisipaa ya Dubai itachukua hatua zote za kisheria dhidi ya makampuni na taasisi ambazo zinatoa kelele zinazozidi kiwango kinachoruhusiwa kisheria, kwa mujibu wa Sheria ya Kiwizara," alielezea.

"Unapouliza juu ya aina ya uchafuzi wa mazingira, tunahesabu kila kitu isipokuwa uchafuzi unaosababishwa na kelele, ambao unaacha madhara makubwa kwa afya za watu. Tafiti za kimataifa zimeonyesha kuwa kelele ni aina ya uchafuzi wa mazingira hatari sana kwa afya ya umma, na zina madhara mabaya katika mfumo wa kusikia, misuli, mfumo wa uyeyushaji wa chakula wa mwanadamu, zinaongeza uwezekano wa kupata msongo wa mawazo na uchovu, na kumwezesha mtu kutumia vilevi vinavyozidi kiwango kilichokubalika kimataifa," alisema.

"Kutokana na msimamo huu, Manisipaa ya Dubai imekuwa ikifuatilia kwa ukaribu zaidi suala la kelele kwa muda mrefu, na kutoa kipaumbele muhimu kwa mazingira kwa njia nyingi, kwa kuzindua mipango ya kuhakikisha kuwa kunakuwepo na utulivu katika Falme za Kiarabu, ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa hewa safi, maji safi au kupunguza kiasi cha joto," Lootah alisema.

"Lengo la Manisipaa ya Dubai ni kujenga mji mzuri kabisa ambao unaonyesha mafanikio na utulivu na kuishi katika maisha endelevu, na hivyo kuamua kutekeleza mradi huo, kwa kushirikiana na mkakati wa Kiidara wenye lengo la kuendeleza mafanikio ya kimazingira katika Falme za Kiarabu, kwa kutengeneza sera, kanuni na programu zenye ufanisi ili kuondokana na changamoto zote za kimazingira zinazotokana na ukuaji wa kasi," aliongeza. (END/2014)

 

 
English Version
Versión en español
Version em português
 Latest News in Swahilli
News in RSS
UAE: Dubai Yaahidi Kudhibiti Uchafuzi wa Mazingira Unaosababishwa na Kelele
UAE: Mfuko wa Khalifa Wandelea Kusambaza Misaada kwa Watu Walioyakimbia Makazi yao Nchini Iraq
UAE: Shirika la ERC Lasambaza Msaada wa Dharula kwa Wakazi wa Jiji la Sheikh Zayed, Kaskazini mwa Ukanda wa Gaza
UAE: Shirika la Ndege la Emirates Lazindua Safari za Moja kwa Moja kwenda Brussels
UAE: Mkataba wa Makubaliano na Umoja wa Mataifa Wasainiwa Kukarabati Jengo Namba 17 katika Makao Makuu ya Geneva
UAE: Msaada wa Dharula kwa Watu Walioyakimbia Makazi yao katika Eneo la Kurdistan Nchini Iraq
UAE: Makamu wa Rais Mohamed bin Zayed Amtakia Mafanikio Mema Waziri Mkuu Mteule wa Iraq
UAE: Shirika la Nusu Mwezi Mwekundu la Falme za Kiarabu Lasaidia Familia za Wakimbizi wa Gaza Kurejea Nyumbani
UAE: Shirika la Nusu Mwezi Mwekundu Latoa Misaada zaidi kwa Raia wa Gaza Walioyakimbia Makazi Yao
UAE: GWU, FAO Wasaini Mkataba wa Makubaliano wa Kuwezesha Wanawake Katika Kilimo
More >>
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également >>
 News in Swahili
News in RSS
XML error: The element 'html' is used but not declared in the DTD/Schema.