Inter Press Service News Agency
Thursday, April 26, 2018   20:20 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions


Mafanikio ya Afrika Kwenye Usalama wa Chakula
Miriam Gathigah

NAIROBI, Jan 20 2012 (IPS) - Idadi kubwa ya nchi za Afrika zinapata mafanikio makubwa katika kutokomeza njaa na umaskini. Ghana, Liberia, Malawi, Rwanda, Sierra Leone na Afrika Kusini ni miongoni mwa nchi ambazo zimepata mafanikio makubwa katika kufikia malengo haya.

Hii imejionyesha katika ripoti ya utokomezaji wa njaa ambayo inapima usalama wa chakula katika Afrika na kuandaliwa na shirika la ActionAid International, amblo linafanya kazi kuhakikisha kuwa dunia inaondokana na umaskini na pia katika utafiti wa ACORD, Shirika la Ushirikiano katika Utafiti na Maendeleo.

Nchini Ghana katika kipindi cha miaka 15 iliyopita idadi ya watu waliokabiliwa na uhaba wa chakula imepungua kwa kiasi kikubwa kutoka asilimia 34 hadi asilimia nane. Mpango wa kutoa chakula mashuleni umeshawafikia watoto milioni moja, kwa mujibu wa takwimu kutoka wizara ya Kilimo ya taifa hilo la Afrika Magharibi.

Tangu kumalizika kwa vita vilivyodumu kwa muongo mmoja mwaka 2002, Sierra Leone imeongeza kwa kiasi kikubwa ardhi ya kilimo hadi kufikia hekta milioni 1.8, na hivyo kupunguza idadi ya watu wanaokumbwa na njaa kwa karibu asilimia 10, pia kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Kilimo ya nchini humo.

Kilimo, kama ilivyo katika mataifa mengi ya Afrika, ni uti wa mgongo wa uchumi wa Rwanda. Kwa mujibu wa Wizara ya Kilimo na Rasilimali za Mifugo nchini humo, sekta hiyo inazalisha asilimia 45 ya mapato yanayotokana na kuuza bidhaa nje na inachangia wastani wa asilimia 90 ya chakula chote kinachotumiwa ndani ya nchi.

George Nderi, mchambuzi wa masoko mjini Nairobi, alielezea: "Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, sekta ya kilimo nchini Rwanda imekuwa ikikua kwa wastani wa asilimia 4.5, na kuchangia wastani wa asilimia 36 ya pato la taifa, kiwango cha juu zaidi katika Afrika Mashariki."

Alisema kuwa sekta za kilimo za Kenya na Uganda zinachangia wastani wa asilimia 24 katika pato la taifa, huku nchini Tanzania ikichangia asilimia 25.

Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, uchumi wa Rwanda unakua katika kiwango kizuri cha asilimia 7.8, angalau nafasi mbili mbele ya kiwango cha Jumuiya ya Afrika Mashariki.

"Ni muhimu kugundua kuwa baadhi ya nchi zenye ukame mkubwa pia zimepunguza idadi ya watu wanaokabiliwa na njaa. Nchini Ethiopia, kwa mfano, mwaka jana idadi ya watu wanaokabiliwa na njaa ilipungua kutoka milioni 5.2 hadi milioni 3.2, na hivyo kupunguza lishe duni kwa asilimia 32 nchini humo," Nderi alisema.

Kwa mujibu wa Utafiti wa Afya na Idadi ya Watu nchini Ethiopia mwaka 2011, vifo vya watoto chini ya miaka mitano vinasimamia katika asilimia 20 mwaka 1990 lakini vimeshuka hadi asilimia 8.8. Lishe duni inachangia kwa uchache nusu ya vifo hivi kwa mujibu wa Shirika la Afya Ulimwenguni.

Amos Kiptanui, mkulima mdogo katika Jimbo la Bonde la Ufa nchini Kenya, ambalo pia linajulikana kwa kuzalisha chakula nchini, alisema kuwa hatua hizi chanya zimetokana na dhamira za kifedha na kisiasa katika kutokomeza njaa na lishe duni.

"Rwanda ni nchi ya kwanza barani Afrika kusaini Mpango Kabambe wa Maendeleo ya Kilimo Afrika (CAADP). Nchi hiyo pia imeongeza mara mbili matumizi yake katika kilimo hadi asilimia 10 kufikia mkakati wa kisera wa CAADP," alisema.

CAADP inahitaji nchi zilizotia saini mkataba huo kutenga kwa uchache asilimia 10 ya bajeti zao za kitaifa katika kilimo.

"Mataifa ya Afrika ambayo yamepata mafanikio kuweza kulisha watu wake yamefanikiwa kutokana na kuwekeza zaidi katika wakulima wadogo wadogo ambao ni zaidi ya asilimia 90 ya uzalishaji wa kilimo barani Afrika," Nancy Mumbi, mtafiti wa kilimo na afisa ugani nchini Kenya katika Jimbo la Kati, alisema.

