Inter Press Service News Agency
Tuesday, June 19, 2018   19:13 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions


Ujumbe wa VVU Nchini Hauwafikii Vijana
Na Dorine Ekwe

YAOUNDÉ, Novemba 29 2013 (IPS) - Akiwa anatabasamu la kuvutia Beatrice M.* anasema anaishi kwa kaulimbiu "maisha ni mafupi lakini ni mazuri — yaishi kwa ukamilifu wake." Mama wa umri wa miaka 20 ambaye anaishi na VVU anakataa kushindwa na hali yake inayomkabili.

Beatrice, mwanafunzi wa mwaka wa pili wa sayansi ya jamii katika Chuo Kikuu cha Yaounde I, alijikuta akiwa na ujauzito na akiwa ameambukizwa VVU alipokuwa na umri wa miaka 18. "Daktari aliponiambia taarifa hizo kwa mara ya kwanza, nilihisi maisha yangu yamekwisha. Lakini daktari wangu wa magonjwa ya wanawake aliniweka katika matumizi ya kutumia madawa ya kurefusha maisha aina ya Zidolan ili kuzuia mamabukizi ya kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto na aliniambia hali ingekuwa safi," anaiambia IPS. Daktari wake alikuwa sahihi na binti yake ambaye ana umri wa miaka miwili sasa hana maambukizi ya VVU. Beatrice anakumbuka: "Mimba hii ni ya kujitakia. Rafiki wangu wa kiume alitaka niitoe, lakini nilikataa. Nilipomweleza kuhusu kuambukizwa na VVU, alisema alishakwenda kwenye vipimo na akaonekana hana VVU. Halafu akanitelekeza." Wakati huo alikuwa na mimba ya miezi mitano. Beatrice ana imani kuwa rafiki wake wa kiume mwenye umri wa miaka 25 — ambaye alikuwa mwanafunzi mwenzake katika chuo hicho kikuu — ndiye aliyemwambukiza ugonjwa. Alisema alikuwa bikira wakati alipokutana naye. Kwa mujibu wa Flavien Ndonko, mtaalam wa jamii katika Shirika la Maendeleo ya Ujerumani au GIZ, inashangaza kuwa asilimia 20 hadi 30 ya watoto wa kike kati ya miaka 15 na 24 nchini Camroon wanashika mimba zisizotarajiwa. Ripoti ya kimataifa ya mwaka 2013 ya Mopango wa Pamoja wa Umoja wa Mataifa wa Kupambana na UKIMWI (UNAIDS) inasema kuwa watu wapatao 600,000 au asilimia 4.2 nchini Cameroon kati ya wakazi milioni 19 wanaishi na VVU. Wanawake na vijana ni makundi ambayo yameathirika zaidi. Taifa hili la Afrika Magharibi ni miongoni mwa nchi 20 zinazopewa kipaumbele na UNAIDS katika bara la Afrika, na limekuwa na kushuka kidogo sana kwa maambukizi mapya. Beatrice alijifunza kuhusu takwimu hizi baada ya kukuta kuwa ameambukizwa VVU. "Wakati wa mahusiano yetu, hatujawahi kudhani kuwa tungesababisha ujauzito wala kupata UKIMWI. Niliwahi kusikia mambo hayo, lakini sikuweza kuhisi kuwa yangeweza kunipata mtu kama mimi." Wakati anasoma sekondari hajawahi kuwa na nia ya kuhudhuria Mpango wa Elimu ya Maisha na Mapenzi (ELL), elimu ya maarifa iliyotolewa katika shule zote za sekondari nchini kote. Mfanyakazi wa jamii Arlette Ngon anasema nchi inahitaji mfumo mpya wa kuhamasisha. "Mbali na masomo ya sayansi, mpango wa ELL ni wakati pekee ambapo maambukizi ya kujamiiana na UKIMWI yalijadiliwa kwa kina mashuleni. Lakini ujumbe wake unaonekana haukuwafikia vijana." Yvonne Oku, kutoka Mtandao wa Shangazi wa Kitaifa (RENATA), ana imani kuwa kuna kazi zaidi inahitaji kufanyika kupunguza