Inter Press Service News Agency
Monday, June 18, 2018   10:42 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions


Timbuktu Yarejesha Hazina Zake
A. D. McKenzie

PARIS,, May 2 (IPS) - Pamoja na hali tata na vita vinavyoendelea, Mali itafanya kazi ya kujenga na kulinda urithi wake wa kitamaduni, anasema waziri wa utamaduni wa taifa hilo la Afrika Magharibi Bruno Maïga. Maïga alikuwa mjini Paris akihudhuria "siku ya mshikamano na Mali" iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) katika makao yake makuu hapa. Tukio hilo lilikusanya pamoja wataalam wa masuala ya utamaduni, wakuu wa serikali, wanasanaa na wasomi kutathmini uharibifu uliofanyika katika maeneo ya urithi wa kitamaduni ya Mali na maandiko ya kizamani, na kuandaa mpango wa kuchukua hatua.

"Wapiganaji wa jihadi…kwa kuchoma moto maandiko ya zamani, kuzuia masuala ya jadi katika mikoa wanayoikalia, kuzuia watu wasisikilize muziki, kupandikiza hofu …walitaka kutuvunja moyo, kuvunja hisia zetu za kitamaduni," Maïga alisema. "Lengo lao lilikuwa kuharibu zamani yetu, utamaduni wetu, utambulisho wetu, na kwa ujumla wake, utu wetu."

Maïga aliiambia IPS kuwa alikuwa na matumaini kuwa siku hiyo itaanzisha mwanzo wa kujenga upya urithi wa Mali. "Natumaini kutakuwa na hatua thabiti, na hiyo ndiyo sabababu nimekuja hapa, pamoja na matatizo yote yanayoikabili nchi yetu."

Makaburi ya zamani kumi na sita na misikiti mikubwa mitatu katika mji wa kihistoria wa Timbuktu yaliwekwa katika urithi wa dunia wa UNESCO mwaka 1988. Kaburi la Askia katika mji wa Gao, ambalo lilijengwa mwaka 1495, liliongezwa katika orodha hiyo mwaka 2004.

Mwezi Julai mwaka jana kaburi hili na msikiti wa Sidi Yahi liliingizwa katika orodha ya vitu vilivyopo hatarini kufuatia kuvunjwa kwa makaburi 11, na milango ya Sidi Yahi.

Uvunjaji huo uliohusishwa na waasi wa Kiislam – ulifanyika wakati wa mwaka wa vita ambayo ilianza kaskazini mwa Mali Januari 2012. Wakati vikosi vya Kifaransa na Mali vilipochukua mji wa Timbuktu mwishoni mwa Januari mwaka huu, waasi waliorudi nyuma walichoma moto Taasisi ya Ahmed Baba, na kuvunja baadhi ya maandiko ya thamani ya zamani ambayo yalikuwa yakihifadhiwa hapo.

Maïga aliwaambia waandishi wa habari kuwa maandiko ya zamani yapatayo 2,000 hadi 3,000 inawezekana yalipotea lakini nyaraka nyingine zinazokadiriwa kuwa 300,000 zimehifadhiwa katika mahali salama. Alikataa kutoa mahali zilipohifadhiwa nyaraka hizo kutokana na sababu za kiusalama. Maandiko hayo mengi yameandikwa katika karne za 13 hadi 16 na yaliandikwa na wanazuoni maarufu kutoka jiji hilo na maeneo mengineyo.

Maandiko hayo yalikuwa katika mchakato wa kuwekwa katika kompyuta, lakini waasi walivunja kompyuta na vifaa vingine vilivyofungwa kwa ajili ya kazi hiyo, Maïga alisema. "Walivunja kila kitu," aliiambia IPS, akiongeza kuwa mchakato wa kuingiza kwenye kompyuta bado ni kipaumbele kwa wizara ya utamaduni, mara tu amani itakaporejea.

"Mali ina utamaduni mkubwa na historia ambayo inahifadhi mshikamano wa kijamii," Maïga alisema. "Kwa mamia ya miaka, jamii mbalimbali zimeishi pamoja zikiwa na tamaduni tofauti. Ni kutokana na tamaduni hizi tofauti, kumekuwepo na moyo huu wa uvumilivu, na ubunifu huu …ambao waasi wa Kiislam wamejaribu kuuvunja. Lazima tupingane na jambo hili."

