Inter Press Service News Agency
Tuesday, June 19, 2018   19:10 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions


Mabadiliko ya Tabia Nchi Yatoa Somo - Climate Change Teaches Some Lessons
Na Nasseem Ackbarally

PORT LOUIS, Oktoba 9 (IPS) - Utalii, kilimo, uvuvi, maji ya kunywa – mabadiliko ya tabia nchi yanatishia misingi ya jamii na uchumi wa Mauritius. Wakati taifa hilo la kisiwa katika Bahari ya Hindi linaandaa mikakati ya kukabiliana na hali hiyo, linafanya kazi kuhakikisha kizazi kijacho kinajikita kabisa katika kanuni za maendeleo endelevu.

Ikizinduliwa Jul. 5, Sera ya Taifa ya Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchi (NCCAPF) ilihusisha masuala ambayo yanajulikana lakini yanayotia hofu juu ya mustakabali wa baadaye. Nusu ya fukwe katika taifa hilo lenye mvuto mkubwa wa watalii zitapotea ifikapo mwaka 2050, kutokana na kuzama kutokana na bahari inayozidi kuongezeka kina chake na kuongezeka kwa kasi na nguvu ya upepo utakaojitokeza mara kwa mara. Rasilimali za maji safi zinaweza kupungua kwa asilimia ipatayo 13 wakati mahitaji yataongezeka kwa kiasi kikubwa.

"Tunashtushwa kujifunza kuwa kisiwa chetu kizuri au sehemu ya kisiwa hiki – inaweza kutokomea kutokana na kupanda kwa kina cha bahari," mwanafunzi Felicia Beniff aliiambia IPS wakati akitoka katika darasa la mazingira na mabadiliko ya tabia nchi akiwa na rafiki zake wanne. "Tuna mashaka. Tuna miaka mingi ya kuishi. Tutakwenda wapi?"

Mwanafunzi huyo wa umri mdogo katika darasa la Shule ya Sekondari ya MEDCO Cassis katika mji mkuu wa Mauritius wa Port Louis ni miongoni mwa robo ya wanafunzi milioni katika kisiwa hicho ambao watafundishwa kanuni za maendeleo endelevu.

Mauritius inafanya kazi kwa bidii kusahihisha mbinu zisizokuwa endelevu, hasa kwa kupitia Maurice Île Durable.Kuelimisha vijana juu ya maendeleo endelevu ni sehemu ya ndoto hii ya muda mrefu ya kujenga uchumi mpya ambao unazingatia ikolojia.

Katika Sekondari ya Rabindranath Tagore Statehuko Ilot, kaskazini mwa Mauritius, wanafunzi wanaingiza takataka katika shimo kwa ajili ya kuziacha zioze.

"Tunakusanya chupa za plastiki. Tunazima taa na kiyoyozi tunapoondoka darasani. Tunafungua madirisha ili kuruhusu hewa kuingia madarasani. Hii inasaidia kupunguza gharama za shule. Pia tunapanda miti," mmoja wa wanafunzi, Ashootosh Jogarah, aliiambia IPS.

Rafiki yake, Varounen Samy, aliiambia IPS kuwa kwa sasa "wamebadilika mitizamo yao kuhusu mazingira."

Mahen Gangapersad, mwalimu katika shule hiyo, ana imani kuwa raia wa Mauritius wamelichukulia suala la mazingira kwa mtizamo hafifu zaidi bila kutambua madhara yake katika maliasili. Mpango mpya wa elimu unalenga katika kusahihisha hali hii. "Afadhali kuchelewa kuliko kutokufanya kabisa," aliiambia IPS.

Upandaji wa miti, kufunga mitambo ya jua kwa ajili ya nishati mbadala, bustani, bustani za mazingira ya nyumbani, utengaji wa taka, utengenezaji wa mbolea kwa kutumia taka, uvunaji wa maji ya mvua na udhibiti wa maji kwa sasa ni jambo linalojitokeza katika shule nyingi. Mpango huo ni kuwezesha wanafunzi wote kujua hifadhi ya mazingira.

"Kwa hiyo kwa sasa tunafikia watu 250,000 na zaidi," Veenace Koonjal, mshauri maalum wa Wizara ya Elimu aliiambia IPS. Ana imani mafunzo haya yatakuwa na matokeo makubwa katika kutoa uelewa miongoni mwa watu milioni 1.2 juu ya nini wanaweza kupeleka nyumbani kwa familia zao na jamii kwa ujumla.

