Inter Press Service News Agency
Monday, June 18, 2018   10:42 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions


Waelimishaji wa Masuala ya Kujamiiana Wapambana Kuvunja Miiko
Stella Paul

KUALA LUMPUR, Julai 15 (IPS) - Mwandishi wa habari wa Liberia, Mae Azango, anasema alitumia mwaka mzima akiishi "kama panya, huku akipita mti mmoja hadi mwingine" akiwa na binti yake ili kuepukana na wanadini wenye msimamo mkali ambao walitishia kumuua kutokana na kutangaza masuala ya tohara kwa wanawake nchini mwake mwaka jana. Akiwa mwandishi mwandamizi katika gazeti la nchini humo la FrontPage Africa, Azango aliiambia IPS kuwa pamoja na kwamba serikali ya Liberia ilitia saini mkataba mwaka 2012 unaoahidi wananchi wake haki ya habari, inaendelea kushikilia takwimu za haki ya kujamiiana na uzazi kwa waandishi wa habari.

"Kwa kila habari ambayo naandika, nahatarisha maisha yangu," anasema, akiongeza kuwa nategemea kwa kiasi kikubwa taarifa "za vyanzo vya siri" kutoka serikalini kukusanya taarifa, kwani ni habari chache mno zinasambazwa kwa umma.

Matatizo yake yanaungwa mkono na wanawake walio wengi na wataalam wa afya waliokusanyika katika mji mkuu wa Malaysia, Kuala Lumpur kwa ajili ya jukwaa la tatu la kila mwaka la Women Deliver siku ya Alhamisi.

Wakitoka pande zote za dunia, washiriki wa mkutano huo hawana shida na kubainisha malengo: na wameweza kuvunja miiko inayozunguka elimu ya kujamiiana na kujenga mazingira salama ya utetezi, wasomi wa masuala ya afya na waelimishaji kusambaza elimu ya ngono salama na uzazi wa mpango.

Nchini Morocco, nchi yenye jumla ya wakazi milioni 32, mashule yamepigwa marufuku kutoa elimu ya kujamiiana kwa vijana kwasababu wabunge wana imani kuwa ni "dhana ya kishetani, iliyobuniwa kukuza uasherati," mtetezi wa afya ya kujamiiana na ya uzazi, Amina Lemrini, aliiambia IPS.

Anasema mafanikio ya kuboresha huduma za afya ya uzazi nchini mwake yamekuja polepole mno kutokana na miiko iliyoanzishwa na viongozi wa kidini.

Huku serikali ikishindwa kuwakosoa viongozi wa dini, kazi ya kusambaza huduma muhimu za afya inaangukia kwa kiasi kikubwa kwa mashirika ya kijamii, ambayo jitihada zao zinatishiwa.

Lemrini anasema hatambui mwanaharakati hata mmoja wa haki za uzazi ambaye hajatishiwa maisha, hata hivyo serikali haiwapatii ulinzi wowote ule.

Matatizo yao yametambuliwa na wataalam wakongwe katika nyanja ya afya ya uzazi, ikiwa ni pamoja na mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Idadi ya Watu la Umoja wa Mataifa (UNFPA), Babatunde Osotimehin, ambaye aliiambia IPS kuwa imani kali za kidini ni "jambo linalotia wasiwasi" linapokuja suala la kuendeleza afya ya kujamiiana.

Hata hivyo, bado anawataka wanaharakati kuendelea kufanya kazi zao, akiongeza kuwa, "Imani kali zinaendelea katika jamii na dini zote – jambo la msingi ni jinsi gani tunaweza kuwasilisha ujumbe."

Ana imani kuwa kama watu wengi zaidi wanatambua haki na chaguo lao, hawatasita kukataa sheria za kishamba na kile kinachojulikana kama "miiko ya kitamaduni."

"Mtu wa kawaida mtaani hataki hali ambapo kifo kinaita kila wakati kutokana na sababu kwamba hakiwezi kuzuiliwa," alisisitiza.

Hata kwa kuangalia kwa haraka takwimu za kimataifa inatosha kutoa msimamo wenye nguvu wa kuwasiliana vizuri: kwa mujibu wa UNFPA, karibu wanawake 800 wanakufa kila siku kutokana na matatizo yanayohusiana na mimba; kwa mwaka, idadi hiyo inafikia 350,000, ambapo kati ya vifo hivyo, asilimia 99 vinatokea katika nchi zinazoendelea.

Utoaji wa mimba usiokuwa wa kitaalam na kutelekezwa kwa watoto wa kike wadogo wanaojifungua kumeasababisha wastani wa vifo milioni 134 duniani kote.

