Inter Press Service News Agency
Wednesday, November 21, 2018   16:09 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions

Kukabiliana na Sheria ya Kupinga Ushoga Nchini Zimbabwe

Na Busani Bafana

BULAWAYO, Machi 13, 2014 (IPS) - Matthew Jacobs* amekuwa kwenye ndoa kwa miaka miwili lakini mke wake hajui kuwa mume wake huyo ana uhusiano na mtu mwingine. Kama siri yake ingebainika, inaweza kusababisha yeye kufungwa jela. Uhalifu wake ni nini? Ni kuwa na mahusiano ya jinsi moja.

Zimbabwe imepiga marufuku mahusiano ya watu wa jinsi zinazofanana. Hata kama katiba hiyo mpya itahakikisha haki kama zile za usawa na kutokubaguliwa kwa watu, iko kimya katika haki maalum kama zile za ushoga. Na ni hatari, kama siyo suala linaloua, kuwa shoga nchini Zimbabwe – nchi ambako uhusiano wa aina hiyo ni zaidi ya kuwa mwiko. "Haki za kujamiiana ni suala la kufa na kupona, changamoto ni kupata nafasi salama ambapo watu wanaweza kuishi maisha yao wanayopenda," anasema Mojalifa Mokoele, msemaji wa SRC.

