Inter Press Service News Agency
Thursday, June 21, 2018   09:51 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions

Maswali na Majibu
Redio yawapatia Sauti Vijana wa Adeika Kusini - Gives a Voices to South African Youth
Joan Erakit

UMOJA WA MATAIFA, May 2, (IPS) - Lesedi Mogoatlhe amejitolea maisha yake katika kuwawezesha vijana wa Afrika kwa kuwafanya sauti zao zisikike kupitia uandishi wa habari wa redio.Katika wakati wa changamoto za kiuchumi, kisiada na kitamaduni, vijana wa Afrika Kusini wanakabiliwa na masuala magumu mno. Wakiwa vijana wadogo wanahofia juu ya mustakabali wa marafiki zao, familia, elimu na maisha ya jamii, lakini wakiwa kama Waafrika Kusini pia wanakabiliwa na ukweli wa umaskini mkubwa, magonjwa na ghasia.

Mkufunzi wa shirika la Children's Radio Foundation (CRF) nchini Afrika Kusini, Mogoatlhe anaelekeza nguvu katika kujenga maslahi katika masuala ya kijamii, kufufua fikra za kimapinduzi na kujenga mawasiliano.

"Inatia majaribu kuorodhesha idadi ya changamoto na kukosekana kwa usawa ambako kunawakabili watu katika bara, kuzungumzia kuhusu jinsi gani rasilimali zinatumiwa vibaya, au jinsi gani rushwa imekuwa kitu cha kawaida kwa viongozi wa Kiafrika," Mogoatlhe aliiambia IPS, "Lakini hii inaonekana kuwa jambo gumu kama siwezi kuchangia kutoa ufumbuzi wa matatizo haya."

Kuwa na sauti ni jambo muhimu kuwa na chanzo cha kipato, na kwa kupitia mashirika kama la Children's Radio Foundation na wakufunzi kama Mogoatlhe, vijana wengi zaidi watawezeshwa kuwa na ujuzi wa mawasiliano ambao hautawasaidii tu kusema jinsi wanavyoyaona mambo.

Joan Erakit alizungumza na Mogoatlhe juu ya kazi yake katika uandishi wa habari wa redio kwa vijana nchini Afrika Kusini na faida yake kwa maisha ya vijana. Sehemu ya mahojiano yao yanafuata.

Swali: Unawapatia vijana mafunzo ili kuwapatia uwezo siyo wa kwao binafsi tu ila pia kwa ajili ya jamii zao kupitia uandishi wa redio. Mwelekeo mlioanza kuuona ukoje?

Jibu: Vijana wanaotoka mazingira ya vijijini wana njaa ya maarifa zaidi kuliko wa mjini. Wanaonekana kuelekeza nguvu zaidi katika masomo na kuvutiwa na fursa zinazokuja upande wao, na wanaonekana kuwa wazuri katika kujipanga na kutumia kila jukwaa ambalo redio inaleta kwao.

Pia nimegundua kuwa wasaa wa kwanza kuwawezesha vijana ni pale wanapokuwa na kipaza sauti cha kuzungumzia. Kitu ambacho kinawafanya kutoa sauti zao na kusikika kinawafanya kuinua kila kitu.

Swali: Vijana unaofanya nao kazi wanakabilianaje na changamoto za kiuchumi, kisiasa na kitamaduni nchini?

Jibu: Pia ni vigumu kujibu swali hili kwa niaba ya vijana wa Afrika Kusini. Katika baadhi ya jamii, vijana wana wasiwasi kuhusu kuwa na maji ya bomba na chakula. Katika kaya nyingine, vijana wana wasiwasi juu ya kushindwa kuboresha programu zao katika simu za iPhones.

Lakini suala moja ambalo ni la wazi katika dhana yetu ya pamoja ni kukosekana kwa majukwaa kwa ajili ya kutoa sauti zetu kusikika, majukwaa ambapo tunaweza kuzungumza mambo yetu ya kila siku ambayo yanatukabili yanayohusu elimu, ubaguzi wa rangi, jinsia, ghasia, unyanyapaa au kukosekana kwa fursa za ajira.

Jitihada zetu siyo kama rangi ya kijani na nyeupe kama ilivyo kwa wazazi wetu chini ya ubaguzi wa rangi. Wazazi wetu waliuliza, "Ni lini tutapata uhuru?" Sisi tunauliza, "Uhuru ni nini?"

