Inter Press Service News Agency
Tuesday, May 22, 2018   11:01 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions


Uwazi Unaweza Kuimarisha Sera za Kukabiliana na Ukame
Isolda Agazzi

GENEVA, Machi 15 (IPS) - Wanasayansi waliokusanyika mjini Geneva kwa ajili ya Mkutano wa Kwanza wa Watu Maarufu kuhusu Sera za Ukame (HMNDP) katika kipindi cha miaka zaidi ya 30 iliyopita walibainisha ukusanyaji wa takwimu na usambazaji wa taarifa kama moja ya changamoto kubwa za kuzuia ukame kikamilifu. Pia walisema kuwa na malengo sahihi na dhamira ya kisiasa yenye nguvu itakuwa muhimu katika kujenga sera katika ngazi ya kitaifa. Waliyasema haya katika mkutano ambao uliandaliwa kwa pamoja na Taasisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuzuia Kuenea kwa Jangwa (UNCC), Shirika la Chakula Duniani (FAO) na Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO), kati ya Machi 11-15 kujaribu kuanzisha mjadala wa kimataifa juu ya sera za kitaifa.

Pamoja na tofauti za wazi, hasa kati ya mataifa ya Kaskazini na Kusini lakini pia baina ya nchi na nchi, baadhi ya vikwazo vinafanana katika kanda zote, kwa kuanzia na haja ya kukuza ukusanyaji wa takwimu na usambazaji wa taarifa.

Kama ambayo Cesar Morales, mratibu wa mradi wa Tume ya Uchumi ya Amerika Kusini (ECLAC), alivyoiambia IPS pembezoni mwa mkutano huo, "Tatizo siyo ukusanyaji wa takwimu tu, lakini pia jinsi ya kusambaza takwimu hizo."

Anasema katika Amerika Kusini, lakini pia katika maeneo mengine, tatizo linazidishwa na ukweli kwamba baadhi ya taasisi zinakataa kufanya takwimu na tafiti kupatikana bure kwa vyama vya kijamii, umma na mashirika mengine.

"Kwa sasa tunaandaa ripoti kwa ajili ya serikali ya Costa Rica na shirika la hali ya hewa linatutaka kulipia takwimu hizo," alilaumu, akiongeza kuwa katika jamii ya wanasayansi, ambapo kila mmoja anashindania fedha kidogo, hakuna anayetaka kutoa taarifa kwa mwenzake.

"Huu ni mfumo wa Marekani. Kuingiza mifumo ya kisoko katika utafiti wa kisayansi ni jambo zuri lakini halitakiwi kuvuka mipaka," alisisitiza.

Katika kukabiliana na tatizo, wanasayansi wa Amerika Kusini katika mkutano huo walipendekeza kuwepo kwa sera za uwazi katika utoaji wa takwimu na kujenga mifumo ya kitaifa inayohusiana na taarifa za ukame.

Nchini Argentina, Baraza la Taifa la Sayansi na Utafiti wa Kiufundi (CONICET), chombo cha kitaifa kinachoongoza katika kukuza sayansi na teknolojia, kinahitaji utafiti unaofanyika kwa kutumia rasilimali zake kutolewa bure kwa watumiaji wote.

Wanasayansi kutoka Amerika Kusini pia walizungumzia juu ya sekta za madini, ambazo siyo tu kwamba zinatumia kwa kiasi kikubwa rasilimali za maji, na hivyo kuongeza tatizo la uhaba wa maji na ukame, lakini pia kuchangia katika kupungua kwa uungwana wa kitaifa katika kusimamia maji.

Wataalam walielezea mfumo wa sasa wa maendeleo ya misitu ambao unatumiwa na kutangazwa katika bara zima – hasa kukata misitu ya asili kwa ajili ya kilimo cha mazao ya biashara ambayo yanategemea maji kwa kiasi kikubwa kama mikaratusi kuwa kikwazo cha mikakati ya kukabiliana na ukame.

Uchimbaji wa madini ni tatizo jingine kubwa katika baadhi ya mikoa nchini Peru, Bolivia, Chile na Argentina.

"Jamii za asili za India zinaishi katika mabonde …ambako wanatumia maji ya kutosha kwa kupikia. Lakini shughuli za madini katika kanda zina lengo la kutumia maji yote kutengenezea bidhaa kwa ajili ya soko lenye thamani," Morales aliiambia IPS.

Kuondolewa kwa jamii za Wahindi katika ardhi kunachangia katika kupoteza maarifa ya jadi ya jinsi ya kusimamia uhaba wa maji na kukabiliana na madhara ya mabadiliko ya tabia nchi. Wakazi wa zamani wa Peru, kwa mfano, walikuwa wakisafirisha maji katika mifereji maalum iliyobuniwa kuzuia kupoteza maji na walikuwa na mbinu za kilimo sahihi, zinazoendana na rasilimali zilizopo.

