Inter Press Service News Agency
Friday, September 18, 2020   22:31 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions


Uhusiano Dhaifu Kati ya Kuzuia VVU Barani Afrika na Matumizi ya Njia za Uzazi wa Mpango
Na Miriam Gathigah

NAIROBI, Agosti 30, 2014 (IPS) - Katika kukimbilia kuokoa watoto wachanga kutokana na maambukizi ya VVU na kutibu mama zao, wataalam wanaonya kuwa suala la msingi katika kuzuia VVU linapuuzwa barani Afrika – matumizi ya njia za uzazi wa mpango kwa wanawake wanaoishi na VVU/UKIMWI.

Wakati huo huo inajulikana kuwa uzazi wa mpango ni nguzo ya pili ya kuzuia kwa mafanikio maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto (PMTCT), ikiwa ni pamoja na kuzuia maambukizi miongoni mwa wanawake na watoto na kutoa matunzo kwa wale walioambukziwa.

"Mahitaji ya uzazi wa mpango kwa wanawake wanaoishi na VVU mara nyingi yanawekwa nyuma ya pazia, na shabaha kuu ikiwa ni kumfanya mama na mtoto kuwa na afya nzuri," Florence Ngobeni-Allen, msemaji wa Elizabeth Glaser Paediatric AIDS Foundation, aliiambia IPS. Akiwa ni raia wa Afrika Kusini, alikutwa na VVU mwaka 1996, akapoteza mtoto wake kutokana na ugonjwa wa UKIMWI na kwa sasa ana watoto wa kiume wawili wenye afya nzuri.

Uzazi wa mpango ni muhimu katika Afrika Mashariki na Kusini, ambako maambukizi ya VVU pamoja na kiwango kikubwa cha kutokufikiwa kwa mahitaji ya uzazi wa mpango, na ambako wanawake nane kati ya 10 wenye VVU wana umri wa kuzaa, kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA).

Tafiti zinasema kuwa wanawake wanaoishi na VVU wana matamanio sawa kama siyo zaidi ya kujipatia watoto ikilinganishwa na wale wasiokuwa na VVU. Kupunguza kiwango cha uhaba wa huduma za uzazi wa mpango miongoni mwa wanawake hawa ni jambo muhimu ili kufikia lengo la kupunguza maambukizi mapya ya VVU kwa watoto kwa asilimia 90," inasema ripoti ya Umoja wa Mataifa ijulikanayo kama Women Out Loud.

Tafiti za wanawake wanaoishi na VVU nchini Kenya na Malawi zinaonyesha kuwa karibu robo tatu hawataki kupata watoto tena katika kipindi cha miaka miwili ijayo au milele, lakini ni robo tu walitumia njia za kisasa za uzazi wa mpango.

Udhaifu wa mipango

Utafiti wa shirika la Family Health International miongoni mwa wanawake wanaoishi na VVU nchini Rwanda, Kenya na Afrika Kusini ulionyesha kuwa zaidi ya nusu hawakupanga kubeba mimba zao walizo nazo sasa au hivi karibuni.

Pamoja na kuwa wanawake hao walitaka njia za uzazi wa mpango, upatikanaji wake ulikuwa mgumu. Moja ya kikwazo ilikuwa ni wafanyakazi wa afya: walikuwa hawana ujuzi wa kutoa aina mbalimbali ya njia za uzazi wa mpango kwa wanawake wanaoishi na VVU; walikuwa na imani potofu kuhusu usalama wa njia za uzazi wa mpango; wengi wao walitoa kondomu za kiume tu, pamoja na kwamba wanawake walipendelea vipandikizi na sindano, na wengi walikuwa wakitoa hukumu juu ya maisha ya kujamiiana ya wanawake hao.

"Mara nyingine manesi walisahau kuwa wanawake bado wana hamu ya kujamiiana hata kama wanaishi na VVU," anasema Ngobeni-Allen.

Kutokufikiwa kwa mahitaji ya huduma za uzazi wa mpango nchini Kenya kunafikia asilimia 25 nchini kote lakini kunafika asilimia 60 miongoni mwa wanawake wanaishi na VVU, Dk John Ong’ech, mkurugenzi msaidizi katika Hospitali ya Kenyatta aliiambia IPS.