"Mabadiliko ya tabia nchi yanadhoofisha uchumi, misingi ya kijamii na kimazingira ya kisiwa hiki," alisema Waziri wa Mazingira na Maendeleo Endelevu wa Mauritius Deva Virahsawmy, wakati wa uzindizu wa NCCAPF.

Uzinduzi wa mkakati wa kisera ambao maandalizi yake yamekamilika ulifanyika pamoja na uzinduzi wa Kituo cha Taarifa za Mabadiliko ya Tabia Nchi cha Port Louis, mpango ambao ungekusanya taarifa za ndani na za kimkoa juu ya mabadiliko ya tabia nchi na kuzifanya kupatikana kwa kila mtu – wanasayansi, wahandisi, wasanifu wa majengo, ikiwa ni pamoja na wakulima na wanafunzi.

Kuimarisha na kupanua maarifa, ufahamu na taarifa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi ni jambo la msingi katika kukabiliana na ongezeko la joto kisiwani humu. Mauritius, kama ilivyo kwa mataifa mengine ya visiwa, yanaweza kutegemea kubeba mzigo mzima wa mabadiliko ya tabia nchi pamoja na kuchangia kwa kiasi kidogo katika uzalishaji wa hewa ukaa.

Zaidi ya hapo, mkakati wa sera unakubali kuwa jiografia ya kisiwa hicho inazuia kile ambacho kingeweza kufanyika kukabiliana na madhara mabaya ya ongezeko la joto duniani katika uvuvi na ardhi ya mwambao wa pwani, utalii na kilimo.

Khalil Elahee,mwenyekiti wa Ofisi ya Usimamizi wa Kiufanisi wa Nishati, ana imani kuwa watu wameanza kutambua madhara makubwa ya mabadiliko ya tabia nchi.

"Watu wanataka maendeleo endelevu. Kwa hiyo ni suala muhimu kuanza njia mpya za maisha na kuendeleza kisiwa chetu, " aliiambia IPS.

"Kila tunachokifanya kinaweza kisitutosheleze lakini hatua zinazochukuliwa na Mauritius katika mpango wake wa elimu ya mabadiliko ya tabia nchi inasaidia kukabiliana na madhara ya mabadiliko hayo katika kisiwa," Elahee alisema.

Virahsawmy alisema elimu ya mabadiliko ya tabia nchi ingewezesha Mauritius kuimarisha nguvu zake za kukabiliana na hali hiyo katika sekta muhimu za uchumi wake na kuondokana na hatari na kuzuia kupotea kwa maisha ya watu na mali zao.

Mauritius imeshapata tayari dola milioni tatu kutoka kwa Mpango wa Afrika wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchi – unaofadhiliwa na Serikali ya Japan chini ya Mpango wake wa "Cool Earth Partnership for Africa" – katika kuunganisha na kuingiza njia za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi katika mikakati ya kitaasisi na sera muhimu za maendeleo.

Ofisa katika Wizara ya Mazingira na Maendeleo Endelevu aliiambia IPS kuwa mradi wa Tathmini ya Mahitaji ya Kiteknolojia (TNA) pia utakelezwa mwaka huu. Utapata msaada wa kiufundi kutoka Kitengo cha Teknolojia, Viwanda na Uchumi cha Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa, na katika Kituo chake cha Risoe nchini Denmark. Unafadhiliwa na Mfuko wa Mazingira wa Kimataifa katika kiwango cha dola 120,000.

Lengo kuu la TNA ni kuziba pengo kati ya kubainisha teknolojia zinazofaa na kuandaa mpango wa utekelezaji. Lengo ni kuruhusu Mauritius kutekeleza teknolojia za kupunguza uzalishaji wa hewa ukaa na kusaidia njia za kupunguza madhara ya mabadiliko ya tabia nchi jambo ambalo linakwenda sawa na vipaumbele vya maendeleo vya kitaifa.

Serikali ina matumaini kupata fedha zaidi kwa ajili ya jitihada za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kutoka Mfuko wa Hali ya Hewa ya Kijani, mfuko wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi wa Umoja wa Mataifa pamoja na kutoka kwa GEF.

Mbali zaidi na darasani, mipango mingine mingi inayoendeshwa na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali inajazia kile ambacho watoto hawa wadogo wanajifunza mashuleni. Mpango wa "Youth be Aware" unaondeshwa na Shirika la Msalaba Mwekundu la Mauritius, kwa mfano, unashirikisha vijana 600 katika kukabiliana na hatari inayoweza kuletwa na mabadiliko ya tabia nchi katika kisiwa hicho. (END/2013)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The element 'html' is used but not declared in the DTD/Schema.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>