Inter Press Service News Agency
Monday, May 21, 2018   08:01 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions


Ukiwa Mkulima Mdogo Nchini Kenya, uko Mashakani
Na Miriam Gathigah

NAIROBI , Sep 16 2013 (IPS) - Kutokana na hadhari ya usalama wa chakula na maisha ya wakulima kunakosababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa, nchi ya Kenya imeainisha sera mbadala. Sera mojawapo ni ile ya kutegemea teknolojia mpya na kuongeza matumizi ya mbolea na kuua wadudu; na nyingine itahusisha maarifa ya asili na bioanuai.

Cha muhimu ni kuokoa maisha ya wakulima wadodo wadogo nchini humo iwapo itatokea mabadiliko ya ghafla ya hali ya hewa. Kwa mujibu wa Wizara ya Kilimo imekisiwa kwamba wakazi milioni tano kati ya milioni nane nchini Kenya maisha yao yanategemea moja kwa moja kilimo. Lakini wakulima wa Kenya – hususan wadogo wadogo- wanakumbana na maisha yasiyotabirika kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa. Takwimu za msimu uliopita wa kilimo zinaendelea kuonyesha mashaka makubwa ya hali halisi inavyoendelea kutokana na kupungua kwa vyanzo vya maji ikilinganishwa na miaka iliyopita. "Vijito vingi vya mito na mifereji inayotiririka kutoka Milima ya Kenya, Milima ya Mau, Aberdares, Cherangani na Elgon havina maji ya kutosha, au vinakauka kabisa wakati wa kiangazi," Joshua Kosgei, Afisa Kilimo wa Elburgon, jimbo la Rift Valley , analiambia shirika la habari la IPS. Ripoti ya mwaka 2012/2013 ya Shirika la Kimataifa la Kilimo na Chakula nchini Kenya imeonyesha kuwa mvua za vuli za mwezi Oktoba hadi Desemba zilikuwa za kiwango cha chini kuliko wastani. Zaidi ya hayo, ripoti imebaini: "Mfululizo wa nyakati za kiangazi pia umesababisha kunyauka kwa mazao, kuongeza mahitaji ya kupandikiza upya (zaidi ya mara tatu) kulikopelekea kudumaa au kunyauka kwa mazao." Kwa mujibu wa Taasisi ya Kilimo ya Kenya (KARI), zaidi ya watu milioni 10 kati ya idadi ya watu milioni 40 hawana usalama wa chakula, na wengi wao wanaishi kwa chakula cha msaada. Sekta ya kilimo inachangia kiasi cha asilimia 25 cha kipato cha nchi za Afrika Mashariki na asilimia 60 ya mauzo ya nje. Takwimu za serikali zinaonyesha kwamba uzalishaji wa wakulima wadogo wadogo unachangia kwa kiasi cha asilimia 75 ya mazao yote ya kilimo na asilimia 70 ya mazao ya biashara. Chai, moja ya zao kubwa la kuuza nje iliingiza dola za Kimarekani bilioni 1.17 kulingana na Takwimu za Taifa, hali inayoashiria hatari kubwa. Wataalam wanakadiria kwamba mabadiliko ya hali ya hewa yanaweza kuathiri zao la chai kwa zaidi ya asilimia 30 ya pato la zao hilo. "Chai inaathrika sana na mabadiliko ya hali ya hewa," Kiama Njoroge, Afisa Kilimo kutoka jimbo la kati nchini Kenya, analiambia shirika la habari la IPS. "Matokeo yake wakulima wadogo wadogo wapatao, 500,000 wanakabiliwa na hofu kubwa ya maisha." Joel Nduati, mkulima mdogo kutoka jimbo la kati la Kenya, anaongeza: "Ukosefu wa taarifa na kuchukua hatua ili kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa ni changamoto kubwa." Nduati analiambia shirika la IPS kwamba tatizo jingine linalowakabili wakulima ni jakamoyo la maji. "Maji ni mengi wakati hatuyahitaji, ikifuatiwa na kipindi kirefu cha ukame. Tunachohitaji ni mazao mbalimbali yanayoweza kuhimili mabadiliko haya ya hali ya hewa." Hata hivyo kwa mujibu wa Kosgei, mipango ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa imeshaainishwa; kinachokosekana ni njia