Upatikanaji duni wa huduma za uzazi wa mpango kwa wanawake wenye VVU ambao wana uwezekano wa kufa mara sita hadi nane kutokana na matatizo ya mimba ikilinganishwa na wale wasiokuwa na VVU, "ni udhaifu katika mipango ya afya," aliiambia IPS, pamoja na kwamba ni rahisi na inafanya kazi kutoa huduma za uzazi wa mpango kuliko PMTCT.

Wanaume na mama wakwe

Mary Naliaka, ambaye anafanya kazi katika kitengo cha UKIMWI kwa watoto katika wizara ya afya nchini Kenya aliiambia IPS kuwa uzazi wa mpango unapaswa uwe sehemu ya tiba ya VVU na kutoa aina mbalimbali za njia za kupanga uzazi.

Lakini mifumo ya afya katika Mashariki na Kusini mwa Afrika mara nyingi inakabiliwa na uhaba wa vifaa na kliniki nyingi hazina miundombinu ya kutosha.

"Kutumbukiza kipandikizi kwa mwanamke kunahitaji mazingira mazuri yenye vifaa vya kuua vijidudu," Ong’ech anasema.

Sindano ni njia inayotumiwa zaidi na wanawake kwasababu wanaweza kutumia bila waume zao kujua, anaongeza.

Kukosekana kwa usawa wa kijinsia na wanawake kukosa ushawishi kunasababisha matumizi duni ya njia za uzazi wa mpango. Naliaka anasema kuwa katika utamaduni wa Kiafrika, "mama mkwe anaweza kusababisha kuvunja ndoa kama hakuna mtoto anayezaliwa."

Dorothy Namutamba, kutoka Jumuiya ya Kimataifa ya Wanawake Wanaoishi na VVU katika Afrika Mashariki (ICWEA), ambaye ofisi yake ipo Kampala, Uganda, aliiambia IPS kuwa wanawake wameumbwa kuwafurahisha waume zao.

"Kama mwanaume anadai anataka kuwa na watoto kumi ni lazima kukubali na kama hutaki atawatafuta kutoka kwingine," anasema. "Wanaume wengi hawataki wanawake kutumia uzazi wa mpango, hilo ni tatizo kubwa."

Unyanyapaa na unyanyasaji wa majumbani unazidisha tatizo. "Wanawake wanahofia kutaja kuwa wameambukizwa VVU kutokana na kuwa wanaweza kukabiliwa na unyanyasaji wa kijinsia, na hii inazuia kupata njia za uzazi wa mpango," Anthony Mbonye, kamishina wa Huduma za Afya nchini Uganda, aliiambia IPS.

Kutokana na nguvu za wanaume katika utoaji wa maamuzi kuhusu mimba, huduma za afya ya uzazi zinazoshirikisha wanandoa wawili ni muhimu, lakini "vituo vya afya vina msongamano mkubwa mno kuweza kuhudumia wanandoa wa kiume," Naliaka aliiambia IPS.

Ushinikizaji wa kufunga kizazi kwa wanawake wanaoishi na VVU nchini Kenya, Malawi, Namibia, Afrika Kusini na Zambia, huku kukiwepo na kesi mahakamani, kunazidisha utata wa suala la haki na mahitaji ya uzazi na VVU.

"Hii inaaibisha sekta ya afya," anasema Naliaka. Hata hivyo, anaongeza, "kupitia kesi hizi, sekta ya afya na umma umeelewa kuwa wanawake hawa wana mahitaji ya uzazi kama ilivyo kwa wenzao wasiokuwa na virusi."

Eneo moja la kutolea huduma

Ili kusonga mbele, wataalam wanapendekeza kuunganisha VVU, uzazi wa mpango na huduma za uzazi na watoto wachanga ili kuokoa muda kwa watumiaji na wafanyakazi wa afya.

Nchi saba za Kusini mwa Afrika zimeshaanzisha eneo moja la kutolea huduma ambapo wanawake wanaweza kupata ARVs, kupima kansa ya kizazi, ushauri wa kunyonyesha na uzazi wa mpango kwa wakati mmoja, chini ya jengo moja, mara nyingine katika chumba kimoja chenye mhudumu wa afya.

Kuunganisha huduma kunaokoa gharama na kunaleta ufanisi, inasema UNFPA. (END/2014)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The download of the specified resource has failed.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>