Inter Press Service News Agency
Tuesday, June 19, 2018   19:11 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions

TANZANIA
Lulu Yatimiza Ndoto za Mafanikio kwa Wanawake Zanzibar
Na Mwandishi wa IPS

ZANZIBAR, Julai 19 (IPS) - Lulu ni miongoni mwa madini adimu sana ambayo hupatikana ndani ya viumbe bahari wajulikanao kama Chaza(viumbe vitokanavyo na jamii ya Konokono). Madini haya ya Lulu yameendelea kuwa adimu kwenye maeneo mengi kutokana na kukithiri kwa vitendo vya uharibifu wa mazingira hususan vitendo vya uvuvi haramu pamoja na upasuaji wa baruti katika matumbawe ambayo ndiyo nyumba kuu za Chaza.

Watengenezaji wa lulu na mapambo kwa kombe Zanzibar ni mradi wa kimaisha ambao unakusudia kuufanya ukulima wa lulu na utengenezaji wa bidhaa za mapambo kwa kutumia mkono ikiwemo utumiaji wa magamba ya chaza na kombe kama ni njia moja wapo ya kujipatia kipato kwa jamii zinazoishi katika vijiji vya mwambao. Pia ni n jia inayotumika na wananchi hawa kutunza mazingira ya bahari kwa ajili ya vizazi vya sasa na vijavyo. Wananchi hao wamekuwa wakitegemea ukusanyaji wa chaza na makombe kwa ajili ya chakula na biashara. Eneo la Fumba Bondeni wilaya ya magharibi, mkoa wa mjini Magharibi Visiwani Zanzibar ni miongoni mwa maeneo maarufu kwa kilimo cha Chaza za Lulu, uzalishaji na uuzaji wa mapambo yatokanayo na madini aina ya Lulu. Hatua hiyo imefikiwa baada ya muunganiko wa vijiji vinne ambavyo vipo chini ya usimamizi wa Mradi wa Uhifadhi wa Mazingira ya Pwani(Tanzania Coastal Management Partnership- Pwani Project- TCMP- Pwani) ambao unafadhiliwa na shirika la misaada la Marekani USAID na kupata ushauri wa kifundi kutoka Kituo cha Rasilimali za Bahari cha Chuo Kikuu cha Kisiwa cha Rhode nchini Marekani. Wananchi wa vijiji hivyo ambavyo ni Fumba Bondeni, Fumba Chaleni, Nyamazi na Bweleo walifikia hatua ya kuunda umoja baada ya kupata mafunzo ya utunzaji na uhifadhi wa mazingira sambamba na utumiaji sahihi wa rasilimali zinazowazunguka. Baada ya kujikita katika mradi huo, habari za mafanikio zinatofautiana kutoka kwa mwanachama mmoja hadi mwingine. "Sikuona zawadi nyingine ya kumpatia mume wangu kutokana na kitendo chake cha ujasiri wa kuniruhusu kufanya kazi jambo ambalo ni kinyume na mila na desturi zetu zaidi ya kumnunulia Jahazi ili aweze kuendelea na shughuli zake za uvuvi kwa ufanisi mkubwa," anasema Rahma Mussa mkazi wa Kijiji cha Fumba Chaleni, ambaye ameweza kupata mafanikio makubwa kutokana na kilimo hicho cha Chaza za Lulu. Kwa mujibu wa Rahma ruksa ya kufanya kazi kwa mwanamke ni jambo adimu sana kulingana na mila, tamaduni na desturi zao. Kimsingi Rahma ni mama wa familia ambaye kwa sasa ni miongoni mwa wanawake walio katika umoja wa wakulima wa Chaza za Lulu. Awali mama huyu alikuwa akijishughulisha na shughuli za ukataji wa miti na uchomaji wa mkaa na kwa maelezo yake hakuwa akiamini kuwa bahari inaweza kuwa na rasilimali za kumfanya yeye na familia yake wamudu kuendesha maisha yao ya kila siku. "Tumezoea toka enzi na enzi wazazi wetu, waume waliotuoa wote wavuvi lakini maisha yalikuwa ni vile vile bila mabadiliko yoyote zaidi ya kubobea katika umaskini…mimi sikujua kama siku moja bahari inaweza kunifikisha hapa nilipo," anasema. Anasema ndoto za mafanikio zilianza kujitokeza baada ya wanawake kujikusanya ili kuunda vikundi ambavyo vingewezeshwa kutumia rasilimali