Inter Press Service News Agency
Wednesday, April 01, 2015   04:08 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   JAPANESE
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions


Vijana Wasema ni Rahisi Kupata Coca Cola Kuliko Kondomu
Stella Paul

KUALA LUMPUR, Julai 12 (IPS) - "Kama nina kiu na nataka chupa ya Coca-Cola naweza kupata kiurahisi, bila kujali nipo katika dunia gani wakati huo. Lakini ni kwa nini ni vigumu kupata njia za uzazi wa mpango au huduma za afya ya uzazi?" aliuliza Carlos Jimmy Macazana Quispe, mwakilishi wa vijana kutoka nchini Peru ambaye kwa sasa yupo mjini Kuala Lumpur katika mkutano wa tatu wa kimataifa wa wanawake unaojulikana kama "Women Deliver" unaohusu afya na ustawi wa wanawake na watoto wa kike. Akiwa mwanachama wa NGO yenye makazi yake mjini Lima ya Instituto Peruano de Paternidad Responsable (INPPARES), ambayo inasaidia vijana wa Peru kujifunza kuhusu haki zao za kujamiiana na uzazi, Quispe alikuwa akielezea kuchanganyikiwa kwake kuwa asilimia 36 ya watu wenye umri wa kufanya mapenzi nchini Peru-wengi wakiwa vijana hawapati huduma za uzazi wa mpango.

Kuna mamia ya vijana kama Quispe wanaoishiriki katika mkutano wa siku tatu ambao ulianza Mei 28, wengi wao wakitoka nchi zilizoendelea za Asia, Afrika na Amerika Kusini ambako "njia za uzazi wa mpango " zinajulikana kuwa ni kondumu peke yake, hata hivyo mimba za umri mdogo zinazidi kuongezeka na ndoa za utotoni mara nyingi zinaonekana kama za kawaida katika jamii.

Mmoja wa mabalozi ni Shreejana Bajracharya, mshauri mtaalam wa vijana kutoka katika NGO ya Nepal ijulikanayo kama Ipas, inayofanya kazi ya kuzuia vifo na magonjwa yanyotokana na utoaji wa mimba usiokuwa salama nchini humo ambapo asilimia 21 ya mama wote wana umri chini ya miaka 18.

Bajrachayra, ambaye anatoa ushauri kwa vijana walioolewa na wasioolewa wanaofanya kazi viwandani kuhusu ngono salama, anasema kuwa zaidi ya asilimia 80 ya wanawake wenye umri wa kufanya ngono wanafanya ngono isiyokuwa salama na wana hatari ya kupata mimba kutokana na kuhofia kuwa njia za uzazi wa mpango zinaweza kudhuru maumbile yao.

"Nilikutana na kijana ambaye aliniambia kuwa vidonge vya uzazi wa mpango vinaweza kuua figo au moyo," aliiambia IPS, huku akiongeza kuwa: "Na hawa ni wanawake ambao wanaishi katika mji mkuu wa nchi Kathmandu. Kama kiwango cha ufahamu katika mji mkuu kiko chini kiasi hiki, fikiri itakuwaje kwa vijana wanaoishi maeneo ya vijijini."

Kwa mujibu wa Pablo Aguilera, mkuu wa shirika la mjini New York la HIV Young Leaders Fund, hali ni mbaya zaidi kwa jamii nyingi ambazo zinajibainisha kuwa zenye jinsia zaidi ya moja, au watu wanaoishi na VVU/UKIMWI.

Aguilera, ambaye yeye mwenyewe ni kijana anayeishi na VVU, alielezea matatizo mawili yanayofanana: siyo tu kwamba wako katika hatari ya kutokutambua taarifa muhimu juu ya ngono salama na afya ya uzazi, lakini pia wanakabiliwa na kutokutambuliwa, hawaonekani katika rada za tafiti wala jitihada nyingine za kubainisha walengwa katika jamii.

"Tunapaswa kushirikisha vijana wengi zaidi waliopo katika makundi ya pembezoni na jamii zinazonyanyapawa," aliielezea IPS, akiongeza kuwa vijana waliopo pembezoni lazima washirikishwe katika tafiti "siyo kama watu wanaohojiwa lakini kama watu wanaohoji wengine. Hii haitasaidia tu kupokea taarifa za awali kabisa, lakini pia itasaidia kuwahamasisha katika suala hilo kwa uharaka zaidi."

