Inter Press Service News Agency
Thursday, June 21, 2018   09:48 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions


Dawa ya Morphine Inaondoa Maumivu Lakini Bei Inaua Wagonjwa
Busani Bafana

BULAWAYO, Januari 23, 2013 (IPS) - Iliwachukua mabinti wa Gily Ncube wiki mbili kuuza kuku wa kutosha kupata dola 18 zinazohitajika kununulia vidonge vya dawa aina ya morphine ambavyo mama yao anakunywa kila baada ya masaa manne. Katika nchi ambapo ukosefu wa ajira unakadiriwa kuwa asilimia 70, dola 18 kwa kichupa cha vidonge 60 vya uzito wa miligramu 10 kila kimoja ni bei kubwa sana kulipia, ikiwa sawa na bei ya mikate 18.

Lakini familia ndogo ya kijijini haikuwa na chaguo – dawa ya morphine ni dawa pekee ambayo inapunguza maumivu kwa Ncube ili aweze kulala wakati wa usiku.

Ncube anaugua kansa ya mfuko wa uzazi na ipo katika hatua ya nne na kwa sasa yuko taabani kitandani. Hata kwa kupata tiba zaidi, bado anahitaji dawa za maumivu kutokana na hali yake hiyo.

Dawa ya morphine, inampatia Ncube na wagonjwa wengine kama yeye nafuu kiasi. Dozi ya siku ya miligramu 40 inamuwezesha Ncube kukaa, na hata kufanya baadhi ya kazi kuzunguka nyumba yake.

Lakini kutokana na bei ya sasa,ni watu wachache mno wana uwezo wa kununua dawa hiyo, au kuipata inapohitajika.

Maumivu yanajionyesha wazi usoni mwa Ncube wakati akielezea habari yake: kwa miezi sita sasa amekuwa akisubiri orodha ya kufanyiwa vipimo vya mionzi katika Hospitali ya Mpilo mjini Bulawayo, mji wa pili kwa ukubwa nchini Zimbabwe, uliopo kama kilomita 430 kusini magharibi mwa mji mkuu wa Harare.

Mashine ya mionzi imeharibika kwa muda mrefu sasa na mashine mpya bado inafungwa.

"Maumivu ni makali sana," Ncube aliiambia IPS akiwa nyumbani kwake, huku akielekeza kidole kwenye chupa nyeupe ya plastiki yenye dawa aina ya paracetamol, ili kupunguza maumivu, aliongeza. "Ni dawa hizi tu ndizo ambazo naweza kupata kutoka hospitalini."

Kati ya wagonjwa wapatao 7,000 wa kansa nchini, Ncube ni mmoja kati ya watu wenye bahati – anapata msaada, na mara nyingine usambazaji wa morphine, kutoka Hospitali ya Kisiwa cha Bulawayo ambayo imekuwa ikifanya kazi tangu mwaka 1982.

Wakuu wa hospitali hiyo waliiambia IPS kuwa mfumo wa afya haujitoshelezi kabisa na wagonjwa wengi wamefariki dunia wakisubiri kumuona mtaalam wa kansa, mara nyingi kutokana na kuugulia maumivu makali kabla ya kupatiwa dawa ya morphine.

Sister Adelaide Nyathi, ambaye anafanya kazi katika Hospitali ya Kisiwa cha Bulawayo, ana zaidi ya wagonjwa 90 wa kansa chini ya uangalizi wake. Anawazungukia kila wiki, akiwapatia dawa za kutuliza maumivu na kiasi kidogo cha chakula anapoweza kufanya hivyo, lakini wengi wanatabasamu, wanakumbatiana na wana matumaini.

Nyathi alisema hudumu za hospitali hiyo zinategemea zaidi kusambaza dawa aina ya morphine ili kuwapatia ahueni baadhi ya wagonjwa.

"Wagonjwa wetu wengi wapo katika hatua mbaya ya kansa ambapo madawa mengine hayaleti ahueni yoyote ya maumivu ya kansa," Nyathi aliiambia IPS. "Wagonjwa wameniambia kuwa wamezoea maumivu lakini siyo rahisi."

Pamoja na kuwa serikali ya Zimbabwe imekadiria kuwa wagonjwa wa kansa wapatao 7,000 wapo nchini humo, watoaji huduma wanasema idadi halisi ya wagonjwa inaweza kuwa ya juu zaidi, kwani wagonjwa wengi wanafariki kabla ya kutambuliwa.

