Inter Press Service News Agency
Thursday, January 24, 2019   00:15 GMT    

:
Wafadhili Lazima Kutumia Fursa ya Mwaka 2013 Katika Ukanda wa Sahel, Umoja wa Mataifa Watoa Ombi


Na Carey L. Biron


Ikiripotiwa kuwa mgogoro mbaya zaidi wa chakula katika ukanda wa Sahel barani Afrika unaonekana kutatuliwa, ofisa wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa katika eneo hilo, David Gressley, alionya kuwa uwezekano wa kupita katika dharula hiyo haupaswi kuondoa mtizamo wa kimataifa kutoka kile ambacho kinahitaji kufanyika mwaka 2013, ambao anauita mwaka mgumu wa kujenga uhakika wa chakula katika ukanda huo.

WASHINGTON, Oktoba 29 (IPS) -
Uwezekano wa kukabiliana na hali mwaka 2013 umetokana na kukutana kwa vipambele vikubwa vya kimataifa katika Sahel wakati huo huo serikali kadhaa za kikanda, ambazo ni nchi za Niger, zimeshaanza kwa kiasi kikubwa, kazi ya kushughulikia baadhi ya sababu za msingi za uhaba wa chakula katika ukanda huo.

Lakini Gressley ana wasiwasi kuwa fursa hii ingeweza kuondolewa siyo tu na matarajio ya mavuno mazuri kiasi mwaka huu, lakini pia kutokana na hali ya machafuko nchini Mali na hivyo kuondoa mtizamo wa kimataifa.

"Kwa kuwa na habari njema, hatari ni kwamba tutasahau mgogoro wa kudumu – kutaendelea kuwa na masuala ya usalama wa chakula katika ukanda wa Sahel, na tunajua ukame utatupiga tena katika siku zijazo," Gressley, mratibu wa masuala ya kibinadamu kikanda katika Sahel, alisema hapa mjini Washington.

"Tuna fursa ya kuchagua kufanya matatizo sugu kuendelea, kukabiliana na misaada mikubwa, au tunaweza kuanza kuchukua hatua sasa kujaribu kupunguza madhara – kwa watu wanaoteseka na gharama za kuchukua hatua. Lakini tunahitaji dhamira yenye nguvu za kisiasa miongoni mwa nchi na wafadhili kuangalia jinsi gani ya kufanya jambo hilo."

Katika Ukanda wa Sahel – ambapo karibu nchi kadhaa za mpakani mwa jangwa la Sahara kusini mwa Afrika – ziliandamwa na majanga, pamoja na kuwa siyo wa kipekee, lakini ukame wa mwaka jana uliangamiza kabisa mavuno na mifugo. Kutokana na ukame, bado kuna wastani wa kaya milioni 18 katika ukanda wa Sahel zinakumbwa na uhaba wa chakula, ikiwa ni pamoja na watoto wapatao milioni ambao wana utapiamlo mkali.

Kumekuwepo na wasiwasi unaozidi kuongezeka kuwa mavuno duni yatapatikana tena mwaka huu, na Benki ya Dunia ilionya mwishoni mwa Agosti kuwa bei ya mahindi na mtama katika maeneo ya ukanda wa Sahel tayari imeshapanda sana. Lakini kuwasili kwa mvua, pamoja na jitihada kubwa za kimataifa, kumepunguza hofu kidogo.

Kuangalia kipindi cha muda mrefu Hata hivyo, ahadi za wafadhili juu ya jitihada za kimataifa kuhusu Sahel zilifikia dola bilioni 1.6, dola zipatazo milioni 350 zilitoka Marekani na nyingi kutoka Umoja wa Ulaya. (Dola zipatazo bilioni 1.3 kati ya hizo zilikwenda katika jitihada za kukabiliana na mgogoro wa chakula, wakati nyingine zilikwenda katika jitihada zenye fedha kidogo za kukabiliana na wakimbizi ambao walilazimika kukimbia makazi yao.)

Na wakati jitihada hizo hadi sasa zinaonekana kupunguza mgogoro wa chakula mwaka huu, Gressley anasema pesa zilizotolewa zimefanya kazi ndogo kusaidia wanajamii kujiandaa kukabiliana na hali hiyo isiyozuilika.

"Ni vema kujua kuwa hatua ya mapema inaweza kuwa na matokeo chanya," Gressley anasema. "Lakini mgogoro umepata msaada wa kiasi fulani tu kwa muda fulani na kwamba unapotea; kwa kuwa na mvua nzuri, watu tayari wanazumgumzia kuhusu mambo mengine. Kwa uhakika, uchukuliwaji wa hatua za kibinadamu wa aina hii mara zote unahitajika kama kutakuwa na mapungufu ya kisiasa na kimaendeleo – na katika ukanda mzima wa Sahel, ni hakika kuna mapungufu ya kimaendeleo."

Hata katika mwaka huu wenye mavuno mazuri – kwani mwaka huu unaweza kuthibitisha kuwa robo milioni ya watoto bado wanatarajiwa kufariki katika nchi za Sahel. Tatizo hilo la kimuundo la kipindi kirefu, wataalam wanasema, ni hali ambayo inaweza kubadilika na kuwa mgogoro kamili wakati wowote ule.