Kwa mfano, "Mwaka huu umetangazwa kuwa mwaka wa mimea aina ya quinoa," alisema Morales. "Hivi karibuni, mmea huu ulikuwa umeshaanza kutoweka, lakini umeibuka ghafla na kuwa maarufu kutokana na kuwa na protini ya hali ya juu. Unakua karibu kila mahali na kila mmoja anataka kuulima kwani ni biashara kubwa sana nje ya nchi.

"Lakini mmea huu hauwezi kulimwa peke yake na kwa kiasi kikubwa. Unahitaji kupandwa pamoja na mimea mingine ili kulinda bioanuwai na rutuba ya udongo." Lakini wakulima wa biashara wanapendelea zaidi kilimo cha zao moja na hivyo kuwa tatizo kubwa linaloeneza ukame.

Wataalam katika mkutano wana imani kuwa njia ya kuendeleza mfumo bora zaidi wa kukusanya takwimu na kusambaza ni kuwa na mfumo wa sekta mbalimbali kushirikiana katika kukabiliana na ukame.

"Ukame ni suala la kimaendeleo, na wala siyo suala la kimazingira pekee. Kuwekeza katika kukabiliana na ukame kunaweza kuongeza pato la ndani la taifa (GDP)," Bai-Maas Taal, katibu mtendaji mkuu wa Baraza la Mawaziri wa Maji Afrika, aliiambia IPS. "Lakini tatizo ni kwamba gharama za kukabiliana na ukame ni jambo la kukadiriwa tu. Ni madhara ya awali pekee ambayo yanaangaliwa, wakati madhara ya muda mrefu kama yale ya kilimo yanaachwa."

Kwa mujibu wa wanasayansi wa Afrika, kuendeleza sera timilifu za kukabiliana na ukame hakuhitaji kila nchi kuwa na sera zake mpya.

Katika nchi ambayo ina uzoefu mkubwa wa ukame mkali –ambao umetoka katika hali ya kuwa wa bahati mbaya na kuwa wa mara kwa mara – miongo kwa miongo, kila nchi ina baadhi ya taasisi, sera, au mkakati wa kushughulika na suala hilo.

Lakini kujenga uwezo na dhamira kubwa ya kisiasa kunakosekana, kama ambavyo inajitokeza kila mahali duniani.

"Tunahitaji uratibu katika kusimamia ukame," Taal aliendelea. "Nchini Kenya, ni ofisi ya Waziri Mkuu ambayo inaratibu mikutano ya hali ya hewa – kutokana na kuwa mpango huo unatoka katika ofisi ya juu kabisa, mawaziri wote wanashiriki." Kuwa na mwongozo kutoka mamlaka za juu katika serikali pia kunawezesha usambazaji wa taarifa kwenda kwa haraka na kuwa na ufanisi.

Hii ilishuhudiwa nchini Marekani wakati wa ukame mkali wa mwaka 2011-2012, ambapo madhara yalikuwa madogo kutokana na kazi nzuri ya Mfumo wa Kitaifa wa Kutoa Taarifa za Ukame (NIDIS) ambao ulitoa taarifa za mapema.

Wakisisitiza kaulimbiu ya HMNDP – kuwa na sera kamili za ukame katika ngazi ya kitaifa - Adrian Trotman kutoka Taasisi ya Hali ya Hewa na Maji ya Caribbean, alisema, "…Sera za ukame zinafanya kuwa na shabaha ya kulenga katika malengo makuu. Wahusika wanaweza kubadilika, lakini malengo yanabakia yale yale na unaweza kuanzisha na kuendeleza ushirikiano na kuratibu hatua za utekelezaji wakati ukihakikisha kuwa sera zinakuwa rahisi kubadilika."

Miongoni mwa mipango mingi na mapendekezo yaliyopo mezani ni yale yaliyotolewa na wanasayansi wa Afrika kuanzisha mifumo ya bima kwa ajili ya wakulima kupewa fidia wakati wa ukame, na wanasayansi wengine kutoka ukanda wa Pasifiki ya Kusini kuangalia jinsi ya kuanzisha mfumo wa usalama wa ukame kusaidia wanajamii, kama ilivyo kwa Australia, nchi pekee yenye sera kamili ya ukame ya taifa ambayo imewawezesha kuondokana na ukame kama moja ya mambo ya kupewa misaada ya dharula. (END/2013)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The element 'html' is used but not declared in the DTD/Schema.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>