Inter Press Service News Agency
Thursday, June 21, 2018   09:49 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions


Chini ya Ziwa Nyasa Kuna ‘Udongo wa Kipekee’
Thembi Mutch

ARUSHA, Tanzania , Mei 20 (IPS) - Jamii za Watanzania wanaopakana na Ziwa Nyasa hawana ufahamu mgogoro kati ya nchi yao na Malawi unahusu nini, wala ni nini cha umuhimu katika mgogoro huo, wakati jitihada za upatanishi kati ya Malawi na Tanzania zinategemewa kuanza hivi karibuni.

Ziwa lenye ukubwa wa kilomita za mraba 29,000, ambalo kwa upande wa Malawi linajulikana kama Ziwa Malawi, ni eneo la kitalii, chanzo cha mapato na chakula kwa wakazi wa eneo hilo. Lakini tangu Julai 2012, iligundulika kuwa ziwa hilo linaweza kuwa na utajiri mkubwa wa mafuta na gesi, na ugunduzi huu ulifufua upya mgogoro baina ya majirani hao wa kusini mwa Afrika juu ya umiliki wa ziwa hilo.

Malawi inadai inamiliki ziwa lote ambalo linabeba mpaka wa Malawi, Msumbiji na Tanzania. Wakati huo huo, Tanzania inasema asilimia 50 ya ziwa ipo upande wake.

Katika Mkoa wa Mbeya, kusini magharibi mwa Tanzania, wananchi wanaopakana na ziwa wamekuwa wakifanya kazi na NGO ya kitaifa ya HakiArdhi, kuelewa haki zao katika maji hayo.

"Tunajua kuwa tumekubali kutokukubaliana na Malawi katika jambo moja, lakini jamii hizi zinategemea kabisa ziwa hili kwa ajili ya uvuvi kuendesha maisha yao. Hakuna ushauriano kutoka kwetu kuhusu jinsi gani tutafaidika kama kutakuwa na mafuta hapa, hakuna kabisa. Tutapata nini kutokana na hili? Suala la ardhi ni jipya kwetu sisi: hatuna tunalolijua," Saad Ayoub, afisa mipango msaidizi wa shirika hilo, aliiambia IPS kwa njia ya simu.

Wakazi wa kandoni mwa ziwa wanaunga mkono maoni haya. Richard Kilumbo, mkazi kutoka wilaya ya Kyela, ambayo inapakana na Ziwa Nyasa, aliiambia IPS kuwa hana uelewa juu ya sababu za mgogoro huo.

"Tuna ndugu kutoka Mzuzu, Malawi na tulikuwa tukienda kushiriki harusi mwaka jana. Tunashtushwa na kuchanganyikiwa kuona tunaandaa vita dhidi ya majirani zetu. Hatujui ni kwa nini hili ni jambo kubwa miongoni mwa viongozi wetu. Tulisikia watu wakizungumza, tulidhani tulikuwa huru kutembea na kufaidi maisha," alisema.

Inaonekana kuwa tatizo lilianza mwaka 1890, wakati mkataba wa Heligoland ulipoligawa ziwa kwa mujibu wa sheria za kikoloni. Ulifanyiwa marekebisho mwaka 1982 na Umoja wa Mataifa. Hata hivyo, hivi karibuni mwezi Oktoba 2011 rais wa zamani wa Malawi marehemu Bingu wa Mutharika, alitoa zabuni kwa kampuni ya mafuta ya Uingereza ya Surestream Petroleum kuanzisha utafutaji wa gesi na mafuta mashariki mwa ziwa hilo, halafu zabuni nyingine ikatolewa Desemba 2012 kwa kampuni ya Afrika Kusini ya SacOil.

Mwezi Julai 2012, Tanzania ilitangaza kuwa, kwa kusaidiana na Denmark, inapanga kununua pantoni mpya ya thamani ya dola milioni tisa kuvuka maji ya Ziwa Nyasa. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Mijini wa Malawi alidai kuwa Tanzania haina haki ya kufanya shughuli zake katika maji ya Ziwa Malawi, kwani suala la umiliki na mgogoro wa mpaka haujatatuliwa. Katika majibu yake, Hilda Ngoye, mbunge katika bunge la Tanzania kutoka Mkoa wa Mbeya, alidai kuwa mashua za uvuvi na utalii za Malawi zinafanya kazi katika maji ya upande wa Tanzania.

Mambo yalibadilika kuwa mabaya wakati huo kaimu Waziri Mkuu bungeni nchini Tanzania, Samuel Sitta, alipotoa onyo kuwa nchi yake isingesita kujibu uchokozi wowote ule wa kijeshi.

Hadi leo hii, mbinu nyingi zimetumika kutatua mgogoro huo kati ya majirani hao wawili: upatanishi kwa kutumia Rais wa zamani wa Msumbiji Joaquim Chissano, mazungumzo makali juu ya kushambuliana kijeshi, vitisho kupeleka kesi hiyo katika Mahakama ya Usuluhishi ya Kimataifa, hoja ya kupeleka mgogoro kwa maaskofu wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika, na mazungumzo ya kidiplomasia kati ya mawaziri wakuu wa Tanzania na Malawi.

