Inter Press Service News Agency
Monday, June 18, 2018   10:54 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions


UWAMKE SACCOSS Mkombozi wa Wakulima wa Ufuta Bagamoyo
Na Mwandishi wa IPS

Bagamoyo, Julai 19 (IPS) - "Wengi wetu hapa ni wakulima lakini tulikata tamaa kabisa ya kuendelea na kilimo kwa sababu tulikuwa tukipata hasara kila msimu wa mavuno na zaidi tulikuwa tukilima mahindi lakini hayakuletea tija kabisa na wengi tulikuwa na mawazo ya kuachana na kilimo", anasema Mwenyekiti wa Chama cha Kuweka Akiba cha Kijiji cha Mkange cha UWAMKE SACCOSS, Mashavu Said.

Said anasema wakati wakiwa wamekata tamaa, walijitokeza wataalam kutoka Mradi wa Pwani wa Mpango wa Kuhifadhi Mazingira ya Pwani (Tanzania Coastal Management Partnership-TCMP-Pwani) ambao unafadhiliwa na shirika la misaada la Marekani USAID na kuwapatia mafunzo ya utunzaji wa mazingira, afya, ujasiriamali na namna ya kukabiliana na umaskini kwa kutumia rasilimali zinazowazunguka.

Said anasema baada ya kupata mafunzo ya ujasiriamali na namna ya kujikomboa na umaskini na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwa kupanda mimea ambayo inastahimili ukame, walipata upya moyo wa kuendelea na kilimo na badala ya mahindi wakatambulisha zao jipya la ufuta.

"Baada ya kupata elimu kutoka mradi wa TCMP-Pwani tukagundua kuwa kumbe hakuna sababu ya kuacha kilimo badala yake ni kutafuta mazao mbadala ambayo yanastahimili ukame ndio tumeanza na kilimo cha ufuta", anasema.

UWAMKE ni chama cha akiba cha kuweka na kukopa ambacho kimefanikiwa kuwaunganisha wanawake kwa ajili ya kujiwezesha kiuchumi.Chama hiki kipo katika wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani ambapo kati ya wananchama wake 74 wanaume ni tisa tu.

Kwa mujibu wa Said, lengo kuu la kuanzishwa kwa chama hicho ni baada ya kuona na kutambua kuwa ni vigumu kwa mtu mmoja mmoja kupata mafanikio ya haraka na ipo haja ya kuunganisha nguvu ili kukabiliana na hali ngumu ya maisha.

Said anasema chama chao kilianza kikiwa na mtaji wa shilingi 100,000 huku wanachama wake ambao wengi wao ni wakulima wakiwa wamekata tamaa kabisa ya kuendelea na shughuli za kilimo kutokana na kutopata mavuno mazuri katika misimu ya kilimo hali inayosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi.

Hata hivyo, anasema katika SACCOSS hiyo licha ya kupata mafunzo, TCMP- Pwani imewapatia pia kiasi cha shilingi milioni 3 kuongezea mtaji wao na kwamba serikali ya kijiji kutokana na jitihada zao imewapa shamba la heka 50 ambapo tayari wameshapanda ufuta katika heka nne.

Mwenyekiti huyo anasema kwa sasa wana mtaji wa shilingi milioni 14 katika chama chao na wameanza kukopeshana kwa ajili ya kuendeleza shughuli zao mbalimbali za kiuchumi. "Malengo yetu yaliyopo katika hizo heka 50 licha ya kupanda ufuta lakini pia tunataka kujenga jengo la ofisi pamoja na kuweka mizinga ya nyuki kwenye eneo hilo ili kujiongezea kipato na vivyo hivyo kukabiliana na ukame kwa kupanda miti na kutunza iliyopo," anasema, huku akiongeza kuwa "Tunaamini kwa kasi tuliyonayo tutafanikiwa tu kwani mabadiliko ya kimaisha kati yetu tumeanza kuyaona". Licha ya kufanya shughuli za pamoja kama chama, wanachama hao wa UWAMKE wamekuwa wakifanya shughuli za mtu mmoja mmoja ambapo wameendelea kujikita kwenye kilimo na kutafuta mashamba yao binafsi. Akitoa ushuhuda kuhusu mafanikio aliyoyapata, Mwanahamisi Kitivo anasema baada ya kupata mkopo wa zaidi ya shilingi milioni mbili kwenye SACCOSS yao ameweza kununua shamba ambalo lina ukubwa wa heka tano, ambapo heka mbili amepanda mahindi na heka tatu amepanda ufuta.

