Inter Press Service News Agency
Wednesday, April 25, 2018   23:01 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions

Maswali na Majibu
: "Ni Wakati wa Kupigana Vita ya Ubaguzi wa Ushoga"
Rebecca Hanser

UMOJA WA MATAIFA, Januari 4 (IPS) - Kwa zaidi ya miongo miwili sasa, mwimbaji wa kimataifa na mwanaharakati wa haki za binadamu Yvonne Chaka Chaka amekuwa mstari wa mbele katika muziki wa pop nchini Afrika Kusini.

Akiwa amekua wakati wa siasa za Ubaguzi wa Rangi, Chaka Chaka alikuwa na wakati mgumu utotoni mwake. Baada ya kupoteza baba yake akiwa na umri wa miaka 11, mama yake Chaka Chaka aliachwa kuwalea mabinti zake watatu kama mama mjane kwa kutumia mshahara wake mdogo.

Alikulia katika jamii ambayo ilijaa ubaguzi wa kijamii, matabaka na ukabila, lakini hii haikumzuia Chaka Chaka kuhitimu masomo yake akiwa na diploma mbili kutoka Chuo Kikuu cha Afrika Kusini (UNISA).

Alionekana mjini Johannesburg mwaka 1985 na alikwenda kutoa albamu yake iliyoshinda tuzo yenye nyimbo kama "I Cry for Freedom", "Back on my Feet" na "Power of Africa".

Chaka Chaka hakufikia tu ngazi ya kuwa nyota nchini Afrika Kusini na katika muziki aina ya Mbaganga –mtindo wa muziki wa Afrika Kusini – lakini pia alipewa jina la "Malkia wa Afrika."

"Kuwa mtu maarufu na kufuatiliwa na wengi ni faida kubwa lakini inakuja na wajibu maalum," mwanamuziki huyo aliiambia IPS katika mahojiano.

Malkia wa Afrika anajulikana pia kwa kazi za misaada kwa jamii. Kwa kuongeza katika jukumu lake kama Balozi wa Hisani wa UNISA na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Gestetner Tshwane, UNICEF pia imemteua kuwa Balozi Maalum wa Malaria katika kanda za Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika.

Chaka Chaka alizungumza na mwandishi wa Umoja wa Mataifa Rebecca Hanser jinsi alivyokua nchini Afrika Kusini, maisha yake kama nyota wa kimataifa, na kazi yake kama mwanaharakati wa haki za binadamu anayepambana na kutokujua kusoma na kuandika, umaskini, ubaguzi dhidi ya ushoga na maradhi kama VVU na malaria.

Swali: Ukiwa umekulia nchini Afrika Kusini, hali ilikuwaje katika suala zima la ubaguzi wa rangi nchini mwako?

Jibu: Nilizaliwa huko Soweto na kukulia chini ya ubaguzi wa rangi. Mapambano dhidi ya ubaguzi yalijipenyeza sana katika mishipa yangu ya damu. Najua ina maanisha nini kutendewa kama mtu asiyekuwa na thamani kutokana na ngozi yako.

Tulipoijenga upya nchi yetu tuliijenga kwa misingi ya usawa na utu sawa wa kila mtu katika jamii yetu.

Tulijifunza somo juu ya ugumu wa maisha nchini Afrika Kusini lakini hatutasahau. Nelson Mandela alijenga taifa la Upendi wa Mvua na naamini sote ni sawa. Hilo ndilo tulilofikiri: uhuru wetu.

Swali: Katika bara zima la Afrika, ubaguzi uliojikita katika rangi, ukabila na mapendeleo ya kujamiiana bado unaonekana. Habari za matumizi ya nguvu na ubaguzi dhidi ya jamii ya mashoga uliotokana na familia zao wenyewe zinatufikia karibu kila siku. Wewe ukiwa mama, una jibu gani katika hili?

