Inter Press Service News Agency
Wednesday, April 25, 2018   07:52 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions


Wakazi wa Makazi Duni Wasema "Hapana " kwa Fedha za Damu - Slum Dwellers Say "No" to Blood Money
Miriam Gathigah

NAIROBI, Jan 10 (IPS) - Huku ikiwa imebakia miezi miwili kabla Wakenya hawajapiga kura kwa kile kinachoonekana kama uchaguzi wenye ushindani mkubwa na uliogawanyika sana katika historia ya nchi, wengi wanahofia kuwa taifa hili la Afrika Mashariki lenye wakazi wanaozidi milioni 40 hawajaona kumalizika kwa ghasia za uchaguzi. Hii inajitokeza pamoja na kwamba wanasiasa wawili maarufu - Uhuru Kenyatta na William Ruto - bado wanasubiri hatma yao katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC) wakikabiliwa na uhalifu dhidi ya ubinadamu wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi mwaka 2007-2008.

Vurugu za baada ya uchaguzi, ambazo zilisadikika kusababishwa na kuhamasishwa na vyama hivi viwili vya kisiasa, ziliacha maelfu ya watu kufariki dunia, zaidi ya 3,000 kujeruhiwa na mamia kwa maelfu kuyahama makazi yao.

"Hata hivyo, bado wanasiasa wasiokuwa wastaarabu wanaendelea kueneza ushawishi wao katika makazi duni nchini kote Kenya. Hapa (katika makazi duni), kwa kiasi cha dola moja au mbili, na hata chini ya hapo, watu wanaweza kutishiwa, kujeruhiwa au hata kuuawa kwa wale wanaoonekana kuwa wapinzani wa kisiasa," Peter Muga, mchambuzi wa kisiasa aliyepo mjini Nairobi, aliiambia IPS.

Uhaba wa ajira na umaskini umeacha mamilioni ya wapiga kura katika makazi mbalimbali duni kushawishiwa na wanasiasa ambao hawana hofu kuhusu kuchukua hatua kali kunyamazisha wapinzani.

"Lakini kutokana na wanasiasa hao kukosa nguvu za kukabiliana na wapinzani katika boksi la kura, wanawapatia pesa vijana katika makazi duni kufanya mambo yao mabaya," Muga aliongeza.

Kampeni ya kusema "hapana"

Katika jitihada za kuzuia madhara mabaya zaidi yanayohusiana na rushwa ya uchaguzi na ghasia zilizochochewa na uchaguzi wa mwaka 2007-2008, wakazi wa makazi duni ya Mathare - makazi makubwa zaidi mjini Nairobi ambayo yana wakazi 500,000 - wamenzisha harakati zenye jina la 'Tia Rwabe Zi' (Sema Hapana kwa shilingi za Kenya 200).

"Wanasiasa wanatupatia ksh 200 (kama vile dola mbili) kupambana na wale ambao hawawaungi mkono," Julia Njoki, mwanachama mwanzilishi wa Tia Rwabe Zi, aliiambia IPS.

"Mara nyingi, wagombea wanaoisigishana wanatoka makabila tofauti. Uadui huu mara nyingi unageuka kuwa ukabila. Wakati tukiongea, Mathare tayari imeshagawanyika, kuna baadhi ya makabila ambayo hayawezi kuishi au kugombea nafasi za kisiasa katika baadhi ya maeneo," aliongeza.

Kwa mujibu wa Njoki, harakati hizi zilitokana na kifo na uharibifu ulioshuhudiwa wakati wa mgogoro wa baada ya uchaguzi wa mwaka 2007-2008, ambao ulichochewa na wakazi wa makazi duni.

"Katika harakati hizi tunasema hapana kwa hongo za uchaguzi. Wengi wetu sisi ni vijana, ambao ni watoto wa kiume na watoto wa kike na wanawake. Pia tumewafikia wengine katika makazi mengine duni kama vile Kibera," alisema, akimaanisha makazi duni makubwa zaidi mjini Nairobi, moja ya makazi duni makubwa kabisa barani Afrika.

Umaskini unaendesha vyama vya siasa.

Lakini kampeni hiyo imechukua mwelekeo utakaokuwa na kazi kubwa na haitaweza kuwa na ushindi wa kiurahisi.

Hata kumbukumbu za umwagaji damu za mwaka 2007-2008 hazitazuia wananchi wa Kenya maskini kufanya kile ambacho wanaweza kufanya kupunguza mzigo wa mazingira duni wanayoishi.

Wakati wakazi wa makazi duni ya Kibera walianzisha mfumo wa 'vyoo vya kurusha', Wakenya wengi wenye makazi yenye hadhi na vyoo bora waliwacheka wenzao.

Lakini kwa wakazi wa makazi duni wenyewe, kulazimishwa kujisaidia katika mifuko ya plastiki na kutupa uchafu hewani kutokana na kukosa vyoo na maeneo ya kutupia taka siyo jambo la kuchekelea. Wala jambo la kukojoa kwenye makontena ya plastiki halifai kuchekelea.