Wataalam wanaoongoza katika masuala ya afya ya uzazi wanatambua haja ya kuongeza jitihada. Babatunde Osotimehin, mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA), anakubaliana kuwa kuna uhaba wa takwimu za afya ya kujamiiana na uzazi, lakini anasema UNFPA inasaidia mashirika ya serikali duniani kote kutambua haja ya kutokomeza hali hii.

Hata katika wakati ambapo takwimu zipo, serikali hazizitumii kwa "malengo ya kiutendaji kama vile kupanga mipango, na hiyo ni changamoto kubwa," Osotimehin aliiambia IPS.

Jyoti Shreshtha, mwanafunzi wa udhamili kutoka Kathmandu, alisema serikali ya Nepali "haifanyi jitihada za kutosha za kutoa elimu" juu ya masuala ya vijana kama vile VVU/UKIMWI na haki za kujamiiana.

Katika nchi kama za Bangladesh, anasema kiogozi wa wanafunzi Umme Mahbuba, matukio na mikutano kuhusu mimba, ndoa za utotoni, ngono salama na matumizi ya uzazi wa mpango inalenga zaidi wasomi na wataalam. "Mara nyingi vijana hawahusishwi katika majukwaa haya kana kwamba masuala hayo siyo ya kwao," Mahbuba aliiambia IPS.

Hii kwa kiasi inaweza kuhusishwa na maneno ambayo yanazunguka mazungumzo ya afya ya kujamiiana. Kwa mujibu wa Faustina Fynn-Nyame, mkurugenzi mkaazi wa Taasisi ya Kimataifa ya Marie Stopes (MSI) nchini Ghana, vijana wanatengwa na matamshi kama ya "kupanga uzazi", ambayo hawawezi kuyaelewa.

"Kuna haja ya kuchukulia suala la mawasiliano kwa uzito mkubwa na kutumia maneno ambayo ni rafiki kwa vijana," alisema.

Lakini hakuna hata moja kati ya mbinu hizi za ushirikishwaji wa vijana zitakwenda mbali bila ya kuwekeza kwa kiasi kikubwa katika jitihada hii ya kimataifa.

"Kuna haja ya kuchukua hatua za haraka kuwekeza zaidi katika kujenga mbinu bora za mawasiliano na kujenga ujuzi wa mawasiliano," alisema Aguilera.

Baadhi ya nchi zinakabiliwa na matatizo ya kifedha na nyingine hazina matatizo hayo. Sinthuka Vive, mwanafunzi kutoka eneo lenye vita la Jaffna kaskazini mwa Sri Lanka, anasema serikali inajitahidi kufadhili huduma za afya ya uzazi.

"Wakati wa vita hospitali nyingi ziliharibiwa," aliiambia IPS. "Chache ambazo zilibaki zinajitahidi kutoa huduma kwa wanawake walioolewa. Vijana, wakati huo huo, hawana pa kwenda, hakuna anayewapatia ushauri nasaha wala taaarifa."

Suala la ufadhili limekuwa mjadala mkubwa katika mkutano unaoendelea nchini Malaysia, hasa juu ya ahadi zilizotolewa Julai 2012 katika mkutano wa kilele wa uzazi wa mpango mjini London, ambapo viongozi wa dunia waliahidi jumla ya dola bilioni 2.6 kutoa hudum za uzazi wa mpango kwa wanawake na watoto wa kike milioni 120 katika nchi maskini zaidi duniani ifikapo mwaka 2020.

Bado inasubiriwa kuona kama fedha hizo zitatolea kuboresha afya ya kujamiiana na uzazi wa mpango kwa vijana duniani kote. (END/2013)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
Activists Protest Denial of Condoms to Africa’s High-Risk Groups
Decent Employment Opportunities for Young People in Rural Africa
Kenya Struggles with Rising Alcoholism
Smugglers Peddle ‘Conflict Diamonds’ from Central African Republic, Ignoring Ban
Winners Announced for Free Expression Prize
Gates Foundation Slammed for Plan to Privatise African Seed Markets
Opinion: Water and Sanitation in Nigeria – Playing the Numbers Game
High-Tech to the Rescue of Southern Africa’s Smallholder Farmers
Sparks Fly As Sierra Leone’s VP Is Expelled From Party
Women Often Forgotten In Cases Of Forced Disappearance
More >>
  Dernières Nouvelles
News in RSS
Activists Protest Denial of Condoms to Africa’s High-Risk Groups
Decent Employment Opportunities for Young People in Rural Africa
Kenya Struggles with Rising Alcoholism
Smugglers Peddle ‘Conflict Diamonds’ from Central African Republic, Ignoring Ban
Winners Announced for Free Expression Prize
A lire également>>