Inter Press Service News Agency
Saturday, March 28, 2015   12:18 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   JAPANESE
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions

Mwaswali na Majibu
Kutegemea Demokrasia Kuleta Maendeleo Endelevu
Busani Bafana

BULAWAYO, Januari 4 (IPS) - "Kukuza shinikizo la kimazingira na kuongezeka kukosekana usawa kiuchumi kunazidisha mabadiliko makubwa ya kijamii duniani, na hivyo kuifanya demokrasia iliyopo kuingia katika majaribu," Halina Ward, mkurugenzi wa shirika lenye makao yake mjini London la "Foundation for Democracy and Sustainable Development", anaiambia IPS.

"Demokrasia, hata hivyo, haifanyi kazi nzuri, inazidisha tu madhara ya changamoto hizo, badala ya kuziona kama fursa za kuleta mageuzi."

Shirika hilo, ambalo linafanya utafiti wa maendeleo endelevu, linajaribu kuhusisha demokrasia na maendeleo endelevu katika andiko lake la "ilani ya mabadiliko", ambalo litazinduliwa kimataifa Machi 2013. Ilani hiyo ni wito kwa wananchi wa kimataifa na viongozi wa kutafuta njia za kujenga demokrasia ili kuwa na mazingira yenye afya na usawa kwa wote.

Ward anamwambia mwandishi wa IPS Busani Bafana ni kwa nini anadhani demokrasia inaweza kuleta maendeleo endelevu. Sehemu ya mahojiano inafuata:

Swali: Ni nini kinakuja kwanza, demokrasia au maendeleo?

Jibu: Kuna mjadala mkubwa juu ya swali hilo, na kuna baadhi ya serikali za kimabavu ambazo zinasema kuwa unatakiwa kuleta maendeleo ya kiuchumi kwanza na baadaye demokrasia. Kutokana na mtizamo huu, swali hili siyo sahihi. Wasiwasi wetu ni maendeleo endelevu kuliko ukuaji wa kiuchumi. Na ilani hii haihusu "kushinikiza demokrasia". Kama ukianza na mtizamo wa maendeleo endelevu, ambayo yanahusu dhana za usawa na hifadhi ya mazingira ikiwa ni pamoja na maendeleo ya kiuchumi, hakuna cha kutenganisha demokrasia.

Moja ya mambo chanya ambayo yamekuja mwaka huu katika mkutano wa Umoja wa Mataifa ni kutambua kuwa demokrasia ni muhimu kwa maendeleo endelevu. Na tunadhani kuwa demokrasia yenyewe inahitaji maendeleo endelevu – kwasababu maendeleo yasiyokuwa endelevu na yasiyokuwa ya usawa, ikiwa ni pamoja na kuendelea kushindwa kutokomeza umaskini uliokithiri, kunaweza kuleta vikwazo vikubwa vya demokrasia.

Swali: Katika bara la Afrika, demokrasia na maendeleo endelevu bado ni ndoto. Ni tofauti gani italetwa na ilani hii katika bara la Afrika?

Jibu: Tunafanya kazi na dhana kuwa watu, vikundi vya kiraia na wawakilishi waliochaguliwa wanaweza kutoa ahadi ambazo kwa pamoja zinaweza kuleta mabadiliko katika demokrasia. Tumechukua dhana ya kutengeneza "mabadiliko ya kujirudia rudia" kwa kuzindua ilani na michakato ya kufanyia majaribio na ubunifu. Tunatumaini kuwa ilani itakuwa rasilimali muhimu kwa watu na mashirika mahali popote kujua kuwa ni muhimu kuzungumzia jinsi gani ya kuingiza demokrasia katika maendeleo endelevu.

Lakini nina wasiwasi kuwa wasomaji wa Afrika wa ilani watakuta kuwa kuna mengi ya kufanyika kuwezesha mifumo kadhaa ya demokrasia katika bara inakuja kuwa kweli. Pia napenda kusisitiza kuwa tumekuwa na maoni machache kutoka kwa raia wa Afrika ikilinganishwa na watu katika pande nyingine za dunia katika kukusanya maoni ya ilani hii.