Lakini kumekuwepo na ukosoaji kuwa mgogoro huo umetumika kukuza umaarufu wa kisiasa, badala ya kuhakikisha kulinda maslahi ya wanajamii.

"Ziwa hili linapaswa kutumika kuboresha vipato na maisha ya wakazi wanaolizunguka katika pande zote. Ziwa ni rasilimali – badala yake linatumiwa kama sehemu ya mchezo wa kisiasa kukuza umaarufu wa kisiasa," mwandishi wa habari za mazingira nchini Tanzania na mtaalam aliyefuatilia habari hiyo kwa miaka mingi, na ambaye anaandikia magazeti kadhaa ya Kiswahili na katika blogu yake, Felix Mwakyembe, aliiambia IPS.

"Hakuna mgogoro wa mpaka kati ya wanajamii wanaozunguka ziwa, ni mgogoro kati ya wanasiasa, suala la kisiasa katika ngazi za juu, wanaotaka kuchaguliwa katika chaguzi za Malawi mwaka 2014 na Tanzania mwaka 2015. Kwa bahati mbaya, wanajamii wanageuka kuwa mateka. Wanakosa taarifa za kutosha na elimu kuelewa maana na ukubwa wa tatizo hili," Mwakyembe alisema.

Kilumbo anakubaliana naye.

"Kwa kweli hakuna shida katika jamii, hakuna kabisa. Wavuvi kutoka Tanzania wanafanya shughuli zao kama kawaida, na pamoja na kuwa tunajua suala hilo lipo katika taarifa za habari, hatujui linasababishwa na nini," alisema.

Masuala ya kutafuta rasilimali katika Ziwa Nyasa yanafanana na migogoro mingine kikanda linapokuja suala la umiliki, mgawanyo na utoaji wa leseni za utafutaji wa mafuta, na juu ya ni nani anayelipia mitaji ya uwekezaji.

Katika maeneo mengine ya Afrika Mashariki, kama vile Bonde la Albertine na Mbuga ya Maporomoko ya Murchison nchini Uganda, na Mbuga ya Virunga nchini Rwanda, kuna pande mbili za kuangalia mchakato huu – kusambaza taarifa za tathmini ya mazingira na kushirikisha kikamilifu wanajamii katika upangaji wa uchimbaji mafuta, na mgawanyo wa mafuta hayo".

"Sina ninalojua juu ya mipango ya mafuta, sijui kabisa. Na sijawahi kusikia kuhusu tathmini ya mazingira na sijawahi kuona ripoti ya aina hiyo," Kilumbo alisema. Akiwa anacheka, aliongeza: "Ni vigumu kujua mgogoro unahusu nini."

Ni kweli kabisa, haionekani wanajamii kuelewa mgogoro huu unahusu nini, wala haki zao katika mchakato huu ni nini.

Nyanda Shuli, meneja wa utetezi na vyombo vya habari wa asasi ya kiraia ya HakiElimu, aliiambia IPS kuwa msisitizo unapaswa kuwekwa katika uwajibikaji wa kifedha na uwazi, na kwamba kipato kinachoingia na uwekezaji lazima kuelekezwa kwa jamii.

"Bila kujali matokeo ya mgogoro huu ni nini, tunapaswa kufikiri na kukabiliana na suala kubwa la jinsi gani jamii zetu katika maeneo ya vijijini zinaendelea, kutafuta njia kwa watu kufahamu haki zao, na nini wanaweza kutarajia, kutoka jamii maskini kabisa zisizokuwa na nafasi kuzunguka Nyasa, hadi kwa jamii zilizopo mbali na ziwa.

"Lakini kwa sasa maamuzi yanatolewa katika makao makuu, Dar es Salaam, na hakuna uhusiano au mjadala wenye maana katika mikoa. Ni jambo gumu zaidi kwasababu umbali ni mkubwa mno, na usafiri, mitandao ya simu na barabara ni mibovu," alisema.

Katikati mwa kutokuelewana, kuna jambo moja ambalo linahitaji kukumbukwa. Kuna "udongo wa kipekee" chini ya ziwa, na uwezekano wa kupatikana kwa mafuta mengi na gesi asilia.

Hadi leo hii, hakuna ushahidi wa wazi kuwa jamii zinazozunguka ziwa, iwe upande wa Malawi au Tanzania, watakuja kufaidika na utajiri huo.

Lakini kwa wakati huu, Kilumbo ana imani kuwa kuna samaki wa kutosha kuvua.

"Ndiyo, naweza kusema Wamalawi wanapata samaki wengi, lakini hii inatokana na kwamba sisi Watanzania tunapenda samaki wadogo na wachanga. Lakini kuna samaki wa kutosha. Sijui kama kuna mipango ya kuchimba mafuta, sijui kabisa." (END/2013)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The element 'html' is used but not declared in the DTD/Schema.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>