Ikikusanya takwimu duniani kote, UNFPA inakadiria kuwa "mamilioni ya watoto wa kike" wanafanya ngono isiyokuwa salama na wanakosa taarifa za uzazi wa mpango. Osotimehin hivi karibuni aliandika kuwa "mahitaji yasiyofikiwa ya uzazi wa mpango ni miongoni mwa asilimia 33 ya watoto wa kike kati ya miaka 15 na 19 …nchini Ethiopia, asilimia 38 nchini Bolivia, asilimia 42 nchini Nepal, asilimia 52 nchini Haiti na asilimia 62 nchini Ghana."

Nyaradzayi Gumbonzvanda, mkuu wa Chama cha Vijana wa Kikristo Wanawake (YWCA), aliiambia IPS kuwa kuwekeza katika mawasiliano ya afya ya kujamiiana na uzazi ni suala la kuchagua.

"Tunahitaji mazingira mazuri kwa wale wanaojadili suala hili," alisema. "Tunahitaji kulinda vyombo vya habari – hili siyo chaguo. Serikali lazima iongeze kiwango cha ushirikiano na kutoa msaada wa kisheria pale ambapo haupo."

Gumbonzvanda anadhani kuwa uandishi wa habari wa kiraia unapaswa kuchukua nafasi kuondokana na hatari inayotokana na misimamo mikali, siyo kwa kutoa sauti tu kwa wale ambao mara nyingi hawasikiki, lakini pia kuwapatia uwezo wananchi wa kawaida kuchukua hatua.

Hakuna mahali ambapo nguvu ya uandishi wa habari wa jamii imeonekana zaidi kuliko kipindi cha mapinduzi nchini Misri mwaka 2011, ambapo blogu, tweeter, na Facebook vilichukua nafasi ya vituo vya televisheni, magazeti na vituo vya redio katika kuwafikia watu.

Leo hii Wamisri wanakabiliana na sera za kihafadhina za utawala wa chama cha Muslim Brotherhood, ambapo mitandao ya uandishi wa habari wa kijamii imegeuza suala la afya ya uzazi na kujamiiana mada ambayo imetelekezwa na Uislam.

Ahmed Awadalla, afisa jinsia na afya ya kujamiiana kwa Afrika katika Shirika la Wakimbizi la Mashariki ya Kati (AMERA), aliiambia IPS kuwa kila mmoja anajadili suala la hatari ya kuwekwa kizuizini, kukamatwa na kuwekwa jela.

Matokeo yake idadi ya wenye blogu inaongezeka kila siku, kwani wananchi na watetezi wanakimbilia katika nafasi ya mtandao kutafuta usalama wao katika kusambaza taarifa.

"Ninapoandika katika blogu kuhusu haki za kujamiiana za wanawake navunja sheria mbili," Awadalla alisema. "Kwanza, kwa kuzungumza kuhusu suala ambalo limezuiliwa na pili kuzunguma kama mwanaume, ambaye hatakiwi kuchukua nafasi ya mwanamke." Pamoja na kukabiliana na ukandamizaji mbaya, hakuna ambacho kitamrejesha nyuma kutoa utetezi wake.

Lakini wakati wananchi wanabuni mawazo mapya ili kukabiliana na vitisho vikali vya kutoa elimu ya kujamiiana, wataalam wanasema serikali lazima isiachwe kwa kushindwa kutoa huduma hizi za msingi.

Serikali za bara la Asia, Afrika na Amerika Kusini, lazima ziwajibishwe na wafadhili wa kigeni, anasema Agnes Callamard, mkurugenzi mtendaji wa Article 19, London.

"Kila serikali imejitolea kutumia kiasi fulani cha fedha wanazopata (katika afya ya kujamiiana)," alisema, hivyo kufuatilia kumiminika kwa misaada kunaweza kushinikiza serikali kuboresha rikodi zao za kutawanya taarifa.

Wakati shirika lenye makao yake Mexico la Grupo de Información en Reproducción Elegida (GIRE) lilipoanza kufuatilia misaada inayopaswa kusaidia katika usambazaji wa taarifa za afya ya uzazi na kujamiiana mwaka 2011, "tuligunndua kuwa karibu dola milioni zilikuwa zimepotea," alisema Mtetezi wa Haki ya Habari wa GIRE Alma Luz Beltrán y Puga. "Tulifungulia mashitaka serikali kutokana na hili. Kama ufuatiliaji kama huo utafanyika duniani, unaweza kusababisha uwajibikaji wa kiasi kikubwa."

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO), nchi zenye maendeleo zinachangia karibu dola bilioni 6.4 kusaidia kutoa taarifa za afya ya uzazi katika nchi zinazoendelea. Kwa sasa ni hiari ya mashirika ya kijamii kuhakikisha kuwa fedha zinatumika kwa umakini. (END/2013)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The element 'html' is used but not declared in the DTD/Schema.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>