Inter Press Service News Agency
Monday, June 18, 2018   10:49 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions


Mgogoro wa Ziwa Nyasa Wazua Hofu kwa Wavuvi
Mabvuto Banda

KARONGA, Malawi, May 6 (IPS) - Tangu akiwa na umri wa miaka tisa, Martin Mhango kutoka kijiji cha Karonga kaskazini mwa Malawi hajawahi kufahamu njia nyingine ya kumwingizia kipato zaidi ya uvuvi. Na katika kipindi cha miaka 33 iliyopita amekuwa akivua samaki kwa uhuru katika Ziwa Nyasa – hadi Oktoba mwaka jana alipokamatwa na kuweka kizuizini na kupigwa na vikosi vya usalama vya Tanzania.

"Walinikamata, wakanichukua hadi ufukweni ambako walinipiga na kuniweka kizuizini. Waliniambia kuwa nimevuka mpaka kinyume cha sheria na nilikuwa navua samaki katika upande wa Tanzania," Mhango, 42, aliiambia IPS. "Pia niliambiwa nisivue tena samaki katika upande wao tena. Amezoea kuvua samaki katika pande zote za ziwa kwa miaka mingi, alisema, kama ilivyo kwa wenzake wavuvi kutoka nchini Tanzania.

Mgogoro dhidi ya ziwa la tatu kwa ukubwa barani Afrika ambalo linajulikana kama ziwa Nyasa nchini Tanzania na Ziwa Malawi kwa upande wa Malawi umeanza katika kipindi cha nusu karne iliyopita.

Malawi inadai kumiliki eneo zima la ukubwa wa kilomita za mraba 29,600 za ziwa hilo ambalo mipaka ya mataifa ya Malawi, Msumbiji na Tanzania hupitia humo.

Wakati huo huo, Tanzania inasema asilimia 50 ya ziwa hilo ipo nchini mwake.

Mgogoro wa mataifa hayo ya kusini mwa Afrika ulifumuka wakati Malawi ilipotoa kibali cha kutafuta mafuta kwa kampuni yenye makao yake nchini Uingereza ya Surestream Petroleum mwaka 2011 kutafuta uwezekano wa kuwepo kwa mafuta na gesi katika Ziwa Nyasa.

Mamlaka nchini Tanzania yanataka kampuni ya Surestream Petroleum kuachana na mipango yoyote ile ya kuchimba mafuta na gesi katika ziwa linalogombaniwa hadi mgogoro utakapotatuliwa. Lakini Malawi imekataa kutii amri hiyo.

Mwezi Desemba mwaka jana, serikali ya Malawi ilitoa leseni ya pili kubwa zaidi ya kutafuta mafuta kwa kampuni ya Afrika Kusini ya SacOil Holdings Limited.

Hadi sasa makampuni hayo mawili bado hayajaanza kuchimba kutafuta mafuta yanajaribu tu kuchunguza kitovu cha ziwa ambacho kimejificha.

Lakini familia nyingi za wavuvi kama ile ya Mhango ambazo zinafanya kazi zao katika Mto Songwe kaskazini mwa Malawi tayari zimenaswa katika mtego huu, na hivyo kuwafanya wavuvi kuwa na hofu kuwa nchi hizo mbili zinaweza kutumbukia katika vita.

Baada ya tukio la Oktoba, Mhango amekuwa mwangalifu sana asiweze kuvuka maji yanayosemekana ni ya upande wa Tanzania, jambo ambalo limeathiri kipato chake.

Kupungua kwa samaki kumepunguza kipato chake kutoka zaidi ya dola 286 kwa mwezi hadi dola 142.

"Nimekuwa nikiendesha maisha yangu yote kwa kutegemea uvuvi na hii ni mara ya kwanza siwezi kuvua samaki kwa uhuru katika ziwa hili na nahofia mustakabali wa maisha yangu ya baadaye," alisema.

Josiah Mwangoshi, 52, anakumbuka alikuwa mwenyeji wa vijiji viwili wakati alipokuwa akikua – kijiji kimoja upande wa Malawi na kingine upande wa Tanzania.