Jibu: Habari hizi zinanivunja moyo wangu. Jambo la kusikitisha, tunasikia habari kama hizo kutoka maeneo mengi tofauti ya dunia. Je haitoshi kuwanyanyapaa, kuwabagua na kuwashambulia dada na kaka zetu ambao ni mashoga?

Ukweli kwamba mtu hawezi kutegemea hata upendo wa wazazi wake mwenyewe ni hali mbaya. Ni aina gani ya mama ambaye unaweza kumfanyia mtoto wako namna hii?

Nikiwa kama mama wa watoto wanne wa kiume, naona kazi yangu ikiwasaidia kuwa watu wazuri; kujitambua; kuwa wenye furaha na salama; kupenda na kupendwa. Mara nyingi nimesema kuwa sijali kama wananiletea nyumbani wake Wahindi au Maalbino, Patricia au Peter, ninachojali tu ni kwamba wawe na furaha maishani.

Swali: Hivi karibuni ulijiunga na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon na mwanamuziki wa mitindo ya pop Ricky Martin katika tukio maalum juu ya haja ya kuwa na uongozi katika kupambana na ubaguzi dhidi ya ushoga katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa. Unaweza kuelezea juu ya sheria barani Afrika, na hasa sheria dhidi ya ushoga katika mataifa ya Afrika?

Jibu: Nchi nyingi mno katika bara bado zina sheria ambazo zinatishia ushoga na zinautaja kama kosa la jinai.

Wakati mataifa ya Ulaya yanapotuambia kuwa sisi kama Waafrika tunatakiwa kuondokana na sheria hizi, unasikia watu wakisema "Hapana, sisi siyo makoloni tena, hizi ni sheria zetu na tutaendelea nazo." Lakini sheria hizi zinatoka wapi? Katika karibu nchi zote zililetwa na watawala wa kikoloni wa zamani. Nyingi ziliandikwa mjini London katika Karene ya 19! Hazina nafasi katika Afrika ya kisasa.

Ninaposikia kuwa wabunge nchini Uganda wanataka kuanzisha sheria ya hukumu ya kifo kwa mashoga au kuwa wabunge nchini Nigeria wanataka kuimarisha adhabu zilizopo kwa wanandoa wa jinsia moja, inanifanya kuwa na hasira na mkanganyiko ambao watu wanapandikizwa nao. Ni lini tumeanza kufanyiana sisi wenyewe ukatili kama huo?

Tunahitaji kuanza tena na kukumbuka kuwa sisi sote tulizaliwa tukiwa huru na sawa na tunatakiwa kuwa na nafasi ya kuishi jinsi tulivyo katika maisha yetu yote. Tunahitaji kuheshimiana na wala siyo kuhukumiana au kuogopana.

Swali: Unadhani nini kinapaswa kubadilika kutatua hali ya wale wanaobaguliwa na kushambuliwa kutokana na kuwa tofauti na sisi?

Jibu: Jambo la kwanza kufanya ni kuondokana na sheria hizi za zamani ambazo zinafanya ushoga kuwa kosa la jinai na tunahitaji kuwa na sheria za kulinda kila mmoja asibaguliwe, ikiwa ni pamoja na kubaguliwa kwa misingi ya upendeleo wa kuchagua wapenzi na kutokana na jinsia ya mtu. Mara tutakapokuwa tumefanya hili, tuna kazi kubwa mikononi mwetu, ambayo ni kubadili mitizamo yetu kwa jamii, kusaidia watu kufungua mioyo yao na mawazo yao.

Kubadili sheria ni hatua muhimu ya kwanza, lakini itachukua njia ya elimu, mafunzo na kuzungumza pamoja kuondokana na ubaguzi dhidi ya ushoga. Lakini tunajua inawezekana. Tunapata mafanikio katika vita dhidi ya ubaguzi wa rangi na kujamiiana. Ni wakati wa kuchukua hatua kupambana na ubaguzi wa ushoga. Hii ni vita ambayo tunaweza kushinda kama wote tutatimiza wajibu wetu. (END/2013)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The element 'html' is used but not declared in the DTD/Schema.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>