Inter Press Service News Agency
Sunday, September 22, 2019   19:38 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions


TANZANIA - Watoaji Huduma za Uzazi wa Mpango wa Kujitolea Wawafikia Wananchi wa Vijijini
Na Marko Gideon

PANGANI, FEB 4 (IPS) - Hashim Ali Said ni mtoaji wa huduma za uzazi wa mpango katika jamii (CBD) ambaye ana dhamira ya kweli ya kusaidia jamii yake katika kijiji cha Mkalamo na vijiji vingine vya jirani. "Kuna wakati wanajamii wanakuja kunigongea mlango hata saa sita za usiku kutaka niwapatie kondomu kwa ajili ya kupanga uzazi na kujilinda na magonjwa ya kujamiiana," anasema Said mwenye umri wa mika 42.

Said, baba wa mtoto mmoja wa kike anasema alianza kueneza elimu ya idadi ya watu, afya na mazingira (PHE) katika jamii yake baada ya kupata elimu ya jinsi ya kuunganisha dhana ya uzazi wa mpango na hifadhi ya mazingira mwaka 2009 kutoka mradi wa BALANCED ambao unatekeleza miradi inayojikita katika suala zima la uzazi wa mpango ili kuchangia shughuli za hifadhi ya mazingira zinazoendeshwa na Kituo cha Rasilimali za Pwani (CRC) na Mradi wa Pwani wa Mpango wa Kusimamia Mazingira ya Bahari na Pwani (TCMP-Pwani) ambao unafadhiliwa na USAID.

Anasema kwa sasa emeelimisha familia nyingi katika jamii yake umuhimu wa uzazi wa mpango, kujiunga na vikundi vya kuweka na kukopa (SACCOs) na kutumia majiko banifu.

"Nina mifano mingi ya wanafamilia katika jamii yangu ambao hawakuwa wakijali suala la kuachanisha umri kati ya mtoto na mtoto, lakini kwa sasa wanajali kuzaa watoto wao kwa nafasi nzuri," anasema.

Said na CBDs wengine katika vijiji kadhaa vinavyozunguka Mbuga ya Wanyama ya Saadani katika mwambao wa Bahari ya Hindi wilayani Pangani wamepata heshima kubwa kutoka kwa jamii zao kutokana na kazi yao. Wamepewa majina kama ya watoaji wa huduma za afya, wakombozi, wafanyakazi wa afya na hata kuitwa madaktari.

"Watu wanatuheshimu kwasababu wakati wote tupo kwa ajili ya kuwahudumia. Wanatambua kuwa hata kama wakija kwetu saa sita za usiku tutawapatia huduma," Said alisema.

Watoaji wa huduma za uzazi wa mpango katika vijiji vingine walizungumzia umuhimu wa kuwa na CBDs katika jamii zao. Wanasema watu wanapendelea huduma zao kutokana na kwamba wako karibu nao, huduma hizo zinapatikana wakati wowote wanapozihitaji na zimeweza kupunguza umbali na haja ya kusafiri mara kwa mara kwenda kwenye vituo vya afya vilivyo karibu kwa ajili ya kupata huduma hizo na pia huduma za CBDs zinatolewa bure.

Mmoja wa wamiliki wa maduka yanayouza kondomu katika kijiji cha Mkalamo anasema idadi ya watu wanaokwenda kununua kondomu dukani kwake imepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na huduma za CBDs kuwa za bure.

Hata kama wanaweza wasijue mchango mkubwa wanaoutoa katika kusaidia kuokoa maisha ya akina mama na watoto wa kike na wa kiume kitaifa na hata kimataifa, jitihada za CBDs zinaonekana kutambuliwa na ripoti ya Shirika la Idadi ya Watu la Umoja wa Mataifa (UNFPA) inayojulikana kama "State of the World Population Report 2012 "By Choice, Not by Chance: Family Planning, Human Rights and Development" .