fasaha ya kuwasilisha taarifa hizi kwa wakulima. "Kwa mfano, Taasisi ya Utafiti wa Chai Kenya (KARI) imevumbua aina 45 za chai, lakini wakulima wengi bado hawazitumii kwa sababu hawajui iwapo zinapatikana," anasema Kosgei. Anaongeza zaidi kwamba aina nyingine tano za viazi na nyingine kadha za zao la mboga aina ya kabichi pia zimevumbuliwa na taasisi hiyo la KARI. "Wakulima wangapi wanaelewa hilo, ukiachia mbali matumizi ya aina mpya ya mbegu?" Usambazaji wa taarifa hizi unasababishwa na uchache wa Maafisa wa Kilimo. Wakati FAO imependekeza kuwepo kwa Afisa Kilimo kuhudumia wakulima 400, kwa sasa, Kenya ina Afisa Kilimo mmoja ambaye huhudumia wakulima 1,500 kwa mujibu wa Chama cha Kimataifa cha Kilimo na Maendeleo Vijijini. Wakulima wadogo wadogo wa Kenya wanazalisha moja ya tano ya kinachowezekana, anasema Afisa Kilimo. Lakini sio kila mtu anakubaliana na taarifa za Kosgei. "Suluhisho ni kurudisha maarifa ya asili ambayo yanakuza mazao ya mizizi. Mkakati unaounganisha kwa pamoja kilimo kisichotumia mbolea za kemikali," Gathuru Mburu, mratibu wa Mtandao wa Bayoanuwai Afrika analiambia shirika la IPS. "Wakulima wanazalisha chini ya kiwango kutokana na matumizi makubwa ya madawa. Kilimo cha kawaida kinatumia mbolea ya asili. Mazao yaliyobaki baada ya mavuno hutumika pia kama mbolea," Mburu anaeleza. Njoroge anakubali, kwa kusema kuwa nchi hususan zaRwanda, Ethiopia na Ghana wanapiga hatua za maendeleo katika kuboresha usalama wa chakula na maisha kwa kutumia maarifa ya asili. Lakini mabadiliko ya elimu ya viumbe na kilimo kinarudisha nyuma teknolojia mpya ambayo ni tegemeo kubwa. "Kushutumu matumizi ya madawa sio suluhisho. Wakulima lazima wapatiwe njia mpya za kisayansi," mtafiti wa bayoanuai John Kamangu analiambia shirika la IPS. "Tunahitaji mbinu mpya zitakazowezesha kuzalisha mbegu zinazostahimili ukame na mvua nyingi." Lakini Mburu anapinga jambo hilo na kusema kwamba mbinu hizo hazikuzaa matunda barani Afrika. "Serikali za Kiafrika zinajivua wajibu wao wa kifedha kwa ajili ya sekta ya kilimo, na kuachia mwanya kwa mataifa makubwa kuingiza fedha wakati ni hao hao wanaoinyonya Afrika," anasema. "Haya ni makampuni yanayoendeleza uzalishaji wa madawa. Mbegu zao zinahitaji madawa mengi ili ziote. Mbegu hizi pia humea katika sehemu maalum," Mburu anasema. Kosgei anakubaliana naye, kwa kusema kuwa hawa wawekezaji lengo lao kubwa ni kupata faida na sio kuilisha Afrika. Mburu anahofia kwamba kuwapa ruhusa wawekezaji, serikali itakuwa inatumia sera zinazowaumiza wazalishaji wadogo wadogo ambao wanazalisha asilimia 70 ya chakula nchini. "Mataifa makubwa yanataka kuua sekta binafsi, kwa maneno mengine wakulima wadogo wadogo. Baadhi ya Sheria zinazotayarishwa zinahusiana na mbegu na nyingine za kupinga mbegu bandia," Mburu anaeleza. "Sheria inayopinga mbegu bandia inalenga kudhibiti mbegu. Wananchi wetu wanatumia mbegu za asili (ambazo hazijadhibitiwa) hawataweza kufanya hivyo mara sheria hiyo itakapoanza kutumika." Mburu anasema kwamba mbegu hizi "hazina mahusiano yoyote na mabadiliko ya hali ya hewa. Mbegu hizi zinadhibitiwa na makampuni sita duniani ambayo yanamiliki mabilioni ya dola katika uwekezaji na hawahitajiki kubadili mfumo ikilinganishwa na mbegu asilia." (END/2013)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The element 'html' is used but not declared in the DTD/Schema.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>