Inter Press Service News Agency
Monday, June 18, 2018   10:54 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions


Kesi ya Kukomesha Hukumu ya Kifo Nchini Gambia Yaangukia katika Mahakama Isiyokuwa na Meno
Saikou Jammeh

BANJUL, Januari 4 (IPS) - Mahakama ya jumuiya ya kiuchumi katika Afrika magharibi inatarajiwa kusikiliza kesi ya kiraia inayotaka kukomeshwa kwa hukumu ya kifo nchini Gambia mwezi huu wa Desemba, miezi minne baada ya kunyongwa kwa wafungwa tisa na hivyo kuushtua ulimwengu.Umoja wa Vyama vya Kiraia Gambia (CSAG), ambao unahusisha vikundi kadhaa vya vugugu ya demokrasia, ulipeleka kesi hiyo kwa Mahakama ya Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS), ambayo ina mamlaka ya kutoa maamuzi juu ya ukiukwaji wa haki za binadamu. Mahakama hiyo iko wazi kwa watu wote kutoka jumuiya ya ECOWAS, ambayo Gambia ni mwanachama.

Kesi hiyo ni jaribio la kuokoa maisha ya wafungwa 38 waliobakia ambao wako katika foleni ya kutaka kunyongwa ambao ni pamoja na wakuu wa zamani wa ulinzi na usalama wa taifa, maofisa wa jeshi wa zamani na wafanyabiashara wakubwa.

Lakini wataalam wa haki za binadamu nchini Gambia wana wasiwasi juu ya uwezo wa mahakama hiyo wa kuwajibisha taifa hili dogo la Afrika Magharibi juu ya uamuzi wowote linaotoa. Wakati uamuzi wa mahakama hiyo ni wa kisheria kwa wanachama wake, hapo kabla Gambia imekuwa ikipuuza maamuzi ya mahakama hiyo.

"Aina ya mshikamano tunaouona katika ukanda huu mdogo ndiyo kitu kinachotufanya tuwe na furaha," Banka Manneh, mwenyekiti wa CSAG, aliiambia IPS. "Kesi hiyo ilipangwa kufanyika Okt. 31, lakini hata hivyo haikufanyika. Lakini tayari imeshawekwa kwenye kalenda kufanyika mwezi Desemba."

Mwanasheria maarufu wa haki za binadamu nchini Gambia Ousainou Darboe aliiambia IPS: "Nina imani kuwa sasa ni wakati kwa serikali kuchukua hatua kukomesha hukumu ya kifo na kufanyia marekebisho sheria ya sasa ili wale wote waliopo katika hukumu ya kifo kubadilishiwa hukumu zao na kuwa vifungo vya kawaida."

Umoja huo wa mashirika ya kiraia pia umeitaka mahakama ya ECOWAS kuiamuru serikali ya Gambia kukabidhi miili ya wafungwa watatu walionyongwa kwa familia zao "ili waweze kufanyiwa mazishi ya heshima na kufanya maziko ya kidini ambayo ni muhimu katika mazingira kama hayo na yanakwenda sambamba na mila na desturi za wakazi wa nchi hiyo."

Wanaharakati pia walitoa ombi la jumla ya dola milioni moja kulipwa kama fidia kwa familia zenye ndugu zao walionyongwa.

Amadou Bah, mwanafamilia wa mmoja wa wafungwa walionyongwa, aliiambia IPS kuwa familia yake haijaambiwa rasmi juu ya kesi iliyofunguliwa kwa niaba yao. Lakini alisema alifurahishwa mno na kesi hiyo. "Kila mtu amekuwa akizungumza la kwake tangu kunyongwa kwa wafungwa hao, lakini hakuna ambaye alitaka kuchukua hatua. Wanaharakati ambao wameishitaki serikali wamefanya kazi nzuri na tutawaunga mkono na pia watapata maombi yetu."

Wafungwa arobaini na saba wamekuwa wakisubiri kunyongwa katika magereza yenye msongamano wa wafungwa nchini Gambia kabla ya zoezi la kunyongwa la Agosti 23. Hadi wakati huo hakuna ambaye aliwahi kunyongwa kwa karibu miaka 30. Hii ilisababisha shirika la haki za binadamu kimataifa la Amnesty International, kuiweka nchi hiyo katika kundi la nchi zinazotaka kukomesha hukumu ya kifo. Lakini nchi hiyo ilipokonywa hadhi yake baada ya wafungwa tisa, wakiwepo wanaume nane na mwanamke mmoja kunyongwa kwa siri.

Utawala wa Rais Yahya Jammeh ulitetea uamuzi wake, ukisema kuwa unyongaji huo ulikuwa muhimu kukabiliana na kuongezeka kwa vitendo vya uhalifu. "Na kama ninaweza kusaini vibali vya kunyongwa kwa watu 10,000 ili kuokoa maisha ya raia wa Gambia milioni 1.6, nitafanya hivyo kwa furaha kubwa," Jammeh alisema kufuatia kunyongwa kwa wafungwa hao.

Baadaye, serikali ya Gambia ilizidiwa na shinikizo kutoka ndani na nje ya nchi na hivyo kutangaza kusitisha kutoa hukumu za kifo. Lakini wengi walikataa kukubaliana na maneno ya rais huyo mwenye utata.

Magazeti ya ndani yanaripoti kuwa wafungwa 38 wanaobakia wanaishi katika hofu kubwa ya kunyongwa.

