Inter Press Service News Agency
Monday, June 18, 2018   10:52 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions


Kutumia Pamoja Maarifa ya Jadi Duniani Kote
Milagros Salazar

, Julai 15 (IPS) - Mji huu wa kaskazini mwa Australia uliwakusanya pamoja kupeana uzoefu. Ni jamii za jadi za kabila la Shipiba wanaopigania kukatwa kwa magogo kwa wingi katika msitu wa Amazon na wanajamii kutoka jamii ya Ando- Kpomey nchini Togo, ambao wanalinda msitu wa hekta 100. "Bila ya kuwa na msitu hatuna kitu tunachobaki nacho – ni kama kupoteza maisha yetu," alisema Juan Chávez, kutoka kabila la Shipibo mwenye asili ya India kutoka katika mkoa wa Ucayali nchini Peru, wakati wa mazungumzo na IPS wakati wa mapumziko katika mkutano wa Mtandao wa Makabila ya Wenyeji (WIN) ambao ulimalizika Jumatano Darwin, Australia.

Chávez na wengine wamefanya kazi katika kipindi cha miaka 15 iliyopita kuwezesha koo za makabila sita ya Shipibo kutokuhamasishwa kuingia katika uvunaji haramu wa magogo kutengeneza faida ya haraka, na kuwezesha kurejesha mila za makabila ya wenyeji katika kutunza misitu.

Ili kufanikisha hilo, waliandaa mipango ya maendeleo ya jamii, ili kufufua maarifa ya jadi ya jinsi ya kusimamia ardhi, maji na rasilimali za misitu, kwa msaada wa Chama cha Utafiti na Maendeleo (AIDER), NGO iliyopo nchini Peru.

Wawakilishi 1,200 wa makabila ya jadi kutoka baadhi ya nchi 50 waliangalia suala la mafanikio ya WIN katika siku ya tatu ya mkutano juu ya kufufua tamaduni za mababu na za jadi katika mazingira ya kuleta maendeleo endelevu na wala siyo kutegemea tu katika maarifa ya kisasa; pia ni muhimu kuangalia katika jamii zetu tunakotoka," anasema Chávez.

Baadhi ya mifano hii, kama ule wa Shipibo ilitolewa na Chávez, wameshinda zawadi ya Mpango wa Ikweta, ambao unaleta pamoja Umoja wa Mataifa, serikali, mashirika ya kijamii, biashara na mashirika yaliyojikita katika jamii ili kujenga maendeleo endelevu.

"Sisi siyo mashetani maskini; pia tunakuja na ufumbuzi," kiongozi wa makabila ya jadi wa Ecuador Manuel Tacuis alisema katika uwasilishaji wake katika moja ya topiki kwenye WIN. Ujumbe kutoka Ecuador ulikuwa mkubwa zaidi kutoka Amerika Kusini, pamoja na Brazil.

Wakati wawakilishi wa jamii za jadi kutoka duniani kote wakibadilishana uzoefu, imekuja kuwa wazi zaidi kuwa maisha ya kila siku na changamoto zinazokabili watu wa vijijini barani Afrika hazitofautiani sana na zile zinazowakabili wakazi wa jadi katika misitu minene ya Amazon.

Jamii ya Ando-Kpomey katika taifa la Afrika Magharibi la Togo ilianza miaka kumi iliyopita kurejesha msitu katika ardhi yao, ambao ulikuwa umeangamizwa na uchomaji wa moto katika uoto wa asili kunakofanywa na wawindaji.

Koku Agbee Koto, mwakili mwenye miaka 35 na hamasa kubwa kutoka jamii hiyo, aliiambia IPS kuwa mbinu za uharibifu hatimaye zimepunguzwa kwa kiasi kikubwa.

Hadi sasa zaidi ya hekta 100 za msitu zimerejeshwa na kufaidisha wanakijiji wapatao 2,500, alisema.

