Inter Press Service News Agency
Tuesday, July 16, 2019   05:15 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions


Uhaba wa ARV Waukabili Mfumo wa Tiba wa Msumbiji
Na Amos Zacarias

MAPUTO, Agosti 25, 2014 (IPS) - Uhaba mkubwa wa madawa ya kupunguza makali ya Ukimwi nchini kote Msumbiji unatishia afya na maisha ya mamia kwa maelfu ya watu wanaoishi na VVU ambao wameshaanza kutumia madawa hayo.

Baadhi ya watu 454,000 wanatumia madawa ya kupunguza kasi ya Ukimwi (ARV), au sawa na moja ya tatu ya watu milioni 1.6 ambao wanaishi na VVU nchini Msumbiji mwaka 2013, kwa mujibu wa takwimu za serikali.

"Wagonjwa wetu wanalalamika kuwa hawapati dozi za kutosha," anasema Judite de Jesus Mutote, rais wa Hi Xikanwe ("tupo pamoja," katika lugha ya Kishangani), kikundi ambacho kinasaidia watu kupata tiba ya ARV mjini Maputo.

Ili ARVs kuwa na ufanisi, vidonge lazima kunywewa kila siku wakati unaofanana. Kukatiza kutumia dawa kuna madhara makubwa kwa afya.

"Kuacha kutumia dawa kunasababisha kuongezeka kwa idadi ya virusi, magonjwa nyemelezi na kunaleta usugu kwa madawa, huku wagonjwa wakihitaji madawa yenye nguvu na ya gharama kubwa, ambayo wakati mwingine nchi inakuwa haina uwezo wa kuyanunua," Jose Enrique Zelaya, mkuu wa Mpango wa Pamoja wa Kupambana na Ukimwi wa Umoja wa Mataifa (UNAIDS) nchini Msumbiji, aliiambia IPS.

Taarifa za vyombo vya habari nchini kote, hasa katika majimbo ya kati na kaskazini, zinaonyesha kuwa watu wanakwenda mara kadhaa kliniki huku wakiwa wanatumia fedha na muda wao lakini wanarejea wakiwa hawana madawa au wakiwa na madawa ya kutumia kwa wiki mbili badala ya mwezi mzima.

Wagonjwa katika maeneo ya vijijini wanaathirika zaidi. "Katika maeneo ya vijijini, umbali kati ya kliniki na makazi ya wagonjwa ni mrefu sana, na barabara ni tatizo," anathibitisha Zelaya.

Katika jimbo la kati la Sofala, mashambulizi kutoka kwa kikundi cha waasi yamesababisha kufungwa kwa njia kuu ya barabara, na hivyo kulazimisha magari ya abiria kuendeshwa katika misafara inayoongozwa na wanajeshi, na hivyo kuzuia usambazaji wa bidhaa muhimu kama vile madawa.

Lakini hata Maputo, mji mkuu wa nchi, haujaachwa katika uhaba wa ARV, kama ambavyo inathibitishwa na wanachama wa Hi Xikanwe.

Baadhi ya wagonjwa wanaamua kununua madawa kwa bei ya juu katika masoko yasiyokuwa rasmi, huku wakiwa hawana uthibitisho wa ubora wake. Wengi wanadhani kuwa ARVs kutoka kliniki za serikali zinaishia katika masoko yasiyokuwa rasmi.

Salmira Ngoni*, mama mwenye umri wa miaka 26 ambaye anaishi na VVU, aliweza kuvumilia miezi ya uhaba wa madawa katika kliniki ya Ndlavela, jijini Matola, kama kilomita 20 kaskazini mwa Maputo. Mwezi Disemba alitoa hongo kwa mfamasia ili kumuuzia vidonge 15 vya ARV bila hata ya kujali dozi kwa gharama sawa na dola 10 za Kimarekani.

Mwezi Januari, Ngoni aliyekuwa amechanganyikiwa alichukua hatua kali zaidi: aliachana na matumizi ya kliniki ya serikali na kujiunga na mpango wa DREAM kwa ajili ya watu wanaoishi na VVU, unaoendeshwa na Jamii ya Wakatoliki ya Sant’Egidio. DREAM haijawahi kupatwa na uhaba wa madawa ya ARV.