Huduma ni chache mno, na kwa sasa moja ya chaguo lililobaki kwa watu maskini – ni Hospitali ya Kisiwa cha Bulawayo, moja ya hospitali za zamani zaidi nchini Zimbabwe – ambayo iko katika hatari ya kufungwa kutokana na gharama kubwa za uendeshaji na misaada michache ya wafadhili.

Hospitali hiyo ina manesi watano tu ambao wanatunza wagonjwa wa kansa wapatao 200 kutoka katika jiji zima, ambao wanawatembelea kila wiki. Wakati wana uwezo wa kuleta ahueni, hawawezi kuokoa kila mgonjwa mwenye mahitaji makubwa.

Sekesai Dziva aligundulika akiwa na kansa ya koo mwaka 2010 na alipitia katika taabu kubwa. Watoto wake wa kiume walifanya kazi kubwa kutafuta dola 84 za kununulia dawa aina ya chemotherapy ambayo ilimsadia kidogo sana.

Lakini mara nyingi fedha zinakosekana na wakati kama huo aliugulia maumivu kwa siku kadhaa. Alifariki miezi sita baadaye, huku akiacha watoto watatu wenye umri wa kati.

Pamoja na kuwa vidonge vya morphine na sindano vinatengenezwa nchini Zimbabwe, gharama bado zinasumbua wengi, hali ambayo mmoja wa wataalam wa afya wana imani kuwa inaweza kusahihishwa kwa kutumia morphine ya maji, ambayo imetengenezwa kutokana na unga wa morphine, na wafanyakazi wa maduka ya dawa na hata manesi wanaweza kufundishwa jinsi ya kuiandaa na kutengenezwa katika taasisi za afya za nchini humo.

"Tunatambau wagonjwa wengi hawawezi kununua dawa aina ya morphine ya vidonge kwasababu dola 18 ni pesa nyingi," Mkuu wa Huduma za Hopsitali ya Kisiwa cha Harare, Dk. Dickson Chifamba, aliiambia IPS. "Dola 18 zinaweza kufikia dola 54 kwa mwezi, hata kwa mtu anayetumia dozi ndogo ya kidonge cha miligramu 10 kwa kila masaa manne."

"Morphine ya maji ni chaguo bora kama wafanyakazi wa afya watapatiwa mafunzo katika kuandaa dawa hiyo kutoka kwenye morphine ya unga," Chifamba alisema. "Wataalam wa madawa wanaweza kufanya hivyo lakini mara nyingi wanalaumu kuwa inatumia muda mrefu."

Kwa sasa kuna jitihada za kushirikisha washirika wa ndani na nje kusaidia kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa afya, hasa wataalam wadogo wadogo wa madawa katika taaasisi za ndani, kutengeneza morphine ya maji.

"Dawa ya maji itafanya tiba kuwa nafuu; pia ina nafuu katika usambazaji wake kupitia hospitali za serikali," aliongeza.

Kwa mujibu wa Mamlaka ya Kudhibiti Madawa ya Zimbabwe (MCAZ), hospitali na famasi zinaruhusiwa kuhifadhi unga wa morphine kutengenezea dawa ya maji, ambayo ni nafuu na inafaa kwa wagonjwa ambao wana maumivu sana kuweza kutumia vidonge.

Kwa kushirikiana na Bodi ya Kimataifa ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya (INCB), MCAZ inaandaa na kuchambua takwimu za kimataifa za kutumia madawa ili kuyasambaza kwa wingi nchini Zimbabwe kila mwaka.

Mwaka jana, kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa MCAZ Gugu Mahlangu, Zimbabwe ilitumia jumla ya kilo 3.6 za morphine pamoja na kutengewa kilo 11.25 kwa mwaka 2012.

Mahlangu aliongeza kuwa matumizi ya dawa za kupunguza maumivu kama morphine ni mdogo sana barani Afrika, ukiondoa Afrika Kusini,ikilinganishwa na maeneo mengine ya dunia.

"Pengine mitizamo ya madaktari katika usimamiaji wa madawa inahitaji kubadilika," alisema.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO), watu wapatao milioni 4.8 wenye maumivu makali ya kansa hawapati tiba kila mwaka. INCB ilibainisha kuwa nchi zilizoendelea zinatumia karibu asilimia 80 ya dawa aina ya morphine, huku nchi katika dunia inayoendelea wakitumia asilimia inayobaki.

(END/2013)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The element 'html' is used but not declared in the DTD/Schema.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>