kiwango cha maambukizi mapya. RENATA, asasi isiyokuwa ya kiserikali inaelimisha vijana jinsi ya kuzuia mimba na VVU kupitia kwa "shangazi", ambao ni mama wenye umri mdogo ambao wamepatiwa mafunzi ya afya. Aubin Ondoa, mtaalam wa masuala ya jamii, anaelezea IPS kuwa hatari kubwa kwa watoto wa kike ni kuanza kufanya mapenzi wakiwa na umri mdogo ikiwa ni pamoja na kukosa taarifa. Kwa mujibu wa Shirika la Idadi ya Watu la Umoja wa Mataifa, umri wa wastani wa kuanza mapenzi nchini Cameroon ni miaka 15.8, wakati msichana mmoja kati ya watatu mwenye umri wa kati ya miaka 20 hadi 24 amekuwa na mtoto kabla hajafikisha miaka 18. "Zaidi ya hapo, watoto wa kike wanalengwa zaidi na wanaume watu wazima ambao wanawarubuni kwa kuwapa pesa," Ondoa anaongeza. Kwa vijana wa kike ambao hawana taarifa na hawana au kipato chao ni kidogo, matokeo ya kufanya ngono isiyokuwa salama ni kupata mimba na VVU. Beatrice kwa sasa anatumia kondomu akifanya mapenzi na mpenzi wake. Yupo katika mahusiano na mwalimu wa shule ya sekondari ambaye hana VVU, anajua kuwa mwanamke huyo anaishi na VVU lakini anataka kumuoa. Lakini mwanamke huyo amekataa kwani anaweza kumwambukiza. Ana wasiwasi kuwa kama wakioana hawatakubali tena kutumia kondomu. Kizazi Chanya — shirika la kupambana na UKIMWI lililoundwa mwaka 1998, ambalo lina wanachama 60 wengi wao wakiwa walimu — limekuwa chanzo cha msaada kwa Beatrice.Kundi hilo lilimsaidia kuweza kuishi na hali ya VVU. Mwanamke huyo kijana ameamua kutunza siri ya hali yake ya maambukizi. "Wazazi wangu hawapo tayari; napendelea kuwaacha katika giza. Nina wasiwasi kunyanyapaliwa," anasema. Kwasababu anaishi na dada wake wawili, inabidi awe msiri mno ili wasigundue hali yake. "Ninajificha sana. Itakuwa vigumu kama mtu akiniona nakunywa dawa kila mara," anasema. Anamsafirisha mtoto wake ambaye anaishi na wazazi wake kijijini kuja katika mji mkuu wa nchi wa Yaoundé kufanyiwa vipimo vya afya yake. Katika kijiji, anasema, "hakuna kitu kinachoitwa usiri wa kitabibu." Nchini Cameroon, tiba ya kukabiliana na makali ya VVU inatolewa bure; anatakiwa kulipia vipimo vya damu na CD4 mara mbili kwa mwaka, ambavyo vinagharimu dola 34. "Ingekuwa ngumu sana kama ningetakiwa kulipia kila kitu," anasema. Wagonjwa katika maeneo ya vijijini hawana bahati sana. Mara nyingi wanatakiwa kusafiri kwa miguu kwa kilomita 44, kupitia msituni ili kufika katika kituo cha afya. Beatrice anampenda mtoto wake mchanga wa kike na angependa kuwa na watoto wengi zaidi, lakini anatamani wafanyakazi wa afya wangefanya kazi kwa weledi zaidi. "Nilichanika wakati wa kujifungua, lakini mkunga alikataa kunishona. Pia alikataa kumpeleka mtoto wangu kufanyiwa vipimo," anasema huku akitokwa na machozi. Kwa upande wake, tabia hii haihusiani na jambo jingine zaidi ya unyanyapaa na ni jambo ambalo halitaki kabisa katika kaulimbiu yake ya kuishi maisha ya ukamilifu. (END/2013)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The element 'html' is used but not declared in the DTD/Schema.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>