"Kufanya huduma za uzazi wa mpango zipatikane kwa kila mtu katika nchi zinazoendelea kunapunguza gharama za huduma za afya ya uzazi na watoto wachanga," inasema ripoti hiyo. "Uzazi wa mpango una faida kubwa kwa wanawake, familia na jamii kwa ujumla. Kwa kumwezesha mtu kuchagua idadi ya watoto anaotaka na kutoa nafasi ya kutosha kati ya mtoto na mtoto, uzazi wa mpango umewawezesha wanawake na watoto wao kuishi maisha marefu na yenye afya."

Said anasema elimu ya idadi ya watu, afya na mazingira imemweza kumshawishi yeye mwenyewe kununua jiko banifu kwa ajili ya kupunguza matumizi ya kuni katika familia yake ambayo ni chanzo cha kuangamiza misitu na kuharibu mazingira nchini. "Katika siku za zamani nilikuwa natumia jiko la mafiga matatu ambalo lilitumia kuni nyingi na kutoa moshi mwingi. Moshi ulinifanya kununua sufuria kila siku kwani zilichakaa mapema kutokana na moshi mwingi," anasema. "Moshi pia ulihatarisha afya ya familia kwani uliongeza uwezekano wa kupata magonjwa ya kupumua". Jiko la mafiga matatu alilokuwa akitumia katika familia yake lilitumia takribani vipande 8 vya kuni kwa kupikia kwa wakati mmoja wakati jiko banifu analotumia sasa hutumia vipande 2 tu vya kuni.

"Mke wangu alikuwa akilalamika kila siku kutokana na kwenda porini kukusanya kuni mara kwa mara, lakini sasa amepunguziwa mzigo wa kwenda porini mara kwa mara," anasema. "Mke wangu anasema jiko hilo pia limempunguzia muda alioutumia kuchochea kuni jikoni."

Said anasema amepata ombi maalum kutoka kwa mke wake kutengeneza jiko jingine kwa ajili ya kutumiwa na wapangaji katika nyumba yao.

Dhamira ya kweli ya kusaidia jamii yake imeivutia zahanati ya Mkalamo kumchagua kuwa dereva wa piki piki ya kubebea wagonjwa ya magurudumu matatu.

"Moyo wangu wa kujitolea umefanya kituo cha afya kunichagua kujiunga kwenye kampeni ya kudhibiti ugonjwa wa malaria na kupata zawadi ya baiskeli kutoka Wizara ya Afya. Mara tu baada ya kampeni, nilichaguliwa kuwa dereva wa pikipiki ya kubebea wagonjwa ya magurudumu matatu," anasema. Kuwa dereva wa pikipiki ya kubebea wagonjwa ni kazi nyingine ya kujitolea anayoifanya Said kusaidia jamii yake. "Nimekuwa nikiendesha pikipiki hii tangu Septemba 2012 bila kupata motisha wowote. Naamka wakati wowote ninapopata taarifa ya kuwepo kwa dharula ya mgonjwa kijijini na kijiji cha jirani cha Mbulizaga ili kumuwahisha katika zahanati yetu. Namshukuru Mungu kwa kunifanya kuwa na moyo wa kujitolea," anasema.

Mbali na majukumu ya kueneza huduma na elimu ya idadi ya watu, afya na mazingira, Said ni mfano tosha wa wanaume wanaojali uzazi wa mpango katika jamii yake. "Nina mtoto mmoja tu ambaye ana miaka minne. Kama Mungu akipenda nikapata mtoto mwingine sasa, nafasi ya kutoka mtoto mmoja hadi mwingine itakuwa kubwa na iliyopangiliwa vizuri. Na, katika mipango yangu siwezi kuwa na watoto zaidi ya 4," anasema.

Said pia ni mfano wa kuigwa kwa wanaume wengi katika maeneo ya vijijini na mijini nchini Tanzania ambao bado wanadhani jukumu la kupanga uzazi ni la wanawake pekee. Wanawake na wanaume wana jukumu la kupanga uzazi, kulinda afya za familia na kutunza mazingira na maliasili kwa ajili ya vizazi vya sasa na vijavyo. (END/2013)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The download of the specified resource has failed.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>