Inter Press Service News Agency
Monday, June 18, 2018   10:46 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions


Raia wa Cameroon Waona Mpango wa REDD - Cameroonians See REDD
Na Monde Kingsley Nfor

YAOUNDE, Oktoba 9 (IPS) - Kukosekana kwa uhakika wa umilikaji wa ardhi na upatikanaji wa ardhi zenye misitu ni kizuizi kinachoweza kuzuia utekelezaji wa mpango wa pamoja wa Umoja wa Mataifa wa Kupunguza Uzalishaji wa Hewa Ukaa Unaotokana na Uteketezaji wa Misitu na Ukataji Miti (REDD) nchini Cameroon.

Katika eneo la Adjab, kijiji cha raia wazawa katika mkoa wa kusini mwa Cameroon, Chifu Marcelin Biang aliiambia IPS kuwa anahisi sheria zilizopo zinasukuma wakazi wa maeneo hayo kuangamiza misitu ili waweze kuwa na msingi wa kutoa madai yao.

Kufuatia mgogoro wa ardhi kati ya wakazi wa Adjab na kamuni ya mbao, kipande cha ardhi yao kilirejeshwa kwao – lakini kwa masharti kuwa wanakijiji wanaonyesha uthhibitisho kuwa wanatumia ardhi kufanya vipato vyao kuwa endelevu.

Biang alisema kuwa wanategemea misitu kwa ajili ya uwindaji wanyama, kupanda mbogamboga na kukusanya kuni. Kulima katika ardhi kubwa siyo sehemu ya utamaduni wao, lakini sasa lazima wajifunze jinsi ya kupanda miweze na miti ya mpira ili waendeleze ardhi yao.

"Tumechanganyikiwa juu ya tufanye nini," alisema Biang. "Walitutaka kuhifadhi msitu, lakini tutafanya hivyo lini, wakati wakataji wa miti kwa ajili yam abo wamefika."

"Hata kama REDD haitatuletwa pesa, itatuletea utawala bora." - Augustine Njamnshi, wa NGO ya Mandeleo ya Rasilimali za V iumbe Hai na Hifadhi ya Mazingira Cameroon, alisema.

Mipango ya Cameroon ya utekelezaji kwa mafanikio wa miradi ya REDD utazuia nchi kutatua changamoto za muda mrefu katika kusimamia misitu na rasilimali nyingine.

Mwezi Januari, mipango ya mpango wa REDD kwa taifa hili la Afrika ya kati ilipitishwa na Mfuko wa Kusimamia Hewa Ukaa kwa Kutumia Misitu (FCPF) uliopo chini ya benki ya Dunia .

"nchi zenye misitu zinaweza kupata malipo kutokana na kuhifadhi hewa ukaa, lakini hili lazima litokane na upangaji wenye ufanisi na utekelezaji wa Mchanganuo wa Maandalizi (RPP)," Serge Menang, mtaalam mwandamizi wa masuala ya mazingira wa FCPF nchini Cameroon aliiambia IPS.

FCPF ilipatia Cameroon msaada wa dola milioni 3.6 katika kutekeleza mpango wake wa RPP, ambao unaandaa mkakati wa kitaifa.

Mataifa ya Kusini yanatarajia kupata malipo makubwa kutokana na wachafuzi wa hali ya hew awa Kaskazini kutokana na Kusini kuhifadhi mazingira na kuongezeka kwa misitu. Miiti inashikilia kiasi kikubwa cha hewa ukaa, ambayo kama ingetolewa ovyo katika anga, ingechangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa joto duniani.

Mipango ya REDD inataka kupelaka kiasi Fulani cha faida ya kuhifadhi misitu kwa wahifadhi kwa njia ya stakabadhi za hew ukaa, ambazo zinaweza kuuzwa kwa makampuni yanayochafua anga katika nchi za Kaskazini ambayo yangependa kupunguza kiasi cha athari zinazotokana na uzalishaji wao wa hewa ukaa. REDD inakwenda mbali zaidi na kuhusisha kilimo.

"Mkakati wa REDD umejikita katika dira ya taifa ya kuifanya REDD kuwa chombo cha maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika taifa hilo," Joseph Amougou wa Timu ya Kitaifa ya Kuratibu Mpango wa REDD nchini Cameroon, aliiambia IPS.

Ili kufikia ndoto hii kutahitaji kupatia ufumbuzi changamoto zilizopo za kiutawala, ikiwa ni pamoja na kufanya tathmimi na kuimarisha sera na kuhakikisha kuwa kuna ushiriki wenye maana na wa jamii zinazotegemea misitu – hasa makundi yaliypo pembezoni katika maeneo ya vijijini kama vile wanawake na watu wa makabila ya wenyeji.