Swali: Je vijana wanahisi sauti zao zinasikika, aidha kupitia redioni au nje ya redio?

Jibu: Kwa vijana wengi wa Afrika Kusini, baadhi wanatoka maeneo ya vijijini ambako hawapati habari, na masuala ambayo yanawapa changamoto hayaandikwi kwenye vyombo vya habari. Wana uwakilishi mdogo katika vyombo vya habari. Kuwahoji watu wazima majumbani na katika jamii ni suala ambalo haliwezi kusikika, na maoni yao hayachukuliwi wakati maamuzi muhimu yanapotolewa katika jamii.

Kupitia mradi wa redio ambao tumeanzisha, vijana wanazungumzia kuhusu mimba za utotoni, matumizi makubwa ya pombe, kuishi na VVU na mambo haya yana maana gani katika jamii na katika maisha yao.

Wanatueleza kuwa mawazo waliyokuwa nayo ya zamani yanabadilika kupitia redio, badala ya kuitwa majina vijana wasiokuwa na heshima na wavivu, sasa wanaonekana kama viongozi na mabalozi wa jamii zao.

Swali: Katika kazi yako, unawezaje kuzungumzia suala la kuishi na VVU?

Jibu: Kwa sasa natoa mafunzo kwa kikundi cha vijana wanaoishi na VVU kutoka Khayelitsha ili kuwa waandishi wa redio. Mchango wangu ni kuhamasisha kutoa maoni yao, kujifunza, kuwapatia ujuzi na kuwakumbusha mazuri na mabaya ambayo yanaweza kusababishwa na habari zao wanazotangaza katika jamii.

Kama mwanafunzi anataka kuelezea hali yake ya kuathirika kutokana na kuhisi ana usalama kutokana na kwamba hawezi kujulikana kupitia redioni, nawataka kufanya hivyo kwa kujificha. Huwa sijihusishi katika kujaribu kutatua masuala ambayo yanakuja.

Katika mradi huu, mwezeshaji mwenza ni mshauri nasaha wa VVU na pia ni mwanaharakati, mtu anayeaminiwa na vijana. Pia tunaanza kutoa mafunzo juu ya usiri na maadili; tunatengeneza sheria za chombo cha habari ambazo zitatufanya kuaminiani miongoni mwetu.

Swali: Shirika kama la CRF ni muhimu kwa kiasi gani?

Jibu: Kazi ambayo CRF inafanya ni muhimu kwasababu inalenga vijana ambao wana maisha magumu na fursa chache. Kupitia mradi wa redio, siyo tu kwamba vijana wana nafasi ya kutoa sauti zao katika habari wanazoandaa na maoni, lakini pia wanajifunza mawasiliano, redio na utafiti wa mambo ambayo yanaweza kuwapatia fursa katika maisha yao ya baadaye.

Kupitia redio, vijana wanaweza kuuliza maswali juu ya nini hakifanyi kazi katika jamii yao, wanatafuta ufumbuzi na kuhubiri mabadiliko; wanakuwa wakala wa mabadiliko katika jamii. Wana uwezo wa kuwasiliana kwa lugha zao za kienyeji na kujifunza kuhusu nini kinajitokeza katika jamii zao pia.

Hivi karibuni tulizindua Mtandao wa Waandishi Vijana Afrika Kusini ambao unahusu vijana 15 kutoka redio tofauti 12 nchini. Vijana wanatengeneza vipindi vya kila wiki vinavyolenga katika masuala ya jamii, na wanaonyeshana vipindi hivi miongoni mwao kupitia jukwaa la kijamii la kubadilishana vipindi vya redio la Soundcloud. Kupitia mfumo huu, wanaweza kutoa taarifa za nini kinajitokeza miongoni mwa vijana wenzao katika maeneo ya vijijini katika nchi ambavyo havionyeshwi na vyombo vikubwa vya habari.

Baadhi ya vijana ambao hawana fursa kuzungumza katika darasa la wanafunzi 40 watakuwa na fursa ya kuzungumza kupitia vipaza sauti na kusikika kwa wengi. Redio inasaidia kuonekana na kutambulika, na inaongeza kujiamini. Katika nchi ambapo vijana ndiyo sehemu kubwa ya wakazi, ni muhimu kwa sauti zao na maoni kusikika na kujenga mustakabali wa baadaye ambao wataurithi. (END/2013)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The element 'html' is used but not declared in the DTD/Schema.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>