Inter Press Service News Agency
Friday, February 15, 2019   21:43 GMT    
  Subscribe !
 

Enter your email and receive TerraViva Africa, our free weekly journal

   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions

UAE:
GWU, FAO Wasaini Mkataba wa Makubaliano wa Kuwezesha Wanawake Katika Kilimo
Kwa Wahariri: Taarifa ifuatayo imetolewa na Shirika la Habari la Falme za Kiarabu (WAM)

ABU DHABI, Julai 22 (WAM) - Katika kutekeleza maelekezo ya Sheikha Fatima bint Mubarak, mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (GWU) wa Muungano wa Falme za Kiarabu (UAE) na Balozi wa Hisani wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), Noura Al Suwaidi, Mkurugenzi wa GWU, na Abdu bin Qasim Al Osairi, mratibu wa zamani wa kanda ndogo ya FAO katika Baraza la Ushirikiano wa Mataifa ya Ghuba (GCC) na Yemen na Mwakilishi wa FAO katika UAE, walisaini mkataba wa makubaliano wa kuwajengea uwezo wanawake katika sekta ya kilimo.

Mkataba huo wa makubaliano utawezesha wanawake wa Falme za Kiarabu kukuza soko la ajira kwa kuanzisha miradi ya kilimo na viwanda vya vyakula.

Noura Al Salaiti, Mratibu wa Kitaifa wa Mradi wa Kujengea Uwezo Wanawake, alisema kuwa FAO, kwa upande wake, itatoa utaalam wake wa kiutawala na kiufundi katika kujenga uwezo katika maeneo ya kuanzisha ujasiriamali mdogo na wa kati, wakati GWU itatoa fedha na vifaa kusaidia mradi huo utakaotekelezwa kwa awamu.

Alisema warsha tisa za kibiashara zitafanyika kutoa mafunzo kwa wanawake 225 katika eneo zima la UAE kwa ushirikiano kati ya serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali katika Falme za Kiarabu.

Lengo la mradi ni kuhamasisha wanawake kuanzisha biashara zao wenyewe na kuendeleza biashara ambazo tayari zinafanyika, kilimo, na miradi ya chakula. Kupitia mfumo wa kufanya kazi kwa pamoja, wanawake watajifunza dhana ya ujasiriamali na nguvu, udhaifu, fursa na vitisho (SWOT) vya kufanya ujasiriamali pamoja na kuwapatia mafunzo ya uongozi na kuibua vipaji vyao. (END/2014)

 

 
English Version
Versión en español
Version em português
 Latest News in Swahilli
News in RSS
UAE: Dubai Yaahidi Kudhibiti Uchafuzi wa Mazingira Unaosababishwa na Kelele
UAE: Mfuko wa Khalifa Wandelea Kusambaza Misaada kwa Watu Walioyakimbia Makazi yao Nchini Iraq
UAE: Shirika la ERC Lasambaza Msaada wa Dharula kwa Wakazi wa Jiji la Sheikh Zayed, Kaskazini mwa Ukanda wa Gaza
UAE: Shirika la Ndege la Emirates Lazindua Safari za Moja kwa Moja kwenda Brussels
UAE: Mkataba wa Makubaliano na Umoja wa Mataifa Wasainiwa Kukarabati Jengo Namba 17 katika Makao Makuu ya Geneva
UAE: Msaada wa Dharula kwa Watu Walioyakimbia Makazi yao katika Eneo la Kurdistan Nchini Iraq
UAE: Makamu wa Rais Mohamed bin Zayed Amtakia Mafanikio Mema Waziri Mkuu Mteule wa Iraq
UAE: Shirika la Nusu Mwezi Mwekundu la Falme za Kiarabu Lasaidia Familia za Wakimbizi wa Gaza Kurejea Nyumbani
UAE: Shirika la Nusu Mwezi Mwekundu Latoa Misaada zaidi kwa Raia wa Gaza Walioyakimbia Makazi Yao
UAE: GWU, FAO Wasaini Mkataba wa Makubaliano wa Kuwezesha Wanawake Katika Kilimo
More >>
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également >>
 News in Swahili
News in RSS
XML error: The element 'html' is used but not declared in the DTD/Schema.