zitokanazo na Bahari katika kukabiliana na umaskini. "Nilipopata taarifa za kutaka kujiunga na wenzangu katika vikundi kutoka washauri wa mradi wa TCMP, nilitafakari na kukubaliana na wenzangu kujiunga katika vikundi ambavyo baadaye tulipata mafunzo ya matumizi ya rasilimali zitokanazo na bahari ikiwemo kilimo cha chaza za lulu",anafafanua. Rahma anasema awali kutokana na kutokuwa na jengo la kuweka biashara zao walikuwa wakizitembeza kwenye magari ya watalii hatua iliyomuwezesha kujifunza lugha mbalimbali za kigeni ikiwemo Kiitaliano ili kutamka bei na kupata wateja kirahisi. "Sasa hivi najua kiitaliano yaani zile bei nazipanga kwa lugha zao mwanzo nilikuwa naogopa lakini sasa nipo tayari kukabiliana na mtu yeyote yule na kuzungumza naye biashara. Nimepata ujasiri mkubwa sana hata kuzungumza mbele za watu kutokana na shughuli hizi",anasema. Kuhusiana na soko la bidhaa zao anasema ni kubwa na la uhakika ingawaje limekuwa ni la msimu kuanzia mwezi Julai hadi Machi ambapo kunakuwa na wimbi la watalii kutoka nje ya nchi. "Wageni wengi wanaanza mwezi wa saba kundi la kwanza ni la Waitaliano, wanakuja wazungu wengine na mwezi wa kumi wageni wengi ni kutoka Afrika ya Kusini katika kipindi hicho tunaingiza kuanzia dola 150 au wakati mwingine Euro 200 kwa siku katika msimu. Kusema kweli biashara inakuwa ni kubwa sana katika msimu huo wa Julai mpaka Machi kila mwaka," anabainisha. Kwa mujibu wa mwanakikundi huyo ni kwamba kutokana na kilimo hicho maisha yao kwa ujumla yamebadilika na wameweza kupata mitaji ya kutosha katika kuanzisha biashara nyingine. Mradi wa kilimo cha Chaza katika vijiji hivyo ulianza mwaka 2006 baada ya kujitokeza kwa wahisani na wafadhili mbalimbali ambao walifanya utafiti na kubaini kuwa iwapo mazingira yatalindwa basi rasilimali hiyo inaweza kuwa endelevu kwa kizazi cha sasa na baadaye. Lulu za maji ya baharini hupatikana katika ukubwa na maumbile tofauti, hufanyika ndani ya gamba la chaza na kimsingi wananchi katika vijiji husika hujishughulisha na ukulima wa lulu kwa awamu zote toka kupachikwa kwa mbegu hadi uvunaji wa lulu ambazo hutengeneza mapambo na kombe ambazo husafishwa na kutengenezwa bidhaa kama vile mikufu, hereni na bangili. Alli Mataka, ni miongoni mwa wanakikundi ambao wanalima Chaza za Lulu katika maeneo hayo ambaye anasema ili kukabiliana na hali hiyo wameweka maeneo tengefu ya miamba kwa ajili ya uzalishaji endelevu wa chaza. Mataka anasema tangu kupandikizwa kwa vifungo vya chaza mpaka uzalishaji wa Lulu ni zoezi linalochukua kwa kipindi cha mwaka mmoja ingawaje mauzo yake nayo hudumu kwa mwaka mzima. "Pamoja na kwamba utaona ni muda mrefu tangu kupandikiza kwa vifungo mpaka kupatikana kwa lulu lakini pia lulu inayopatikana unaweza kuiuza kwa mwaka mzima," anafafanua Mataka. Kutokana na upatikanaji wa chaza kuhitaji uzamiaji baharini wanavikundi wanaoendesha kilimo hicho wamejigawa katika makundi ambapo wanaume ndiyo wazamiaji baharini na wanawake wamekuwa watengenezaji wa mapambapo yanayotokana na Lulu pamoja na Magamba ya Chaza. Miongoni mwa mapambo yanayotengenezwa kutokana na aina ya viumbe bahari hao ni pamoja na hereni,mikufu,na bidhaa nyingine mbalimbali za urembo. (END/2013)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The element 'html' is used but not declared in the DTD/Schema.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>