Inter Press Service News Agency
Tuesday, June 19, 2018   19:12 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions

TANZANIA
Mabadiliko ya Tabia Nchi Yanahitaji Kubadili Mazao ya Kilimo
Marko Gideon

PANGANI, Machi 7 (IPS) - Kuendelea kwa ukame unaotokana na mabadiliko ya tabia nchi katika vijiji vya Mwembeni na Sange wilayani Pangani mkoani Tanga kumesababisha kuzidi kupungua kwa upatikanaji wa chakula na hivyo kutishia maisha ya wakazi wa vijiji hivyo. Lakini mradi wa Pwani unaofadhiliwa na shirika la USAID umeamua kuingilia kati kusaidia kunusuru maisha ya wakazi hao na vipato vyao.

Mradi huo unasaidia vijiji hivyo viwili kupanda mazao ya migomba na ufuta ambayo yanastahimili ukame na magonjwa na pia yanakomaa kwa muda mfupi. Mazao hayo yalipendekezwa na wananchi wanaoishi katika vijiji hivyo.

Kilimo cha majaribio cha ndizi zinazostahimili ukame na magonjwa na zinazokomaa vizuri kilianzishwa katika kijiji cha Mwembeni kama zao mbadala baada ya mazao ya mahindi na mpunga ambayo yalikuwa yakitegemewa katika miaka ya zamani kushindwa kuhimili ukame unaotokana na mabadiliko ya karibuni ambao umeongezeka kwa kiasi kikubwa katika miaka ya karibuni.

Kilimo cha ndizi ni sehemu ya mipango ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ambayo inaendeshwa na mradi wa Pwani, ambao pia unapata msaada wa kitaalam kutoka Kituo cha Rasilimali za Pwani cha Chuo Kikuu cha Kisiwa cha Rhode nchini Marekani.

Mipango hiyo ya mabadiliko ya tabia nchi pia inahusu tafiti mbalimbali zinazofanywa na mradi juu ya athari za mabadiliko ya tabia nchi na jinsi wananchi katika vijiji vya mwambao wa Pwani wanaweza kuepukana na athari hizo na pia kuongeza ufahamu wa watu juu ya mabadiliko ya tabia nchi.

Katika kijiji cha Sange, kilimo cha ufuta kimeanzishwa kama mradi wa majaribio kusaidia wanakijiji hao kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Wanaume kwa wanawake katika kijiji cha Mwembeni wamepanda aina mbalimbali za migomba zilizotoka katika taasisi ya utafiti wa kilimo Tengeru mkoani Arusha. Aina hizo za ndizi ambazo zimegawiwa kwa wanakijiji 10 ni pamoja na mkono wa tembo, mzuzu, Chinese Grandenine, n.k. Kwa mujibu wa afisa ugani wa Mwembeni aina hizo za ndizi zinaweza kukomaa kwa kipindi cha miezi 9 tu. Mavuno ya ndizi yanatarajiwa kuvutia wanakijiji wengine kuanza kilimo cha ndizi. Wakulima wapya watapatiwa mbegu za migomba kutoka kwa wanakijiji wenzao ambao tayari wameshafaidika na mradi huo.

Mpangilio kama huu pia utatumika katika kijiji cha Sange ambapo wanakijiji 10 walipatiwa mbegu za ufuta ambazo zinastahimili ukame na magonjwa na pia zinakomaa mapema kutoka taasisi ya kilimo ya Nariendere mkoani Mtwara. "Yunatarajia mradi huu kuwa na faida kubwa kwani mbegu zitaweza kusambaa kwa wakulima wengi katika wilaya nzima. Tutahakikisha kuwa mbegu zilizoboreshwa zinasambaa kwa kila mtu wilayani humu," alisema Mkurugenzi wa Wilaya ya Pangani, Rashid Neneka.

Wakati kilimo cha ndizi katika kijiji cha Mwembeni kinatarajiwa kupunguza hali ya usalama wa chakula kwa wakazi wa kijijini humo, kilimo bora cha ufuta kijijini Sange kinatarajiwa kuboresha upatikanaji wa chakula ikiwa ni pamoja na kuingizia wanakijiji kipato.

Bwana Mahmood Jumaa ni mkulima wa ufuta katika kijiji cha Sange ambaye pia anafaidika na mradi wa TCMP Pwani. Anasema ufuta ni miongoni mwa mazao muhimu ya kibiashara katika kijiji hicho ambapo soko lake halina shida. Anasema kwa sasa kilo moja ya ufuta inauzwa kwa Shs 1500 za Kitanzania na ana uwezo wa kuvuna hadi kilo 650 kama mvua zikiwa ni nzuri.

"Mwaka juzi nilivuna kilo 650, lakini mwaka jana nimevuna nusu yake kutokana na kupungua sana kwa mvua," anasema Jumaa’.

Kiasi hiki ni sawa na kuingiza kiasi cha zaidi ya Shs 970,000 kwa mavuno, kiasi mabacho ni kikubwa mno kwa wakazi wa kijijini ambao wengi wao wanaishi kwa chini ya dola moja kwa mwaka.

Anasema kuwa kilimo cha ufuta kimesaidia kwa kiasi kikubwa kuendesha familia yake ikiwa ni pamoja na kumudu kusomesha watoto wake.

Hata hivyo, amefurahishwa na mradi wa TCMP Pwani kuwatafutia mbegu za ufuta zilizoboreshwa hasa ambazo zinastahimili ukame kwani mvua zimekuwa zikipungua mwaka hadi mwaka na hivyo kupungua kwa uzalishaji wa zao hilo.

Picha kuhusu makala haya zinapatikana katika mtandao wa http://tcmppwani.blogspot.com/2013/03/kilimo-cha-mabadiliko-ya-tabia-nchi_8.html

(END/2013)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The element 'html' is used but not declared in the DTD/Schema.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>