Lakini wawakilishi wa Togo na Peru walikubaliana kuwa maarifa ya jadi hayakutosha kuweza kusimamia ardhi kwa njia endelevu zaidi na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

"Inabidi tukubaliane na tamaduni zote: tamaduni za wenyeji na sayansi," alisema Chávez, baada ya kukubali kuwa bado kuna upinzani miongoni mwa watu wake kutambua mchango wa sayansi.

Wajumbe wa makabila ya wenyeji wanaoshiriki katika mkutano wa WIN walionyesha kuwa wawazi.

Koto, kutoka Togo, alikuwa akiandika kila kinachozungumzwa katika mkutano huo, na kutumia Kiingereza chake kidogo alicho nacho kuuliza kutaka taarifa zaidi, kuomba namba za simu na anuani za barua pepe, " anasema Chávez, wakati ameweza kuzungumza kiurahisi kwa Lugha ya Kifaransa alipokutana na washiriki kutoka nchi zinazoongea Kifaransa kutoka bara la Afrika.

Koto alishangazwa na mafanikio ya utalii ekolojia katika jamii ya Anja Miray nchini Madagascar, jambo ambalo alihisi lingeweza kuigwa na kijiji chake.

Jamii ya hifadhi ya Anja imeweza kusimamia utalii ekolojia na msitu, mshindi mwingine wa Tuzo ya Ikweta, na hivyo kuzalisha kipato kwa ajili ya wazee, watoto na jamii za wanyonge, ambao wanasaidiwa huduma za msingi na ufadhili, wakati wakirejesha hadhi ya msitu na kupunguza ukataji miti na kuenea kwa jangwa.

Víctor Samuel Rahaovalahy, mmoja wa viongozi katika jamii hiyo inayoongozwa na chama cha Anja Miray, aliiambia IPS kuwa bado walikuwa wakifanya kazi ya kutafuta jinsi ya kuzalisha kipato zaidi na njia bora zaidi za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

"Tunahitaji kujengea jamii uwezo zaidi, lakini pia kwa jamii zinazotuzunguka," Rahaovalahy alisema. "Sote tutapaswa kuja pamoja kupambana na kuenea kwa jangwa katika njia bora zaidi," aliongeza, akisema kuwa jamii za jadi na serikali lazima kufanya kazi pamoja kwa karibu ili kupata matokeo mazuri.

Siyo washiriki wote walikuwa wanajua fika jinsi ya kukabiliana na mambo mabaya yanayojitokeza katika maeneo yao au jinsi ya kukabiliana na changamoto kama madhara ya mabadiliko ya tabia nchi.

Kwa kipindi cha zaidi ya muongo mzima, watu wa kabila la Sami kaskazini mwa Sweden wamekabiliwa na hali isiyokuwa ya kawaida ya barafu kutokana na mabadiliko ya tabia nchi. Lakini bado hawajakusanyana pamoja kukabiliana na mabadiliko ya haraka kwa njia ya kujipanga zaidi, pamoja na maarifa ya jadi waliyonayo, mwanabaolojia Berit Inga, ambaye ana asili ya kabila la Sami, aliiambia IPS.

Inga alisema kabila la Sami walikuwa wanakabiliana zaidi na mabadiliko ya papo kwa papo, kama vile shughuli za uchimbaji wa madini.

Lakini kila mmoja katika mkutano alikubaliana kuwa haikuwa rahisi kuja na ufumbuzi kwa kujitenga.

Meneja wa Mpango wa Ikweta, Eileen de Ravin, aliiambia IPS kuwa uzoefu wa jadi wenye mafanikio unapaswa kuigwa na serikali katika kuandaa sera za umma ambazo zinatambua na kuthamini maarifa ya jadi.

Katika muongo uliopita, miradi ya makabila ya jadi 152 kati ya 2,500 ilishinda tuzo ya Mpango wa Ikweta. Wawakilishi wa mashirika ya washindi walikutana katika mkutano kujadili mipango ya baadaye ya WIN. (END/2013)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The element 'html' is used but not declared in the DTD/Schema.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>