Hata hivyo, suala la uhaba wa madawa siyo jipya nchini Msumbiji.

"Kimsingi, tatizo hilo linatokana na mipango mibovu ya wizara ya afya na kuwa na mchakato wa kusambaza madawa kulingana na mahitaji," anasema Zelaya.

Mutote anakubaliana: "Tunaambiwa madawa yanahifadhiwa katika ghala la wizara ya afya lakini tatizo ni usambazaji. Hawana usafiri kwenda katika kliniki za afya."

Ripoti ya mwaka 2010 ya Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) ilitambua changamoto za utoaji wa huduma nchini Msumbiji katika "manunuzi, usambazaji na uhifadhi wa madawa na bidhaa za madawa. Miundombinu duni inaweza kusababisha ucheleweshaji na kuathiri ubora wa madawa kutokana na kuanikwa katika joto."

Kwa mujibu wa WHO, uhaba nchini humo unaathiri "matumizi sahihi ya madawa kutokana na uwezo mdogo wa kusambaza madawa katika ngazi ya kliniki na kuyasambaza katika ngazi ya maduka ya madawa."

Msumbiji ilikuwa na uwiano wa wafamasia 5.6 kwa kila watu 100,000 mwaka 2010, ilisema ripoti hiyo, moja ya uwiano mdogo zaidi miongoni mwa nchi maskini.

Kengele inalia kutoa onyo

Uhaba wa madawa unapungua, lakini kiasi kinachoongezeka kinawashtua wafadhili wa kigeni, ambao wanachangia kiasi kikubwa cha fedha katika bajeti ya Ukimwi.

Mwezi Aprili, kwenye mkutano kwa waandishi wa habari, Balozi wa Uholanzi Frederique de Man, mwakilishi wa Washirika wa Afya nchini, alizungumzia "haja ya umma kununua madawa kutoka kwa wauzaji wasiokuwa rasmi kwasababu idara ya afya mara kwa mara inakosa madawa au inapata madawa ambayo yamekwisha muda wake".

De Man aliitaka wizara ya afya kusikiliza malalamiko kutoka kwa watu na mashirika yasiyo ya kiserikali - NGOs, na kuongeza usambazaji wa madawa.

Suala la kushtusha zaidi ni uhaba wa ARV kutishia mpango wa Msumbiji kuanza kutumia Mpango B+, mpango wa kutoa tiba ambao umependekezwa na WHO kwa ajili ya wanawake wanaoishi na VVU.

Mpango B+ ni mpango wa kutoa madawa ya ARV kwa mama wajawazito bila kujali idadi yao ya chembechembe za CD4.

Mwaka 2013, karibu wanawake wajawazito 85,000 walipatiwa ARVs kuzuia maambukizi kwenda kwa watoto wao. Kati ya hawa, nusu yao walianzishiwa matumizi ya madawa katika Mpango B+. Hii inamaanisha wanatakiwa kupata vidonge 30 kwa mwezi kwa maisha yao yote.

"Ni muhimu kuweka wanawake hawa katika tiba lakini siyo rahisi kutokana na umbali mrefu kati ya kliniki na jamii," alisema Guillermo Marquez, mtaalam wa masuala ya VVU katika Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa mjini Maputo.

Huku kukiwa na maambukizi mapya 56,000 miongoni mwa wanawake mwaka 2012, mahitaji ya kupata tiba ya ARV yataendelea kuongezeka.

Kuhusu watoto, 12,600 waliambukizwa mwaka 2013, kwa mujibu wa takwimu za serikali – hali inayoonyesha kuboreka kwani mwaka uliotangulia watoto 14,000 walipata maambukizi mapya.

Msumbiji ina lengo la kupunguza idadi ya maambukizi ya VVU miongoni mwa watoto hadi kufikia chini ya asilimia 2015.

Lakini Zelaya ana wasiwasi kama lengo hili linaweza kufikiwa kwa wakati. "Ili kufikia lengo hili, madawa lazima yawe yanapatikana, kama sivyo linaweza lisifikiwe."

*Jina limefichwa kulinda siri za mtu binafsi (END/2014)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The download of the specified resource has failed.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>