Wakati wakazi mbalimbali wameweza kuchukua hatua kukabiliana na mustakabali wa wakazi wa makazi duni wasiokuwa na vyoo, siyo mambo mengi ambayo yamebadilika.

Wakati wa usiku, vyoo vya jadi vinakuwa eneo ambalo halifai kufika kutokana na kukosekana kwa usalama. Matokeo yake, wakazi wengi wanaamka na kujisaidia kwenye mifuko ya plastiki katika umbali mdogo kutoka milangoni mwao, na kutokuonekana kwa majirani zao tu kutokana na giza.

"Bado watu wanatumia vyoo vya kurusha kwasababu kutumia vyoo vya umma siyo bure. Fedha zinakwenda kwenye ukarabati," Veronica Wamaitha, mkazi wa Kibera, aliiambia IPS.

Katika siku nzuri, watu wanaoishi katika makazi duni wanaingiza dola mbili hadi tatu, lakini mara nyingi wanaweza kukaa wiki nzima bila kuingiza hata senti moja.

"Lakini bado watu wanapaswa kula," Rob Wangai, mkazi wa makazi duni ya Mathare, aliiambia IPS. "Hakuna kitu ambacho ni cha bure. Hata tumeamua kutumia umeme ambao umeunganishwa kinyume cha sheria; matokeo yake, ni mara chache sana tunamaliza wiki bila kuzuka kwa moto mahali fulani."

Kutokana na hali hii ya watu wanaoishi katika mazingira machafu, wanasiasa wamepata majibu ya matatizo yao.

"Wakazi wa Kenya wamegawanyika sana katika maeneo makuu mawili, wale wanaoishi katika mstari wa umaskini na tabaka la kati. Tabaka la kati kwa kiasi lina elimu na wanaelewa dhana ya kujitegemea - hali hiyo haipo kwa maskini," Ken Ochiel, mchambuzi wa kisiasa mjini Nairobi, aliiambia IPS.

Alisema wale wanaoishi katika umaskini bado wana imani kuwa viongozi wa kisiasa wanabeba ufunguo wa maisha mazuri ya baadaye.

"Huu ni ugonjwa ambao unakula jamii yetu. Viongozi ambao wana pesa na wanaweza kutoa rushwa kwa wapiga kura wanachaguliwa kiurahisi. Lakini kwa uhakika, hawaboreshi hali ya maisha ya maskini ambao wanawapigia kura," alielezea Vesca Kangongo, ambaye anagombea ugavana katika Mkoa wa Bonde la Ufa.

Maoni yake yanaungwa mkono na mwanamke pekee anayegombea urais, Mheshimiwa Martha Karua, ambaye alisema, "Ni kwa nini kaka zangu ambao wanagombea uongozi wa juu nchini wana pesa nyingi, baadhi zimeibwa kutoka katika hazina za umma. Nawataka Wakenya kupigia kura viongozi wanaoangalia masuala ambao wanaweza kuboresha hali ya maisha katika nchi hii."

Karua pia amedai kuwa wanasiasa wako nyuma ya mawimbi ya hivi karibuni ya ghasia na mauji katika makazi duni ya Mathare, ambayo yaliibua kumbukumbu za machafuko ya mwaka 2007-2008 ambapo Mathare, Kibera na makazi mengi ya mjini yalibadilika kuwa maeneo ya mauaji na uharibifu wakati makabila yalipoanza kupigana.

"Katika kila uchaguzi mkuu, wanasiasa wanapeleka askari wao wa miguu katika makazi duni, kutokana na kuwa tabaka la kati haliwezi kukubali dola mbili kutishia watu, na hata kuua," kwa mujibu wa Muga, wakati maskini wanakuwa rahisi kuathirika na rushwa.

Ochiel anakubaliana. "Wanasiasa wanatambua kuwa tabaka la kati ni gumu kulishawishi kwa ahadi, ikilinganishwa na watu ambao unaweza kuwaendesha kwa mlo mmoja kwa siku. Makazi duni pia yanakaliwa na watu wanaofanana tabaka lao ambao ni rahisi kuwapata."

Hata hivyo, wanakampeni ya Tia Rwabe Zi wana nia ya kuleta mabadiliko mwaka huu.

Kundi hilo linafanya mikutano ya mara kwa mara na kuzungumza kwa nguvu dhidi ya ghasia na kukaa bila kazi. "Tunahamasisha kila mmoja kupata ajira na hata kumtaarifu mwingine kama kuna nafasi ya ajira. Lazima watu wawe na kazi za kufanya ili kuondokana na taabu," Njoki alielezea.

Wakati wakikubaliana kuwa kutarajia watu kukataa hongo huku wakiwa katika umaskini mkubwa na njaa ni jambo ambalo ni gumu - na mabadiliko hayo hayatakuja mara moja - alisisitiza kuwa wanachama wa kampeni hiyo wanashawishiwa kuwa jitihada zao ni hatua katika mwelekeo sahihi.

(END/2013)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The element 'html' is used but not declared in the DTD/Schema.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>