Tutazindua ilani kama waraka ambao utakuwa na mtikisiko wa kidunia – lakini kwa kutambua kuwa ilani na mchakato wa kuufanyia majaribio na ubunifu unaoambatana nao, utahitaji kutumia muda mwingi.

Tutafurahishwa, kwa mfano, kama utasababisha kuwepo kwa mpango wa kutengeneza kanuni na hatua maalum kwa muktadha mbalimbali wa Kiafrika.

Ni kama kupatia uwezo wa kufanya kazi wa harakati binafsi za kuleta mabadiliko, badala ya kueneza ilani "yetu" duniani kote.

Swali: Ni kwa nini kuwa na ilani ya mabadiliko?

Jibu: Kwasababu tunataka kubadili miaka yetu mitatu ya ushirikiano, uchambuzi na utetezi katika FDSD kuwa katika warakati wa kuchukua hatua. Ufumbuzi wa mgongano kati ya demokrasia na maendeleo endelevu unaendelea – tumeshawishika kuwa unatekelezwa.

Tunachohitaji ni waraka mzuri ambao unajenga faida inayoenea, na kuruhusu ufumbuzi huo kuenea mahali pengine. Tuna imani kuwa ilani itakuwa kichocheo cha mabadiliko, kama ambavyo ilani nyingine zimeweza kufanya katika siku za nyuma, na zitafika mbali zaidi ya jamii ndogo ndogo za ndani kugusa uzoefu unaoonekana wa demokrasia kama mfumo wa kisiasa katika muktadha za aina mbalimbali.

Swali: Ilani italenga kwenye nini?

Jibu: Ilani itaangalia mtizamo mpana wa jinsi gani demokrasia itakavyoonekana inapokuwa na nafasi nzuri ya kuleta maendeleo endelevu, kuorodhesha kanuni za msingi zinazoendana na maono hayo na kutoa mapendekezo ya ubunifu ambao unapaswa kufanyika ili kutekeleza kanuni hizo. Utakuwa ni waraka mdogo, kurasa mbili hadi tatu, wenye sauti chanya na ya kiubunifu ambayo tunategemea itasaidia kuhakikisha mafanikio.

Swali: Demokrasia inaweza kuleta maendeleo endelevu?

Jibu: Kwa sasa demokrasia ina uwezo wa kuleta maendeleo endelevu lakini haifanyi hivyo. Mara nyingi demokrasia zinaelekezwa kukidhi maslahi ya muda mfupi ya uchaguzi, na kulenga kwa kiasi kidogo katika ukuaji wa kiuchumi. Katika kufanya mambo kuwa mabaya zaidi, baadhi ya demokrasia hata hazina haki za msingi. Zinakiuka haki za msingi za binadamu, zinashindwa kutoa habari na haki, na zinakosa kuheshimu utawala wa sheria. (END/2013)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
Decent Employment Opportunities for Young People in Rural Africa
Kenya Struggles with Rising Alcoholism
Smugglers Peddle ‘Conflict Diamonds’ from Central African Republic, Ignoring Ban
Winners Announced for Free Expression Prize
Gates Foundation Slammed for Plan to Privatise African Seed Markets
Opinion: Water and Sanitation in Nigeria – Playing the Numbers Game
High-Tech to the Rescue of Southern Africa’s Smallholder Farmers
Sparks Fly As Sierra Leone’s VP Is Expelled From Party
Women Often Forgotten In Cases Of Forced Disappearance
Anger Seethes in Gabon after Wood Company Sacks Protesting Workers
More >>
  Dernières Nouvelles
News in RSS
Decent Employment Opportunities for Young People in Rural Africa
Kenya Struggles with Rising Alcoholism
Smugglers Peddle ‘Conflict Diamonds’ from Central African Republic, Ignoring Ban
Winners Announced for Free Expression Prize
Gates Foundation Slammed for Plan to Privatise African Seed Markets
A lire également>>