Aliongeza kuwa mwaka 2011, serikali ya Rwanda iliwekeza dola milioni tano za nyongeza katika sekta ya kilimo.

"Kutokana na bajeti ya kilimo kufikia dola milioni 112, rasilimali hizi zinaendelea kusaidia wakulima nchini Rwanda kwa njia ya kutoa ruzuku za pembejeo kama vile mbolea za chumvi na kutoa mafunzo juu ya teknolojia za kisasa ambazo zinaweza kuboresha uzalishaji. Kwa uhakika, kumekuwepo na programu ya serikali ya kukuza matumizi ya kilimo," Numbi alisema.

Nchi nyingine ambazo zimeboresha mgawo wao wa kibajeti katikia kilimo ni pamoja na Sierra Leone, Kenya na Malawi.

Tangu mwaka 2005, Malawi imejitahidi kutenga kwa uchache asilimia 10 ya bajeti yake ya kitaifa katika kilimo. Bajeti ya kilimo nchini Kenya imeongezeka kwa kasi kutoka asilimia nne katika mwaka wa fedha uliopita hadi asilimia tisa katika mwaka wa fedha wa sasa. Iko nyuma ya asilimia moja tu kufikia mkakati wa kisera wa CAADP.

Usalama wa chakula nchini Ghana umechangiwa na uwekezaji wa muda mrefu wa nchi hiyo katika kilimo.

"Kama ilivyo kwa Rwanda, kuna mradi wa kutoa ruzuku ya mbolea nchini Ghana ambao unawezesha wakulima kuhifadhi ardhi iliyochoka kutokana na usimamiaji mbovu," Mumbi alisema.

"Nchi ambazo zimeboresha usalama wa chakula ni zile ambazo zimelinda ardhi zao zisiharibike kutokana na sababu mbalimbali kama vile matumizi ya kupitiliza ya mbolea za kemikali, uchomaji wa moto, ukataji wa miti na ufugaji wa kupita kiasi."

Nchini Kenya, uharibifu wa Msitu wa Mau ulisababisha mabadiliko makubwa ya hali ya hewa yaliyosababisha kupungua kwa mvua, ambayo iliathiri kilimo katika Jimbo la Bonde la Ufa na hivyo kusababisha uhaba wa chakula.

Msitu wa Mau unaongoza kwa kunyonya hewa ya ukaa nchini humo na pia ni hifadhi kubwa ya vyanzo vya maji. Msitu huo pia unahusika katika kuzuia mafuriko na kupunguza mmomonyoko wa udongo. Taifa hilo limejikita katika kampeni kubwa ya kurejesha msitu huo na kuufanya kuwa na faida zaidi ambazo zitaboresha upatikanaji wa chakula katika ukanda huo.

Senegal imekuwa ikifanya kazi katika mpango kabambe wa kujitosheleza kwa chakula ifikapo mwaka 2015. Taifa hilo linawapatia wakulima ruzuku za mbegu na pembejeo za mbolea. Pia linaendesha mpango wa usalama wa chakula na lishe bora kwa watoto wa chini ya miaka mitano, na akina mama wajawazito na wanaonyonyesha.

Nchi nyingine zinazofanya jitihada zinazoonekana waziwazi katika kuboresha usalama wa chakula ni pamoja na Algeria Morocco, Misri, Tunisia, Botswana na Gabon.

Pamoja na kuwa nchi nyingi zinaweza kupambana na njaa na zipo katika mwelekeo mzuri, bado kuna jitihada kubwa zinazohitajika kuchukuliwa kama ambavyo Ousainou Ngum, mkurugenzi mtendaji wa ACORD anavyosema.

"Ni lazima mataifa ya Kiafrika yajipange katika sera zake za uwekezaji ili kuelekeza nguvu katika kilimo na uzalishaji wa chakula. Mgogoro wa chakula unaolikabili bara hilo unatokana na kukosekana kwa sera madhubuti. Kama viongozi watashindwa kuratibu sera zao vema, mamilioni ya Waafrika wataendelea kukabiliwa na njaa kutokana na uhaba wa chakula.

"Ni lazima viongozi wetu kujenga vitega uchumi ambavyo vinafaa kwa sekta ya kilimo, huku vikilenga katika wakulima wadogo, wanawake na wafugaji. Kwa uchache Waafrika milioni 270 kati ya wakazi wote barani humo wapatao milioni 800 walikuwa wakikabiliwa na njaa. Ili kukabiliana na hali hii, mikakati ya kuongeza uzalishaji wa chakula katika bara lazima kuangalia zaidi suala la usalama katika umilikaji wa ardhi na upatikanaji bora wa masoko." (END/2013)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The element 'html' is used but not declared in the DTD/Schema.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>