Inter Press Service News Agency
Monday, May 21, 2018   07:58 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions

Maswali na Majibu
Zana Nyingine ya Kupambana na Tohara Duniani
Julia Kallas

UMOJA WA MATAIFA, Januari 23, 2013 (IPS) - Kwa wastani wa watoto wa kike na wanawake milioni 140 wanaoishi wakiwa wamefanyiwa tohara (FGM), inaonekana ni kuchelewa kuchukua hatua. Lakini tangu dunia ipige marufuku FGM mwishoni mwa mwaka jana, wanaharakati wana matumaini kuwa wengi wa watoto wa kike na wanawake wataepukana na kitendo hiki cha kinyama.

Alvilda Jablonko, mratibu wa Mpango wa kupambana na FGM unaojulikana kama "No Peace Without Justice", amekuwa akipambana kupigwa marufuku kwa kitendo hicho na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa tangu mwaka 2010. Hatimaye azimio hilo lilipitishwa Desemba 20, 2012.

‘‘Kwa hiyo ni ukurasa mpya, ni zana mpya," aliiambia IPS. "(Lakini) zana inaweza kuwa na ufanisi tu kama itatumiwa vizuri."

Mwandishi wa habari wa IPS Julia Kallas alizungumza na Jablonko kuhusu jinsi gani marufuku hayo yatakuwa na matokeo mazuri. Sehemu ya mahojiano yao inafuata.

Swali: Ni nini vikwazo vikubwa ulivyopitia wakati wa kutetea azimio la kupiga marufuku FGM duniani kote?

Jibu: Nadhani kupitishwa kwa azimio na Umoja wa Mataifa ni jitihada halisi za mataifa ambayo yanapambana na suala hilo. Kwa hiyo Burkina Faso ni miongoni mwa nchi ambazo zimekuwa zikiongoza katika ngazi ya kitaifa kupambana na FGM na imeweza kuchukua uongozi katika suala hili.

Walifanya kazi kwa karibu sana na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali (NGOs) na hata muungano wa NGOs. Kimsingi walifanya kazi kuhamasisha kuchukuliwa hatua katika ngazi za kitaifa.

Swali: Jukumu kubwa la "No Peace Without Justice" katika harakati hizi ni lipi?

Jibu: "No Peace Without Justice" imekuwa ikifanya kazi kwa miaka 10 iliyopita juu ya suala hili. Ni shirika ambalo lilianzishwa na Emma Bonino, ambaye alikuwa kamishina wa zamani wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia masuala ya kiutu na ambaye kwa sasa ni makamu wa rais wa Baraza la Seneti nchini Italia. Amekuwa katika mstari wa mbele kupigania haki za wanawakw duniani kote.

"No Peace Without Justice" ilijiunga na idadi kadhaa ya mashirika, mashirika mengi yakitoka barani Afrika, ambayo tayari yalishashiriki katika mapambano dhidi ya FGM kwa miongo. Hivyo ambacho "No Peace Without Justice" imekikifanya kwa kushirikiana na wanaharakati wengi ni kushinikiza serikali kubeba jukumu na wala siyo kuachia kazi zote kufanyw ana wanaharakati.

Swali: Hatua inayofuata ni ipi?

Jibu: Kutokana na kwamba azimio limepitishwa sasa hatua inayofuata ni kuhakikisha linatekelezwa katika nchi husika. Mataifa mengi tayari yamepiga hatua, lakini kuna haja ya kuwa na hatua zinazofanana katika ngazi ya kikanda.

Katika mataifa yanayopakana, ambako kuna sheria katika taifa moja na kukosekana kwa sheria katika taifa jingine, watu wanavuka mipaka ili wakafanyie watoto wa kike kitendo hicho cha kinyama katika mataifa yasiyokuwa na sheria.

Hivyo kuna matarajio kuwa hatua hii itasaidia sana kushinikiza serikali za mataifa mbalimbali kuanza kuchukulia jambo hili kwa uzito, na pia kutoa rasilimali kwa ajili ya utekelezaji wa jambo hili.

Swali: Azimio litakuwa na matokeo kiasi gani katika mataifa husika?

Jibu: Nadhani matokeo yatakuwa makubwa sana. Kwanza kutokana na kuwa wanaharakati ambao walishinikiza serikali zao kuchukua hatua katika ngazi ya Umoja wa Mataifa. Wanaharakati hawa wamefikia hatua ya kushangaza. Hawataacha kuendeleza harakati. Watapata nguvu kutokana na azimio hili. Watakuwa na uwezo wa kwenda kwa jamii zao, serikali, wabunge na mawaziri kuwaambia waanze kuchukua hatua sasa.

Kuna nukuu nzuri sana ya mbunge wa nchini Kenya, Mheshimiwa Linah Jebii Kilimo, ambaye alishinikiza na kufanikisha kutungwa kwa sheria ya kupiga marufuku FGM nchini humo. Na alisema kuwa azimio hili linazidi kuhalalisha kile ambacho amekuwa akipigania katika ngazi ya kitaifa kuingia katika ngazi ya kimataifa.

Wanaharakati wengi duniani kote walisaidia katika kazi yetu. Azimio lilianzishwa na Kilimo. Kama ambavyo nimesema, na kutokana na kuwa walikuwa na nguvu kubwa ya kupambana na FGM huko nyumbani kwao, waliweza kuwa viongozi wa suala hili. Mke wa rais wa Kenya Lucy Kibaki ni mwanaharakati mzuri sana katika mambo mengi, ikiwa ni pamoja na FGM, na alikuwa mratibu wa kimataifa wa kampeni hii. Alifanya kazi kubwa, na pia kufanya ushawishi akiwa na wake za rais wa nchi nyingine.

Moja ya mashirika ambayo tulifanya kazi nayo ni pamoja na "Inter-African Committee on Traditional Practices Affecting the Health of Women and Children". Ni kundi la kamati kutoka nchi 29 barani Afrika na zote zilikuwa zinafanya kazi katika ngazi ya kitaifa kuhamasisha nchi kufanyia kazi jambo hili. (END/2013)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The element 'html' is used but not declared in the DTD/Schema.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>