Inter Press Service News Agency
Monday, June 18, 2018   10:51 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions

ANGOLA
Paneli za Jua Zabadili Maji Machafu Kuwa Masafi
Louise Redvers

LUANDA, Machi 8 2012 (IPS) - Kontena lililopigwa rangi nzuri huku likiwa na paneli za jua katika paa lake na vifaa vya kuchujia maji linaonekana katika kijiji hiki cha vumbi cha Bom Jesus, kama kilomita 50 mashariki mwa mji mkuu wa Angola, Luanda.

Lakini hivi karibuni kontena hilo litatoa lita zipatazo 20,000 za maji safi ya kunywa kwa siku kwa wakazi wapatao 500 ambao kwa sasa wanategemea zaidi kupata maji kutoka katika vyanzo vya maji machafu katika mto wa karibu.

Likiwa limebuniwa na kampuni ya Canada ya Quest Water Solutions, kituo hicho cha maji ya kunywa kinaitwa "AQUAtap" kinafanyiwa majaribio duniani kote katika taifa hikli la Kusini mwa Afrika kwa mtizamo kuwa kama kitafanikiwa, teknolojia hiyo inaweza kuenezwa katika ukanda mzima.

Kwa kutumia nishati ya jua iliyofungwa katika betri kubwa, maji kutoka Mto Kwanza, kama kilomita 50 kutoka kituoni hapo, yanasafishwa kwa kutumia mchanga na chujio. Halafu UV inatumika kuchemshia maji hadi kufikia ubora wa maji ya kunywa unaotakiwa na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) tayari kwa kunywa kupitia kwneye mabomba ya chuma.

"Ni teknolojia ya moja kwa moja na rahisi," alielezea John Balanko wa Quest wakati kwa taratibu kabisa akibonyeza bomba kuruhusu maji kuingia kwenye chupa.

"Ndiyo, inaonekana tekonolojia ya zamani mahali pengine lakini hapa inaonekana ni teknolojia ya juu na ngumu, lakini sivyo ilivyo, ni rahisi sana na uzuri wake ni kuwa inahitaji ukarabati mdogo.

"Mashine yeneywe itahitaji kufanya ukarabati kila mwezi na tunatoa mafunzo kwa baadhi ya wananchi wa Angola ili waweze kuendesha teknolojia hiyo mara tu tutakaporejea Canada."

Mabomba ya chuma ambayo yanatoa maji zaidi ya lita moja kila unapobonyeza yametengenezwa kuweza kusafisha maji kiurahisi.

Balanko na mfanyakazi mwenzake Peter Miele, ambao wote wanatoka Vancouver, wana uzoefu wa kutumia teknolojia hiyo kutatua matatizo ya maji vijijini nchini Canada.

Walipokutana na mkazi wa Angola katika mkutano miaka minne iliyopita nmchini Canada, iliewafanya kuanza kuiangalia Afrika.

AQUAtap imebuniwa kwa jamii za kijijini nchini Angola ambako uhaba wa maji safi na uchache wa vyoo ni mambo yanayochangia kwa kiasi kikubwa vifo vya watto wachanga nchini humo, ambapo mtoto mmoja katika kila watoto watano hufariki kabla hajafikia miaka mitano ya kuzaliwa.

Tangu kumalizika kwa miongo mitatu ya vita mwaka 2002, serikali ya Angola imeshatumia mamilioni ya dola kwa ajii ya ukarabati wa miundombonu na kusambaza huduma za maji kwa wakati wake wapatao milioni 19.

Kama sehemu ya "Agua para Todas" mpango wa (Maji kwa Wote) maji ya bomba nay a visima yamefikishwa kwa wananchi wengi nchini kote, pamoja na kuwa kwa mujibu takwimu za serikali, nusu ya wakati bado hawana maji safi.

Kijiji kilichochaguliuwa na Quest Water Solutions, ambacho kilipendegezwa na mamlaka ya manizipaaa, kina moja ya mabomba ya serikali, lakini wakati, ambao wengi wao ni wakulima wa kujikimu na hawana ajira rasmi, waliiambia IPS mambomba hayajafanya kazi kwa zaidi ya mwaka sasa.

Carlos de Costa Gabriel, 25, a;ikaribisha mashine hiyo mpya na hajaweka siri yeyote juu ya ukweli kuwa alitaka kupata ajira kama mlinzi wa kulinda mshine hiyo wakati wa usiku kuzuia wezi wa paneli za jua.

Alisema: "Tunapenda sana mradi huu. Tumekluwa tukitumia maji ya mto, ambayo yalisababisha matattizo mengi kama vile ya kuhaara na kutapika.

"Nina watoto wa kike wawili wenye umri wa miaka mitatu na mitano hivyo nafurahia sana kwamba sasa tunaweza kusafisha maji ambayo yataondoa matatizo yetu ya kiagfya."

Mama wa watoto watano Joaquina Xavier, 38, aliongeza: "Tunafurahi sana kwa mradi huu. Kwa sasa maji tunayotumia ni machafu sana na ni kazi kubwa kutumia ndoo kuchota maji kutoka mtoni.

"Watoto wanapata magonjwa kutokana na maji haya, na baadhi ya watu katika familia yangu wamefariki kutokana na hali hii, lakini mashine hii, itakuja kusaidia."

Balanko na Miele wanafanya kazi kwa kushirikiana na Wizara ya Viwanda ya Angola, ambayo inajishughulisha na manunuzi ya vofaa kwa ajili ya mrdi wa Agua Para Todas.

Kifaa hicho, moja ya viwili ambavyo vimeingizwa nchini Angola bila gharama ya serikali, vinauzwa kwa gharama ya dola 150,000, na kuwa na grantii ya matengenezo ya miaka miwili.

"Hatuwezi kukanusha sisi ni kampuni inayotengeneza faida ambayo ina bidhaa za kuuza," Balanko alifafanua. "Lakini nadhani unahitaji kutengeneza faida ili uweze kutoa msaada.

"Hii ni gharama ya moja kwa moja kwa serikali, ambayo watailipa lakini wanakijiji watakuwa na maji safi na salama kwa angalau miaka 15 hadi 20 ijayo.

"Pia inapunguza gharama kwa muda mrefu kwasababu gharama ya maji ni dola 2.30 kwa lita 1,000, wakati kwa wakati huu watu wana;lipia dola zipatazo 30 kwa kila lita 1,000, gharama ambazo ni zaidi ya mara 10."

Maji kutoka AQUAtap yatatolewa bure kwa wanakijiji, Balanko alielezea, uamuzi ambao umechukuliwa na mamlaka.

Wakanada wanakubali kuwa kuna hatari inayojionyesha wazi kutokana na ukweli kwamba maji yatakuwa ya bure, kwamba mashine inaweza kuharibiwa, au hata kuporwa na watu ambao watatraka kuuza maji kwa faida yao wenyewe.

Lakini walisema wana matumaini kuwa kijiji wataona mradi kama wa kwao na kuzuia lolote mabalo linaweza kujitokeza. Balanko alisema: "Muda utasema, lakini ana imani kuwa mashine italindwa na kutunzwa. Tutaweka ulinzi hapa na ikiwezekana kuweka taa za mwanga mkali kuongeza usalama.

"Tumewaambia wanakijiji kuwa hii ni mahsien yao na ni lazima waitunze na tumeshirikisha baadhi ya wazee na watu wenye heshima katika jamii kusaidia kueneza ujumbe." (END/2013)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The element 'html' is used but not declared in the DTD/Schema.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>