Inter Press Service News Agency
Wednesday, September 19, 2018   21:41 GMT    
  Subscribe !
 

Enter your email and receive TerraViva Africa, our free weekly journal

   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions

UAE:
Rais wa Italia Atoa Tuzo kwa Raia Wawili wa Falme za Kiarabu
Kwa Wahariri: Taarifa ifuatayo imetolewa na Shirika la Habari la Falme za Kiarabu (WAM)

ABU DHABI, Mei 28 (WAM) - Rais wa Italia Giorgio Napolitano ametoa tuzo kwa Meja Jenerali Ahmed Al Tuniaji, Kamanda wa zamani wa Kikosi cha Wanamaji, na Mahsh Saeed Al Hamili, Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kiusalama wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje ya (UAE), tuzo ambazo zinatolewa na Jamhuri ya Italia kutambua jitihada zao katika kuimarisha mahusiano baina ya UAE na Italia katika Nyanja zote.

Balozi wa Italia katika UAE Giorgio Starace aliwasifu Al Tunaiji na Al Hamili wakati wa sherehe zilizofanyika jana katika Ubalozi wa Abu Dhabi mbele ya Kamanda wa Vikosi vya Wanamaji wa UAE, Ibrahim Salem Al Musharrakh, na idadi kubwa ya raia wa Falme za Kiarabu na makamanda wa jeshi kutoka nchini Italia.

Aliwasifu kwa kupata tuzo hiyo ya heshima, na kupongeza kiwango cha mahusiano baina ya nchi hizo mbili na mafanikio ambayo yamepatikana nchini UAE.

Kwa upande wake, Al Tunaiji alielezea furaha yake na heshima kubwa kupata tuzo hiyo iliyotolewa na Rais wa Italia, akiielezea kama ishara ya upendo na urafiki baina ya Rais na serikali ya Italia na UAE na watu wake. Aliongeza kuwa tuzo za heshima kutoka Italia zitazidisha mahusiano kati ya UAE inayoongozwa na Rais Sheikh Khalifa bin Zayed Al Nahyan na Italia.

Al Hamili aliishukuru pia serikali ya Italia, ujumbe wa Italia na wafanyakazi wa ubalozi wa nchi hiyo kutokana na upendo wao, akiongeza kuwa tuzo za heshima kwa raia wawili wa Falme za Kiarabu ni kutambua uhusiano mzuri kati ya Italia na UAE ikiongozwa na Sheikh Khalifa, na kwa serikali inayoongozwa na Makamu wa Rais na Waziri Mkuu na Mtawala wa Dubai Dubai, Sheikh Mohammed bin Rashid Al Maktoum.

Aliongeza kuwa kulingana na maelekezo ya Rais wa UAE na ufuatiliaji kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje, Sheikh Abdullah bin Zayed Al Nahyan, balozi 72, balozi ndogo 13 na ofisi nyingine za kibalozi tatu zilianzishwa kutumikia raia walioko nje ya nchi. Hadi sasa UAE ina balozi zipatazo 103, balozi ndogo 71 na ofisi za kibalozi na mashirika ya kimataifa 15 ili kukuza uhusiano na nchi mbalimbali duniani kote. (END/2014)

 

 
English Version
Versión en español
Version em português
 Latest News in Swahilli
News in RSS
UAE: Dubai Yaahidi Kudhibiti Uchafuzi wa Mazingira Unaosababishwa na Kelele
UAE: Mfuko wa Khalifa Wandelea Kusambaza Misaada kwa Watu Walioyakimbia Makazi yao Nchini Iraq
UAE: Shirika la ERC Lasambaza Msaada wa Dharula kwa Wakazi wa Jiji la Sheikh Zayed, Kaskazini mwa Ukanda wa Gaza
UAE: Shirika la Ndege la Emirates Lazindua Safari za Moja kwa Moja kwenda Brussels
UAE: Mkataba wa Makubaliano na Umoja wa Mataifa Wasainiwa Kukarabati Jengo Namba 17 katika Makao Makuu ya Geneva
UAE: Msaada wa Dharula kwa Watu Walioyakimbia Makazi yao katika Eneo la Kurdistan Nchini Iraq
UAE: Makamu wa Rais Mohamed bin Zayed Amtakia Mafanikio Mema Waziri Mkuu Mteule wa Iraq
UAE: Shirika la Nusu Mwezi Mwekundu la Falme za Kiarabu Lasaidia Familia za Wakimbizi wa Gaza Kurejea Nyumbani
UAE: Shirika la Nusu Mwezi Mwekundu Latoa Misaada zaidi kwa Raia wa Gaza Walioyakimbia Makazi Yao
UAE: GWU, FAO Wasaini Mkataba wa Makubaliano wa Kuwezesha Wanawake Katika Kilimo
More >>
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également >>
 News in Swahili
News in RSS
XML error: The element 'html' is used but not declared in the DTD/Schema.