Kufuatia siku ya mazungumzo, Mali na washirika wake walipitisha rasimu ya mpango wa utekelezaji kwa ajili ya "ujenzi upya wa urithi wa utamaduni na kulinda maandiko ya zamani." Lazare Eloundou, mkuu wa Kituo cha Urithi wa Dunia barani Afrika katika UNESCO, alisema kuwa gharama za kuingiza kwenye kompyuta maandiko na kujenga upya makaburi zilikadiriwa kufikia kati ya dola milioni 10 na dola milioni 11.

Alisema kuwa shirika hilo limefungua akaunti maalum ya benki kupokea fedha kwa ajili ya kazi iliyopo mbeleni, na siku ya mshikamano ilikuwa na maana ya kutangaza juu ya haja ya kuchangia mpango huo kutoka kwa wahisani binafsi na wa umma.

Aurélie Filipetti, waziri wa utamaduni na mawasiliano wa Ufaransa, ambaye alihudhuria sherehe za ufunguzi, alisema kuwa taasisi za Ufaransa zitashiriki katika kutoa mafunzo kwa wataalam wa utamaduni wa Mali katika maeneo ya uhifadhi na urejeshaji wa urithi wake.

"Mali ni sehemu muhimu ya vyanzo vya sanaa, utamaduni na masuala ya kiroho, na jukumu la Ufaransa, la UNESCO na jumuiya nzima ya kimataifa ni kusaidia watu wa Mali kutambua utu wao na fahari ya utamaduni wao," Filipetti aliwaambia waandishi wa habari.

"Wakati Ufaransa ilipoingilia kati katika mgogoro huo, ilikuwa ni kwa ajili ya kulinda heshima ya taifa la Mali na zaidi ya hapo kulinda watu wa Mali," Filipetti aliongeza. "Na watu wa Mali wanahitaji urithi na utamaduni wao."

Taasisi kama ile ya mjini Paris ya Quai Branly Museum, ambayo inalenga katika sanaa na ustaarabu wa jadi, na Maktaba ya Taifa ya Ufaransa watatoa maarifa yao kurejesha na kujenga upya maeneo hayo, Filipetti alisema.

"Hakuna kanuni ya kiroho au ya kiharakati ambayo inaweza kuwa na sababu ya kunyima watu historia yao," alisema.

Wakati mapigano yakiendelea, huku kukiwepo na mashambulizi ya kila upande, wataalam wanahofia kuwa sanaa za kitamaduni za Mali zitakuwa sehemu ya biashara haramu ya kimataifa ambayo ina thamani ya dola bilioni 6 hadi 8 kwa mwaka.

Wakuu wa UNESCO walisema baadhi ya vitu tayari vinaaminika kuwa katika soko, lakini shirika hilo lina matumaini kuwa serikali za nchi jirani zitachukua hatua kuzuia vifaa hivyo kuingia nchini mwao.

Mkurugenzi mkuu wa UNESCO Irina Bokova alisema kuwa shirika lake lingefanya kazi na washirika wengine na shirika la polisi la kimataifa la Interpol kuzuia uuzaji wa vifaa hivyo. Pia alisisitiza umuhimu wa utamaduni kwa mataifa.

"Tunataka kupeleka ujumbe wenye nguvu kuhusu umuhimu wa utamaduni, umuhimu wa urithi," aliwaambia waandishi wa habari. "Ujumbe ambao unapinga uharibifu wa urithi kwasababu unaangamiza utambulisho wa watu."

Bokova, ambaye alitembelea Mali mwanzoni mwa mwezi wa Februari akiwa na rais wa Ufaransa François Hollande, alisema aliona kwa macho yake kuchomwa moto kwa maandiko ya kale.

"Kwetu sisi, Timbuktu, Gao, urithi wa Mali ni vitu vinavyokwenda mbali zaidi ya kuorodheshwa katika Urithi wa Dunia kwasababu vinaonyesha maendeleo ya ustawi wa Uislam, na mjadala miongoni mwa tamaduni. Maandiko ya kale yana rikodi za sayansi ya Uislam, madawa, utabiri wa nyota, masuala ya kiroho, masuala ya falsafa," Bokova alisema. (END/2013)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The element 'html' is used but not declared in the DTD/Schema.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>