"REDD haitafanya kazi nchini Cameroon bila kuendelezwa kuanzia chini. Haitaweza kutekelezwa bila ya kuhesabu kazi zinazofanywa na wakazi wa maeneo husika ambao wanaendesha kilimo, matumizi ya rasilimali za misitu na ufugaji wa mifugo. REDD inatakiwa kuboresha shughuli zao hizi na hali ya maisha ya watu hao ili wasiongeze shinikizo katika matumizi ya misitu," Amougou alisema.

"Kwa mfano, katika sehemu ya kaskazini mwa Cameroon ambako tatizo kubwa ni la nishati inayotokana na kuni na mkaa, REDD lazima kuweka kipaumblele cha mahitaji ya nishati kwa wakazi wa maeneo hayo."

Tayari kuna majukwaa mengi kuunga mkono aina hii ya ushiriki.Kamati ya Utekelezaji ya Taifa – ambayo ni pamoja na uwakilishi wa watu wazawa – inawaleta mawaziri kujadili pamoja na mashirika ya kiraia na NGOs, wakati ambapo REDD na Jukwaa la Mabadiliko ya Tabia Nchi hupatia mashirika ya kiraia na jamii mahali pa kujadiliana.

Haman Unusa anatoka Kitengo cha taifa cha Kuratibu Mpango wa REDD katika Wizara ya Mazingira na Utunzaji wa Viumbe Asili na Maendeleo, chombo ambacho kina wajibu wa kutekeleza kazi za kiufundi ikiwa ni pamoja na mikutano na ushauriano. Aliiambia IPS kuwa watu wazawa walishiriki katika ushauriano katika mchakato mzima wa maandalizi ya RPP. Hii itaendelea hata katika awamu ya pili ya utekelezaji.

"Wazawa watashiriki kwa kupitia katika mashirika yao mbalimbali. Wazawa pia watajiwakilisha wenyewe katika matawi ya kimkoa na kijamii ya REDD na Jukwaa la Mabadiliko ya Tabia Nchi," Unusa alisema.

"Mpango wa kuunganisha jinsia katika mchakato wa REDD umeandaliwa na utapanuliwa kama sehemu ya muendelezo wa mkakati huo. Wanawake pia wana uwakilishi katika vyombo vya kitaifa – moja ya nafasi za kiutendaji za uratibu wa kitaifa zimetengwa kwa ajili ya wanawake," alisema afisa huyo.

Unusa aliongeza kuwa mkakati wa mawasiliano katika awamu ya utekelezaji utahusisha matumizi ya lugha za kienyeji na mawasiliano kwa njia ya kuona kama vile mabango madogo na makubwa. Wakalimani watatumiwa kuendesha mawasiliano ya pande zote mbili kati ya wawezeshaji wa REDD na wakazi wenyeweji.

Hata hivyo mipango hii ya kuongeza njia za mawasiliano inaweza kuwa na mapungufu yake katika mchakato huo. Kwa mujibu wa Aehshatu Manu, ambaye amewakilisha wanawake wazawa wa Mbororo katika mikutano ya FCPF, wanawake wengi wazawa bado hawajui REDD inataka kufanya nini, na wana wasiwasi wataweza kupoteza misitu yao na mazao yake kama vile vifaa vya ujenzi, mimea ya madawa na chakula.

"Pamoja na ushiriki wa wanaume na wanawake katika mikutano," aliiambia IPS, "ushiriki kamilifu bado haujafikiwa kupitia mkakati wa mawasiliano unaotekelezwa sasa. Bado REDD haifahamiki vizuri kwa wananchi wa maeneo husika."

Amougou alisema kuwa watunga sera wanakabiliwa na changamoto nyingi katika kubuni na kutekeleza mikakati ya REDD na sera."

"REDD ni mpya, lakini ni lazima kujengwa katika mali zilizopo na maono ya utekelezaji wa sera. REDD inaweza kutekelezwa pamoja na sera za kitaifa, kitaasisi na shughuli za utekelezaji zilizopo," alisema.

Tishio jingine la utekelezaji linatokana na kukosekana kwa rasilimali fedha. Dola milioni 3.6 kutoka FCPF ni jambo zuri, lakini bajeti ya jumla ya RPP nchini Cameroon ni dola milioni 28, na hizo bado hazijajulikana zitatoka wapi.

"Ili kuweza kuziba pengo hilo la kifedha, mikakati ya REDD ya Cameroon inatakiwa kujikita katika rasilimali ambazo tayari zipo kama vile orodha ya takwimu za misitu, tafiti za REDD za watu wanaoongoza katika uteketezaji wa misitu na jitihada za kuhifadhi misitu hiyo," Menang alisema. "Na serikali na washirika wengine wa maendeleo lazima kufanya kazi pamoja kusaidia mchakato huu kifedha."

Kutafuta fedha zinazohitajika ni changamoto, lakini Augustine Njamnshi wa NGO ya Hifadhi na Uendelezaji wa Rasilimali za Viumbe Hai nchini Cameroon anaona ni faida kama fedha hizo hazitapatikana. "Kama REDD haitaleta pesa, ituletee utawala bora." (END/2013)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The element 'html' is used but not declared in the DTD/Schema.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>