Kitivo anasema mpaka kufikia mavuno anatarajia kuvuna kilo 300 za ufuta kwa kila heka moja na kwamba bei ya ufuta kwa kilo ni kuanzia shilingi 1500.

"Katika fedha za mkopo nilizopata zilinisaidia kung’oa visiki na kulima kwa kutumia trekta la kukodisha na ndio maana nina matumaini ya kupata mavuno mengi katika msimu huu kwa sababu nimetumia kilimo cha kisasa zaidi: Kama ingekuwa ni jembe la mkoni nisingeweza," anasema mwanachama huyo wa UWAMKE SACCOSS.

Hata hivyo anaiomba serikali na wafadhili mbalimbali kutambua kuwa kilimo pekee ambacho kitamkomboa mkulima ili kuondokana na umaskini ni kilimo cha kutumia zana za kisasa na kwamba hata powertiller zinazotolewa bado hazina tija kwa mkulima kutokana na kushindwa kung’oa visiki.

"Kusema kweli kilimo bora ni cha trekta na hili nimelishuhudia mwenyewe kwa sababu nimelima kwa trekta baada ya kupata mkopo sasa kama kweli serikali imedhamiria kumkomboa mkulima na umaskini waachane na powertillers ambazo hazina tija angalau kila kijiji waweke trekta moja hata kama ni la kukodi watakuwa wamesaidia sana wananchi wa vijijini," anasisitiza.

Mbali ya mafanikio katika kilimo, baadhi ya wanachama wengine wa UWAMKE wameweza kujenga nyumba na kuongeza mitaji ya biashara zao kutokana na shughuli wanazozifanya.

Kwa upande wake, Patrick Kajubili, Mtaaalam wa masuala ya ukuzaji uchumi katika mradi wa TCMP-Pwani anasema kuwa miradi inayotekelezwa wilayani Bagamoyo ni ile iliyolenga kuhifadhi na kulinda mazingira ya bahari na ya ukanda wa pwani na kukuza uchumi kwa wananchi ili waondokane na umaskini kwa kutumia rasilimali zinazowazunguka.

Kajubili anasema kwa kuzingatia kuwa wakazi wengi wa ukanda wa Pwani wamekuwa wakiishi kwa kutegemea bahari, wengi wao wanaendesha shughuli zisizorafiki wa mazingira ya bahari na rasilimali za pwani na siyo endelevu.

Anasema kutokana na kulitambua hilo, TCMP-Pwani imeanzisha miradi ya uhifadhi wa viumbe walio hatarini kutoweka, utengaji wa maeneo tengefu kwa ajili ya uhifadhi wa matumbawe na viumbe bahari sambamba na uhifadhi wa mazingira ya nchi kavu ikiwemo misitu na kuwahamasisha wananchi kujiunga katika vikundi ili kupata mitaji ya kuanzisha shughuli mbadala ambazo ni rafiki kwa mazingira.

"Sasa ili kufanikisha suala zima la uhifadhi endelevu wa mazingira lazima utambulishe shughuli mbadala kwa wananchi husika kwa kuhakikisha wanaongeza kipato na wanamudu kuendesha maisha yao ya kila siku," anasema.

Mtaalam huyo anataja miongoni mwa shughuli za kiuchumi ambazo hufanyika kuwa ni pamoja na uanzishaji wa vyama vya akiba vya kuweka na kukopa, kilimo kinachotokana na rasilimali za bahari kama ufugaji wa samaki, kilimo cha chaza na kilimo cha mwani pamoja na ufugaji wa nyuki ikiwemo kwenye maeneo ya mikoko ambapo waharibifu wengi wanashindwa kukata miti hiyo kwa kuhofia wadudu hao.

Naye Mjumbe wa Kamati ya Uhifadhi wa Mazingira kutoka halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo Injinia Jason Raphael anasema kuwa halmashauri kwa kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira imeanza kutekeleza miradi ya hifadhi ya mazingira wilayani humo na tayari wameshafikia vijiji saba katika wilaya hiyo.

Raphael anasema katika ushirikiano huo wameweza kuchimba visima katika baadhi ya vijiji sambamba na kutambulisha miradi mbalimbali ya maendeleo endelevu katika uhifadhi wa mazingira.(END/2013)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The element 'html' is used but not declared in the DTD/Schema.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>