Inter Press Service News Agency
Monday, June 18, 2018   10:52 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions


Watu Milioni Mbili Wameweka Matumaini yao Katika Usuluhishi wa Mgogoro wa Ziwa Nyasa
Mabvuto Banda

LILONGWE, Mei 20 (IPS) - Zaidi ya familia milioni mbili ambazo zinategemea Ziwa Nyasa kwa ajii ya kipato chao zinasubiri kwa hamu usuluhishi wa mgogoro wa ziwa hilo kati ya Malawi na Tanzania ili kukomesha mgogoro wa umiliki wa ziwa hilo.

Mchakato wa kutafuta ufumbuzi wa mgogoro huo baina ya pande husika utaanza mwezi Machi baada ya makubaliano ya mwezi Desemba ya nchi hizo mbili kutoa kibali kwa Jukwaa la Wakuu wa Zamani wa Afrika na Serikali, linaloongozwa na rais wa zamani wa Msumbiji Joachim Chissano kuendesha usuluhishi huo.

"Baada ya hatua kadhaa za kutatua mgogoro huo, tumekuja kukubaliana kuwa tumeshindwa na tunahitaji upande wa tatu kutusaidia," Katibu Mkuu katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Malawi, Patrick Kambabe, aliiambia IPS.

"Mwezi Januari, Malawi iliwakilisha msimammo wake baada ya kukubali kuwa Jukwaa hilo lingesaidia kutatua mgogoro huo," Kambabe alisema. 
 Katika mahojiano na vyombvo vya habari vya Tanzania, katibu mkuu wa wizara ya mambo ya nje ya Tanzania John Haule alithibitisha kuwa nchi yake pia imekubali kushirikisha viongozi wa zamani na imepeleka msimamo wake kwa Chissano.

"Jukwaa kwa sasa linapitia waraka wetu na baada ya hapo litatafuta taarifa zaidi kama zinahitajika," kwa mujibu wa Haule.

Alisema kuwa alitarajia kuwa suala hilo litatatuliwa katika kipindi cha miezi mitatu.

Kwa mujibu wa mamlaka, Wamalawi wapatao milioni 1.5 na Watanzania 600,000 wanategemea ziwa hilo la tatu kwa ukubwa barani Afrika kwa ajili ya chakula, usafiri na mahitaji mengine ya kila siku.

Wakati IPS ilipotembelea Wilaya ya Karonga, katika mwambao wa Ziwa Nyasa, jamii kuzunguka ziwa hilo zilisema zina wasiwasi kuhusu uhasama unaozidi kuongezeka na wanatarajia maridhiano kupatikana.

"Nilikuwa navuka mpaka kuingia Kyela nchini Tanzania kila baada ya wiki mbili kuuza sukari na kupata nguo, ambazo naziuza upande wa nchini kwetu. Lakini sasa nakwenda huko mara moja tu kwa mwezi kwasababu maafisa uhamiaji wa Tanzania katika mpaka wa Songwe wamekuwa wakali sana," alisema Joyce Nyirongo, mama wa watoto wanne.

Likijulikana kama Ziwa Malawi upande wa Malawi na Lago Niassa nchini Msumbiji, mgogoro wa ziwa hilo umeongezeka kutokana na hifadhi kubwa ya gesi na mafuta, kwa mujibu wa taarifa za karibuni za serikali ya Malawi.

Uwezekano wa kuwepo kwa mafuta na gesi kumeibua upya mgogoro wa mpaka kati ya Malawi na Tanzania, ambao umebaki bila kutatuliwa kwa karibu nusu karne.

Mgogoro ulienea Julai iliyopita wakati Malawi ilipotoa kibali cha kutafuta mafuta kwa kampuni yenye makao yake nchini Uingereza ya Surestream Petroleum.

Na Desemba mwaka jana Malawi ilitoa leseni nyingine kubwa kwa kampuni ya mafuta ya SacOil Holdings Ltd.kutoka Afrika Kusini, hatua ambayo imeongeza msuguano.

Mataifa hayo yamejaribu mara mbili kutatua mgogoro kwa njia za kidiplomasia lakini imeshindikana.