"Nitafanyaje? Ilibidi nioe tu kwasababu ni suala ambalo lilitarajiwa kwangu mimi kulifanya hata kama nilikuwa na uhusiano na mwanaume mwenzangu. Ilibidi niishi maisha haya na ili kuweza kuishi," Jacobs anaiambia IPS. Jacobs ni mmoja tu kati ya mashoga wengi ambao wanalazimika kuishi maisha ya aina hiyo katika taifa hili la kusini mwa Afrika kwani wanajaribu kuzuia unyanyapaa, kubaguliwa na kukamatwa. Siyo suala la siri kuwa rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, ni mkosoaji mkuu wa ushoga na ameshatoa idadi kadhaa ya matamshi makali dhidi ya ushoga kwa miaka kadhaa. Mwezi Julai 2013, alimkosoa mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel Askofu Mkuu Desmond Tutu kuhusu kuunga mkono haki za mashoga na kusema: "Haiwezekani, haiwezekani, haiwezekani kwetu sisi kuunga mkono ushoga nchini Zimbabwe." Mwanaharakati wa kijamii na ofisa mtendaji mkuu wa Habakkuk Trust, Dumisani Nkomo, anaiambia IPS wakati kila raia ana haki ya kutambuliwa utu wake, maisha binafsi na kupata haki zote, katika jamii ya kihafidhina kama Zimbabwe, bado ni vigumu kwa ushoga kukubalika kwa wengi. "Siamini kuwa mashoga wanapaswa kubaguliwa au kufunguliwa mashitaka kwasababu kama ilivyo kwa kila mtu, wao pia ni binadamu," Nkomo anasema. "Nchi yetu ni ya kihafidhina, wakati tunaposhinikiza ajenda hiyo mtu anadharauliwa na kutengwa na jamii. Jambo ambalo kila mtu anafanya katika chumba chake cha kulala siyo jambo la kulifahamu, lakini mara tu utakapoleta jambo la siri machoni mwa umma linakuwa ni tatizo," Nkomo anasema. Ni jambo la kusikitisha ambalo limevutia kuanzishwa kwa Kituo cha Haki za Kujamiiana (SRC), shirika la haki za binadamu lenye makazi yake jijini Bulawayo ambalo linafanya kazi ya kutetea haki za jamii ya mashoga, ambao ni pamoja na wanaume wanaofanya mapenzi na wanaume wenzao, wanawake wanaofanya mapenzi ya jinsi moja, wafanyabiashara ya ngono na kukuza haki za kujamiiana za jamii nzima. Ofisa Mipango wa SRC Nombulelo Madonko anaiambia IPS kuwa kituo hicho kimeweka kumbukumbu za kesi za kudhalilishwa kwa wafanyabiashara ya ngono, wanawake wanaofanya mapenzi ya jinsi moja na mashoga ambako kunafanywa na polisi. "Watu wanapozungumza kuhusu wafanyabiashara ya ngono na mashoga, wanasahau kuwa hawa ni binadamu wa kawaida, ni mama watoto, ni wake za watu, ni baba watoto, ni dada, ni kaka na ni wanaume. Kutokana na hali za maisha yao wameonekana kama siyo watu na sasa hawana haki yoyote," anasema Madonko. SRC ina imani kuwa haki za kujamiiana zinapaswa kuwa sehemu ya jamii pana na wala siyo mwiko kwasababu hakuna jambo la kuonea aibu suala la kujamiiana na vitendo vya kufanya mapenzi miongoni mwa watu wazima. Kwa mujibu wa msemaji wa kituo hicho, Mojalifa Mokoele, kuna kukosekana kwa uelewa wa haki ya kujamiiana nchini Zimbabwe. "Katiba nchini Zimbabwe iko kimya juu ya mahusiano ya kujamiiana lakini inapinga ushoga na ndoa za jinsi moja. Siyo mashoga wote wanataka kuwa na ndoa, lakini tunataka mahusiano yetu kukubaliwa na kutambuliwa. Wanachokitaka wao ni kuishi maisha yao kikamilifu, lakini jambo hilo ni vigumu kulitaka katika jamii ambayo kwa haraka inaweza kutoa maamuzi lakini inaweza kukubali jambo polepole mno," Mokoele anaiambia IPS katika mahojiano maalum ofisini mwake. "Haki za kujamiiana ni suala la kufa na kupona, changamoto kubwa ni kupata nafasi salama ambapo watu wataishi maisha wanayotaka, lakini wanasiasa wametumia suala la ushoga na kila wanalosema limekuwa ndiyo sheria, ndiyo haki," anasema Mokoele. Kuwa shoga kunaleta mzigo mwingine linapokuja suala la kupata haki nyingine kama vile uwakilishi wa kisheria, elimu na huduma za tiba. "Nawezaje kuelezea kwa nesi mpasuko wenye maumivu katika makalio yangu bila kuulizwa niliupataje mpasuko huo?" Gideon Jones* anaiambia IPS. Anasema kuwa pamoja na changamoto hizi familia yake inatambua hali yake na hawana shida na hali hiyo. Wananiunga mkono na kunipa moyo wa kutafuta maisha kutimiza ndoto zangu za kuwa mwana mashairi. Sian Maseko, mkurugenzi wa SRC, anaiambia IPS: "Haki za kujamiiana ni haki za kibinadamu na hakuna mtu ambaye anapaswa kufunguliwa mashitaka kutokana na kile anachopenda." Shirika la Wanasheria wa Haki za Binadamu Zimbabwe (ZLHR) limewakilisha Chama cha Mashoga Nchini Zimbabwe (GALZ), katika kesi za haki za binadamu za mashoga zinazoendelea nchini humo. Mwenyekiti wa GALZ Martha Tholanah alikamatwa mwaka 2012 na kukabiliwa na mashitaka ya kuendesha shirika ambalo halijasajiliwa baada ya polisi kuvamia ofisi za shirika hilo na kupora vifaa vya kieletroni na nyaraka mbalimbali. Mwezi Januari, Mahakama Kuu ya Zimbabwe ilitoa amri kuwa vifaa vilivyochukuliwa virejeshwe na kuwa GALZ siyo shirika la hiari binafsi na hivyo haikupaswa kusajiliwa kwa mujibu wa Sheria ya Mashirika Binafsi ya Hiari. "Inatia shaka kuwa baadhi ya mamlaka nchini Zimbabwe yanazidi kuwa wabaguzi wa GALZ na watu ambao wanajitambulisha kama mashoga," msemaji wa ZLHR, Kumbirayi Mafunda, anaiambia IPS. "Udhalilishaji wowote ule na kufunguliwa mashitaka kutokana na msimamo wa kujamiiana ni janga kubwa na pia ukiukwaji wa sheria za haki za binadamu za kimataifa," anasema. * Majina yamehifadhiwa kuficha kutambuliwa kwa vyanzo vya habari. (END/2014)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The element 'html' is used but not declared in the DTD/Schema.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>