"Kijiji changu kipo kando mwa Mto Songwe na nakumbuka kuwa mto ulipobadilisha mwelekeo wake, tuliweza kuhamia upande wa Tanzania na baadaye kurejea upande wa Malawi wakati mto ulipobadili mwelekeo tena," Mwangoshi aliiambia IPS.

"Lakini sasa nahofia Watanzania wanaweza kunimakata. Siwezi tena kuishi kwa kuvua samaki katika upande wa Tanzania ambako pia nina familia yangu, kwasabau ni wazi sasa kuwa mgogoro umezidi kukua," alisema.

Madai ya kupigwa na kubughudhiwa kwa wavuvi wa nchini Malawi mwezi Oktoba mwaka jana yalisababisha Rais wa Malawi Joyce Banda kukatisha mazungumzo ambayo yameshaanza baina ya nchi hizo mbili.

Mgogoro ulizidi wakati mwezi Novemba mwaka jana Tanzania iliposambaza ramani ambayo inaonyesha mpaka kati ya Tanzania na Malawi upo katikati mwa ziwa hilo.

Banda, akikasirishwa na ramani hiyo na kubughudhiwa kwa wavuvi wa nchini mwake na Tanzania, aliitisha mkutano wa waandishi wa habari katika mji mkuu wa Lilongwe siku chache baadaye na kutangaza kuwa amepeleka suala hilo kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na kufuta mpango wake wa ziara yake ya kitaifa kuitembelea Tanzania.

Lakini Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Patrick Tsere, alitetea hatua ya nchi yake akisema kuwa hakuna wavuvi wa Malawi ambao wamewahi kubughudhiwa katika maji ya ziwa hilo kwa upande wa Tanzania.

"Vyombo vya usalama nchini Tanzania havijahusika katika tabia hiyo. Ni sisi ambao tumekuwa na mashaka kuwa ndege za Malawi zimekuwa zikiruka katika upande wa Tanzania bila ruhusa," Tsere aliiambia IPS.

Wengi wana imani kuwa mgogoro wa ziwa hilo utakuwa mbaya zaidi kama mafuta na gesi vitagunduliwa.

"Mgogoro huu umekuwepo kwa zaidi ya miaka 50 lakini umeongezeka na kuingia katika masuala makubwa ya mjadala wa umma sasa kwasababu ya uwezekano wa kuwepo kwa mafuta na gesi," Udule Mwakasungura, mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha Haki za Binadamu, NGO iliyopo nchini Malawi, aliiambia IPS.

"Ziwa Nyasa lina aina tofauti ya samaki zaidi ya 2,000 — hofu yetu ni kwamba utafutaji wa mafuta na uchimbaji wake utaathiri bayoanuai katika maji hayo ya baridi," aliongeza.

Ziwa hilo limeshuhudia kupungua kwa idadi ya samaki kutoka tani 30,000 kwa mwaka hadi tani 2,000 katika kipindi cha miaka 20, kwa mujibu wa ripoti ya hivi karibuni ya Wizara ya Kilimo nchini Malawi iliyosomwa bungeni mwezi Februari.

Mwezi uliopita, mataifa yote mawili yaliwakilisha misimamo yao baada ya kukubaliana kuwa mgogoro huo utapatanishwa na wakuu wa zamani wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika, ambao pia wanajulikana kama Jukwaa la Afrika.

"Tumekubaliana na Tanzania kuwa tutawakilisha suala hili kwa Jukwaa la Afrika na tumeshawasilisha misimamo yetu. Mchakato wa upatanishi utaanza kabla ya mwisho wa mwezi huu au mwezi Machi," Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Malawi, Patrick Kabambe, aliiambia IPS.

Mhango na Mwangoshi wanaweka matarajio yao katika jitihada za upatanishi.

"Nimekuwa nikifuatilia habari za suala hili kupitia redio na maombi yangu ni kuona viongozi wa zamani wa Afrika wanatatua suala hili kabisa," alisema Mwangoshi.

Mhango ana matumaini kama hayo. "Ninachotaka tu ni kurejea na kuanza shughuli zangu za kuvua kwa uhuru katika ziwa hili — kwasababu bila ya kufanya hivyo, maisha ya baadaye ya familia yangu yatakuwa gizani." (END/2013)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The element 'html' is used but not declared in the DTD/Schema.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>