Ili kuendelea na mpango wa uokozi ambao Umoja wa Mataifa na wengine wanashiriki sasa, Gressley anasema wafadhili wa kimataifa watahitaji ahadi zinazoeleweka kwa mipango ya miaka mitano au hata 10.

Hiyo ni oda kubwa, hasa wakati wafadhili duniani wanapokuza miradi yao wakati huu wa kuchukua hatua kali. Zaidi ya hapo, Umoja wa Mataifa, una sera ya kutokutoa pesa kwa zaidi ya miaka mitatu.

Hata hivyo, bado kuna wafadhili wakubwa ambao miradi ya kukabiliana na ukame katika Sahel inahitaji. Mpango muhimu zaidi unaoweza kufika mbali unaendeshwa na Tume ya Ulaya, ushirikiano ulioanzishwa Juni unaojulikana kama AGIR Sahel.

Wakati lengo la awali la ushirikiano ni katika mgogoro mkubwa wa chakula, tamko lake la awali lilikuwa ni kuangalia mbele zaidi. "Washiriki walikubaliana kuwa jitihada za pamoja na serikali na mashirika katika kanda na washirika wa kibinadamu na maendeleo zinahitajika," tamko hilo linasema kuhusu, "kushughulikia migogoro ya sasa na kupunguza kiwango cha migogoro katika siku sijazo."

Wakati Gressley anapongeza ushirika wa AGIR Sahel, anasema kuwa mchanganyiko wa sasa wa kimataifa wa lengo na mitizamo kwa serikali kadhaa za kanda ya Sahel "inaweza kutokurudiwa kama hatua hazitachukuliwa katika kipindi cha mwaka ujao.

Mtizamo wa kiusalama Kikwazo kikubwa kufuatia shinikizo la mwaka 2013 la jumuiya ya kimataifa kwa ajili ya kukabiliana na ukame katika ukanda wa Sahel kinaweza kuwa hali isiyotabirika ya Mali, ambapo tangu Machi wombwe la kiusalama na kisiasa limesababisha makundi ya waasi kuchukua udhibiti wa sehemu kubwa ya kaskazini mwa nchi.

"Masuala kama haya ya kiusalama tunayoyaona Mali ni tishio kubwa katika mfumo wetu wa kukabiliana na majanga," Gressley anaonya. "Hatari ni kwa wanasiasa kuonyesha dhamira ya kushughulikia mambo yote hayo – kufikiwa na mashirika ya kibinadamu, n.k. – na kusahau kuhusu matatizo ya muda mrefu. Kama hilo likijitokeza, tutapoteza fursa ya kushughulikia suala la usalama wa chakula na pia ubaguzi ambao umeenea sana katika Sahel nzima."

Hata hivyo bado, ufumbuzi wa kisiasa unabakia kutokuwa wa uwazi, kuna mahitaji ya wazi na ya haraka ya kibinadamu ikiwa ni pamoja na misaada ya kiufundi nchini Mali. Wakati huo huo, hali nchini Mali inazidi kuchukuliwa hatua na wapiganaji wa ugaidi, kwani nchi za Magharibi, hasa Marekani, katika wiki za karibuni zimependekeza kwa nguvu kuwa vikundi vya kigaidi, kama vile Al Qaeda katika eneo la Islamic Maghreb, vinazidi kujipenyeza katika machafuo ya nchini Mali.

"Sikubaliani kuwa Mali itakuja kufunika kuonekana kwa ukanda wa Sahel," Joel Charny, makamu wa rais wa sera za kibinadamu katika InterAction, mtandao wa mashirika ya kiraia nchini Marekani, aliiambia IPS.

"Hata hivyo, kwa mwaka ujao kuna wasiwasi halisi juu ya kama tutakuja kuikabili Mali kama suala la kiusalama badala ya kuwa suala la kibinadamu. Tutakuja kuanza kuona mashambulizi ya Marekani nchini Mali? Kama ndivyo, itakuwa vigumu sana kufanya kazi za kibinadamu huko."

Wiki iliyopita, shirika la InterAction lilitangaza kuwa wanachama wake walikuwa wakiomba zaidi ya dola bilioni kusaidia katika usalama wa chakula na lishe, ikiwa ni pamoja na kwa ajili ya eneo la Sahel.

"Tunajua kuwa katika hali kama ya Sahel unapaswa kufanya mambo yote –lazima kuwepo na uwezo wa kuchukua hatua kuokoa maisha ya watu, lakini unaweza kujaribu kuchukua hatua kwa njia ambazo zitawezesha jamii kuwa na nguvu na kuwa na uwezo wa kukabiliana na mtikisiko katika hali ya kawaida," Charny anasema.

"Lakini je mwaka 2013 utakuwa tofauti sana na, kwa mfano, miaka mitano iliyopita – je mwaka ujao utakuwa na changamoto zaidi? Pengine itakuwa hivyo au haitakuwa hivyo. Suala la msingi hapa inahitaji kuongeza jitihada mara mbili kufanya kazi katika ukanda wa Sahel kwa njia ambayo inaruhusu watu kuendesha maisha yao wenyewe." (END/2012)

 
Contact Us | About Us | Subscription | Help us Improve | News in RSS
Copyright © 2019 IPS-Inter Press Service. All rights reserved.