UAE: Shirika la Nusu Mwezi Mwekundu Latoa Misaada zaidi kwa Raia wa Gaza Walioyakimbia Makazi Yao Kwa Wahariri: Taarifa ifuatayo imetolewa na Shirika la Habari la Falme za Kiarabu (WAM)
GAZA, Julai 31 (WAM) - Shirika la Nusu Mwezi Mwekundu (ERC) katika Muungano wa Falme za Kiarabu (UAE) siku ya Jumatano limetoa misaada zaidi ya chakula kwa Wapalestina wa Ukanda wa Gaza ambao wameyakimbia makazi yao kutoka maeneo mbalimbali yanayokabiliwa na mapigano.
Emad Abu Laban, Mkurugenzi wa Ofisi ya ERC katika Gaza, alisema shirika hilo lilisambaza zaidi ya gunia 2,300 za chakula kwa wakimbizi ambao wamehifadhiwa katika mashule yanayoendeshwa na Shirika la Misaada na Kazi za Umoja wa Mataifa kwa Wakimbizi wa Palestina katika Mashariki ya Karibu (UNRWA) au katika nyumba za ndugu zao.
Shirika hilo kubwa la misaada ya kibinadamu katika UAE pia lilitoa vipande 500 vya nguo kwa wakimbizi, hususan watoto katika idadi kadhaa ya shule zilizopo chini ya UNRWA huko Gaza.
Jitihada za karibuni zaidi za ERC huko Gaza ziliratibiwa na Chama cha Nusu Mwezi Mwekundu cha Palestina (PRCS).
Kwa kuongeza, zaidi ya vitanda 20 vilitolewa na ERC katika hospitali ya Deir Al Balah, Gaza, hivi karibuni na kwa sasa hospitali hiyo inaendeshwa na PRCS, na inapokea zaidi ya wagonjwa 50 na kufanya upasuaji wa zaidi ya wagonjwa 20 kwa siku.
Ujumbe wa ERC umeshatembelea Ukanda wa Gaza mara nne ili kuiweka sawa hospitali hiyo na kuzindua operesheni kubwa ya misaada ya shirika hilo.
(END/2014)
|
|
|