Inter Press Service News Agency
Friday, February 22, 2019   20:39 GMT    
  Subscribe !
 

Enter your email and receive TerraViva Africa, our free weekly journal

   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions

UAE:
Shirika la Ndege la Emirates Lazindua Safari za Moja kwa Moja kwenda Brussels
Kwa Wahariri: Taarifa ifuatayo imetolewa na Shirika la Habari la Falme za Kiarabu (WAM)

BRUSSELS, Sep 6 (WAM) - Shirika la Ndege la Emirates katika Muungano wa Falme za Kiarabu (UAE) limezindua ndege yake kwenda mjini Brussels nchini Ubelgiji. Huduma mpya ya kila siku itashuhudia hadi wateja 16,000 wa Emirates wakisafiri katika ndege ya kila siku aina ya Boeing 777-200LR kati ya Dubai na Brussels kila mwezi.

Brussels ni mji wa 145 unaohudumiwa na Shirika la Ndege la Emirates duniani na mji wa 37 barani Ulaya. Shirika hilo linasema litafanya kazi muhimu ya kuunganisha biashara kati ya Ubelgiji na masoko muhimu katika Mashariki ya Mbali. Emirates pia inakadiria kuwa itasaidia katika kuendeleza sekta ya utalii nchini humo, kwani Ubelgiji ni sehemu muhimu ya Ulaya inayounganisha wasafiri kutoka Australasia.

"Emirates ni Shirika la Ndege pekee linalotoa huduma za Daraja la Kwanza kutoka Brussels kwenda mataifa ya Mashariki ya Kati na ya Mbali. Ikiwa ni makao makuu ya mashirika makubwa ya kimataifa tayari tunaona mahitaji makubwa ya wasafiri kutoka masoko kama ya China, UAE, Japan na India, moja ya washirika wakubwa wa biashara wa Ubelgiji," alisema Thierry Aucoc, Makamu wa Rais Mwandamizi wa Emirates Anayeshughulikia Masuala ya Ushirikiano wa Kibiashara na Ulaya na Shirikisho la Urusi. Shirika la Ndege la Emirates linasema UAE ni mshirika mkubwa wa Ubelgiji huku zaidi ya euro bilioni 4 za bidhaa zikiuzwa baina ya nchi hizo kila mwaka. Uingizaji na uuzaji nje wa bidhaa umekua kwa kasi tangu mwaka 2009 huku makampuni 1504 ya Ubelgiji yakisafirisha bidhaa kwenda UAE mwaka jana.

Zaidi ya makampuni 30 ya Ubelgiji yanayofanya kazi kwa mafanikio katika Dubai yamejengwa na makampuni ya Ubelgiji. Kampuni ya Ujenzi ya Ubelgiji ya Besix imefanya kazi muhimu katika ujenzi wa Burj Khalifa na Kampuni ya Jan De Nul Group ilifanya kazi ya kujenga upya ardhi ya mchanga ya ukubwa wa mita 186,500,000 kuwa ardhi bora na ardhi katika Visiwa vya Palm Jumeirah ambavyo ni maarufu duniani.

Utalii kutoka UAE kwenda Ubelgiji umekua kwa kiasi kikubwa katika miaka mitano iliyopita huku idadi ya watalii ikiongezeka zaidi ya mara tatu tangu mwaka 2009. Safari mpya ya moja kwa moja kutoka Dubai kwenda Brussels inatarajiwa kukuza sekta hii zaidi, ikiwa ni pamoja na kuongeza ndege kutoka masoko muhimu ya Mashariki ya Mbali na Australasia.

Usafirishaji wa mizigo kwenda Ubelgiji umefikia asilimia 86 ya GDP nchini humo na ndege za mizigo za shirika hilo za Emirates SkyCargo zitasaidia kuongeza asilimia hizi kwa kuongeza tani 17 za mizigo kwa siku. Bidhaa muhimu zinazosafirishwa nje ni pamoja na madawa ya binadamu, vipuri vya magari, chocolates,mashine na vifaa vya elektroni.

Mapema wiki hii, Shirika la Ndege la Emirates lilizindua huduma yake kwenda jijini Oslo, Norway, na litapanua huduma zake katika bara la Ulaya mwezi ujao kwa kuzindua safari za kwenda Budapest nchini Hungary Oktoba 27. (END/2014)

 

 
English Version
Versión en español
Version em português
 Latest News in Swahilli
News in RSS
UAE: Dubai Yaahidi Kudhibiti Uchafuzi wa Mazingira Unaosababishwa na Kelele
UAE: Mfuko wa Khalifa Wandelea Kusambaza Misaada kwa Watu Walioyakimbia Makazi yao Nchini Iraq
UAE: Shirika la ERC Lasambaza Msaada wa Dharula kwa Wakazi wa Jiji la Sheikh Zayed, Kaskazini mwa Ukanda wa Gaza
UAE: Shirika la Ndege la Emirates Lazindua Safari za Moja kwa Moja kwenda Brussels
UAE: Mkataba wa Makubaliano na Umoja wa Mataifa Wasainiwa Kukarabati Jengo Namba 17 katika Makao Makuu ya Geneva
UAE: Msaada wa Dharula kwa Watu Walioyakimbia Makazi yao katika Eneo la Kurdistan Nchini Iraq
UAE: Makamu wa Rais Mohamed bin Zayed Amtakia Mafanikio Mema Waziri Mkuu Mteule wa Iraq
UAE: Shirika la Nusu Mwezi Mwekundu la Falme za Kiarabu Lasaidia Familia za Wakimbizi wa Gaza Kurejea Nyumbani
UAE: Shirika la Nusu Mwezi Mwekundu Latoa Misaada zaidi kwa Raia wa Gaza Walioyakimbia Makazi Yao
UAE: GWU, FAO Wasaini Mkataba wa Makubaliano wa Kuwezesha Wanawake Katika Kilimo
More >>
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également >>
 News in Swahili
News in RSS
XML error: The element 'html' is used but not declared in the DTD/Schema.