Wanafamilia ambao wafungwa waliobakia kunyongwa hawajapata fursa ya kufika katika magereza ambako wapendwa wao wameshikiliwa, na hawajaruhusiwa kuwasiliana nao. Amnesty International ilimnukuu mke wa mmoja wa wafungwa wanaosubiri kunyongwa akisema: "Hatujui nini kinatokea – nani amekufa na nani bado anaendelea kuishi. Na hatujuai ni nani atafuatia kunyongwa."

Familia za wale wanaosubiri kunyongwa hawajashawishika na madai ya Jammeh kuwa unyongaji huo utasitishwa. Hata hivyo, kwa kiasi wamepata ahueni kuwa serikali inakosolewa kisheria.

"Rais alipotangaza kuwa amesitisha kunyonga, hatujashawishika kuwa alimaanisha kile alichokisema. Sijaridhika kwasababu ninaogopa, siyo mzuri katika kutekeleza ahadi," baba wa mmoja wa wafungwa wanaosubiri kunyongwa aliiambia IPS kwa masharti ya kutokutajwa.

Mwanaume wa umri wa miaka 64 ambaye mtoto wake wa kiume alikutwa na hatia ya uhaini, alikuwa na tahadhari na matumaini yake kuwa kambi hiyo ya Afrika Magharibi ingeokoa maisha ya mtoto wake kwani Gambia ina historia ya kushindwa kesi na kutokuheshimu maamuzi ya mahakama yenye makao yake mjini Abuja.

Katika kipindi cha miaka sita iliyopita mahakama imeshafanya kesi mbili dhidi ya serikai ya Gambia – katika kesi ya utesaji ya Musa Saidykhan na kuwekwa kizuizini kinyume cha sheria kwa Ebrima Manneh, ambao wote ni waandishi wa habari wa Gambia.

Serikali ilikutwa kuwa na hatia dhidi ya kuwekwa kizuizini kinyume cha sheria na iliamriwa kumwachia Manneh, ambaye alikamatwa na polisi mwaka 2006 na hakuonekana tena, na kulipa dola 100,000 kama fidia kwa mwandishi huyo. Hata hivyo, hadi sasa hajaonekana tena na kuna uvumi kuwa ameshauawa.

Saidykhan alifungua mashitaka dhidi ya serikali ya Gambia katika mahakama hiyo baada ya kukamatwa na kuteswa na vyombo vya usalama vya Gambia mwaka 2006 na kushutumiwa kujihusisha katika jaribio la kuipindua serikali. Mahakama iliamua kuwa apatiwe dola 200,000 kama fidia, lakini Gambia haijatoa pesa hizo.

Hata hivyo, mahakama ya ECOWAS inaonekana kuchoka kuvumilia nchi ambazo zinashindwa kuzingatia maamuzi ya mahakama.

"Kukaidi maamuzi ya mahakama ni ukiukwaji wa masharti ya nchi wanachama chini ya mkataba wa ECOWAS," Jaji Awa Nana Daboya, mwenyekiti wa mahakama hiyo, alionya mwezi Julai, akitoa wito kwa kambi hiyo kuwekea vikwazo vya kifedha mataifa ambayo yanakiuka masharti ya jumuiya.

Kambi hiyo inazidi kukabiliwa na wito wa kutakiwa kuchukua hatua dhidi ya nchi ambazo haziheshimu mahakama hiyo. Darboe alisema ni wakati muafaka kwa serikali ya Gambia kuheshimu maamuzi ya mahakama.

"Ni kinyume cha sheria kwa serikali ya Gambia kukubali kufungwa na baadhi ya maamuzi ya ECOWAS na kukataa kuheshimu mahakama. Hivi karibuni, niliwahi kuona tangazo la serikali katika shirika la utangazaji la taifa linalotangaza kodi ya ongezeko la thamani na kuihusisha na itifaki ya ECOWAS. Kama tunaweza kutekeleza VAT, ni kwa nini hatuheshimu mahakama, ambayo tumeshiriki kikamilifu katika kuiunda?

"Suala jingine ambalo wakuu wa mataifa ya ECOWAS wanatakiwa kufanya ni kuchukua baadhi ya hatua za adhabu dhidi ya mataifa ambayo yanaamua kutokuzingatia uamuzi wa mahakama. Mahakama haiko pale kupamba mambo, iko pale kwa makusudi," Darboe alisema.

Mwenyekiti wa CSAG Banka Manneh alisema ana matarajio kuwa serikali ya Gambia ingeheshimu maamuzi ya mahakama.

"Tunatumaini kuwa serikali itazingatia wakati huu kwani hili ni suala la kufa na kupona kwa wengi. Natumia neno ‘natumaini’ kwani Jammeh haheshimu kabisa utawala wa sheria na wajibu wa kimataifa wa taifa la Gambia," alisema.

CSAG ilishutumu nchi hiyo kutokana na kukiuka sheria za kimataifa za haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu. Ukiwa pia unajulikana kama Mkataba wa Banjul, uliandaliwa mwaka 1979 na unataka, miongoni mwa mambo mengine, kuheshimiwa kwa haki ya kuishi. Mkataba huo, ambao uliunda Umoja wa Nchi Huru za Kiafrika, uliridhiwa na nchi zote wanachama, ikiwepo Gambia yenyewe. (END/2013)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The element 'html' is used but not declared in the DTD/Schema.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>