Mataifa yote mawili yanatarajia matokeo mazuri ambayo yatatatua mgogoro huo kabisa wakati mchakato wa usuluhishi utakapoanza mwezi Machi.

Madai ya mikataba ya kikoloni Rais wa kwanza wa Malawi, Hastings Kamuzu Banda, alikuwa wa kwanza kudai kuwa Ziwa Nyasa ni sehemu ya nchi yake. Alikuwa akitoa madai yake hayo kutokana na mkataba wa 1890 unaojulikana kama Mkataba wa Heligoland kati ya Uingereza na Ujerumani, ambao ulielezea kuwa mpaka kati ya nchi hizo mbili uwepo upande wa Tanzania wa ziwa hilo.

Mkataba huo uliridhiwa katika Mkutano wa Kilele wa Umoja wa Nchi Huru za Afrika mwaka 1963 nchini Ethiopia na ulikubaliwa shingo upande na Tanzania.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Malawi Ephraim Chiume aliiambia IPS kuwa msimamo wao unajikita katika Mkataba wa 1890 na kuwa Umoja wa Afrika mwaka 2002 na 2007 ulipitisha azimio la kuendeleza mkataba huo wa kikoloni.

"Mkataba wa Heligoland ulitupatia ziwa lote sisi na huu ndiyo msingi wa msimamo wetu na uthibitisho kuwa ziwa lote ni la kwetu," alisema Chiume.

Msimamo wa Tanzania ni kwamba mkataba huo una mapungufu. Tanzania imebakia na msimamo kuwa inamiliki nusu ya ziwa hilo – ikisema kuwa mpaka kati ya nchi hizo mbili upo katikati mwa ziwa ukiondoa sehemu ya taifa la Msumbiji.

Msimamo wa Tanzania ni kuwa mpaka upo katikati mwa ziwa, na kusisitiza kuwa hii ni kanuni inayofuatwa kama nchi zinamiliki bodi ya maji kwa pamoja.

"Tanzania inafuata sheria za kimataifa, ambazo zinasema kuwa mipaka kwa ujumla inakuwa katikati mwa maji … kwa sababu hiyo Tanzania inamiliki nusu ya ziwa," Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Benard Membe aliiambia IPS katika mahojiano kwa njia ya simu.

Membe alisema mkataba una mapungufu kwasababu umewanyima Watanzania wanaoishi kandokando mwa ziwa haki zao za kutumia maji na rasilimali za majini kuendesha maisha yao ya kila siku.

Hii ni misimamo ambayo Chissano na wenzake wawili; rais wa zamani wa Afrika Kusini Thabo Mbeki na rais wa zamani wa Botswana Ketumire Masire watayapitia.

Suala la Kimazingira Wakati huo huo, mgogoro huo pia umeibua suala la madhara ya kuchimba mafuta katika ziwa hilo la maji baridi ambalo limejaliwa kuwa na aina tofauti zaidi ya 2,000 ya samaki, ambalo linavutia pia wapiga mbizi kutoka duniani kote.

Wanamazingira nchini Malawi wana wasiwasi uchimbaji wa mafuta utaharibu bayoanuai ya ziwa hilo inayovutia utalii wa kimazingira na mazingira ya ziwa hilo na hivyo kuathiri mikoa inayotegemea uvuvi kaskazini mwa nchi.

"Utahatarisha maisha ya mamilioni ya watu kijamii na kiuchumi ambao moja kwa moja wanategemea maji ya ziwa hilo, usafiri na suala la msingi zaidi protini inayotokana na samaki," alisema Reginald Mumba wa shirika lisilokuwa la kiserikali la Hifadhi ya Mazingira.

Baada ya mazungumzo baina ya nchi hizo mbili kushindikana mwishoni mwa mwaka jana, Rais wa Malawi Joyce Banda alielezea nia yake ya kupeleka suala hilo Mahakama ya Usuluhishi ya Kimataifa.

Wanasiasa na wavuvi kwa pamoja kwa sasa wana matumaini yao kuwa mchakato wa maridhiano utaleta suluhisho la amani la mgogoro huo bila hata kuhusisha mahakama hiyo. (END/2013)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The element 'html' is used but not declared in the DTD/Schema.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>