Inter Press Service News Agency
Thursday, June 21, 2018   09:53 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions


Ndoto za ‘Mpango wa Kijani’ Zafifia Katika Maghreb
Julio Godoy

BERLIN, Januari 3 (IPS) - Mpango wa Viwanda wa Desertec (DII), umoja wa makampuni makubwa 21 ya Ulaya, mpango wa kwanza kufunga mtandao wa mitambo ya kuzalisha umeme wa mvuke, umeme wa jua, na umeme wa upepo katika ukanda mzima wa Maghreb katika Afrika ya Kaskazini, ulipokelewa kama ‘mpango wa kijani’. Ukitarajiwa kuzalisha gigawati za umeme 100 ifikapo mwaka 2050, mradi ulihitaji uwekezaji wa euro bilioni 400.

Katika utafiti uliotolewa katika majira ya kiangazi yaliyopita, mpango wa Desertec ulitarajiwa kuunganisha mifumo ya umeme ya Ulaya, Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini ingeruhusu Ulaya kufikia mahitaji yake ya kupunguza hewa ya carbon dioxide (CO2) na kufikia lengo la asilimia 95 katika sekta ya umeme kwa kuingiza hadi asilimia 20 ya mahitaji ya umeme ya Maghreb, na hivyo kuokoa euro bilioni 33 kwa mwaka.

Vile vile, mradi huo ungewezesha mataifa ya Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini kufikia mahitaji yake ya umeme kwa kutumia rasilimali kubwa za jua na upepo zinazopatikana katika ukanda huo, na kufikia asilimia 50 ya upunguzaji wa hewa ya CO2 katika sekta ya nishati pamoja na kuongezeka kwa kiasi kikubwa kwa mahitaji.

Ukanda huo utafaidika na viwanda vya kusafirisha bidhaa nje vyenye thamani ya euro bilioni 63 kwa mwaka.

Kwa sasa, miaka mitatu tangu mradi ulipotangazwa, ndoto ya mpango wa Desertec bado haijafikiwa, na kuufurahia mpango huo kumekosolewa vibaya kuwa siyo wa kiushindani na una udhaifu katika utawala wa kikampuni.

Mradi umepewa jina la "hatua za kukata tamaa" na wafanyakazi wa ndani ambao hawakuridhishwa na mfumo unaofuatwa.

Fursa kubwa

Katika kile kilichojulikana kama "White Book" katika mradi, DII ilidai, "fursa ya muda mrefu ya kiuchumi ya nishati mbadala katika EUMENA (Ulaya, Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini) ni mkubwa zaidi ya mahitaji ya sasa, na fursa za nishati ya jua zinapunguza kila situ."

Wakijikita katika takwimu za taasisi ya utafiti ya Kijerumani na "Club of Rome", ripoti inakadiria kuwa, "katika kila kilomita ya mraba ya ardhi ya jangwa, hadi gigawati 250 za umeme zinaweza kuvunwa kila mwaka kwa kutumia teknolojia ya umeme wa mvuke."

Kila kilomita moja ya ardhi katika MENA "inapata kiasi cha nishati ya jua ambacho ni sawa na mapipa milioni 1.5 ya mafuta yasiyosafishwa. Mitambo ya kuzalisha umeme wa jua katika shamba lenye ukubwa wa ziwa Nasser nchini Misri (Aswan), wa baadhi ya kilomita za mraba 6,000, zinaweza kuzalisha nishati sawa na uzalishaji wa mafuta yote ya Mashariki ya Kati kwa sasa".

Morocco, ambayo itakuwa mwenyeji wa mradi wa majaribio, imekuwa na nia ya kuona ndoto hizo zinazaa matunda, kwani itakuwa na matokeo makubwa katika uchumi wa ndani, hasa katika suala zima la kujenga ajira katika sekta ya nishati mbadala.

Ukirejea mwaka 2009, ‘mitandao ya kijani’ iliundwa katika miji kadhaa katika Morocco, ikiwa ni pamoja na Casablanca. Ikiwa na makampuni madogo yanayoongozwa na vijana wasomi, mitandao hii ilibuniwa kujenga miundombinu muhimu kwa mradi huo.

"Tumeunda makampuni, tumepata mafunzo, lakini katika hali halisi hakuna ambalo limejitokeza sasa," Abdellah Benjdi, mmoja wa wakuu vijana wa kampuni, aliiambia IPS.

Wananchi wa kawaida wanaokabiliwa na bili kubwa za umeme nchini Morocco wanasubiri kwa hamu mradi unaojulikana kama ‘mpango wa kijani’.

Lakini dalili zote zinaonyesha kuwa uvumilivu wao bado haujafikia wakati wa kupata matunda.

Vikwazo visivyokuwa na mwisho

Wataalam walipokea kwa mara ya kwanza uthibitisho wa ugumu wa Desertec Nov. 7 mjini Berlin, wakati ambapo uwasilishwaji rasmi juu ya mitambo ya nishati ya mvuke, nishati ya jua na upepo itakayofungwa katika jimbo la Ouarzazate nchini Morocco, ambayo imepangwa kuzalisha umeme ifikapo mwaka 2014.

Pamoja na kwamba mipango ya ujenzi kiufundi imeshafungwa, bado inategemea kupitishwa na Hispania – kwani Hispania ni mshirika wa msingi katika mradi – kwa kuruhusu umeme kuzalishwa katika kituo ambacho unaweza kusafirishwa kwenda Ulaya.

Serikali ya Hispania, ikiwa imeandamwa na mtikisiko wa kiuchumi, hadi sasa haijaweza kuthibitisha kuunga kwake mkono mradi huo, hali ambayo haina uwezekano wa kubadilika hasa kutokana na kuwa Hispania ni msafirishaji mkuu wa umeme kwenda Morocco na isingeweza kuona hali hii inabadilika kwa utekeleza kimafanikio mradi wa majaribio wa Ouarzazate, wanasema wataalam.

Umoja wa DII ni pamoja na Benki ya Ujerumani ya Deutsche na shirika la Kihispania la kusafirisha umeme na linaloongoza umeme wa gridi la TSO Red Eléctrica.

"Suala la biashara la Kumbukumbu ya Mradi wa Desertec, lililoandaliwa na Shirika la Umeme wa Jua la Morocco la Masen, limejadiliwa kwa undani kwa kipindi cha miaka miwili na makampuni ya Hispania ya TSO Red Eléctrica na Tume ya Ulaya, na kutangazwa kuwa unawezekana kutekelezwa," Mkurugenzi Mtendaji wa DII Paul van Son alisema wakati wa uwasilishaji wake mjini Berlin.

Mradi wa kwanza wa Morocco ukiongozwa na kampuni kubwa ya nishati ya Ujerumani ya RWE ungeweza kuwa na uwezo wa megawati 100 unaotokana na jua na upepo.

Mradi wa pili, unaotumia mvuke na unaosimamiwa na kampuni ya Saudi Arabia ya ACWA Power International, utakuwa na uwezo wa kuzalisha megawati 160.

Miradi yote hiyo inatarajiwa kuanza kufanya kazi ifikapo mwaka 2014.

Van Son alithibitisha, "Wawekezaji wameshapatikana, ruzuku za awali zimepatikana, na viwanda vinataka kushiriki." Lakini Hispania ilikataa kupeleka wawakilishi katika uwasilishaji wa Berlin, na hadi sasa imeshindwa kusaini mradi wa Morocco.

Van Son imeshawishika kwamba "washirika wengine katika mazungumzo haya, kutoka Morocco na EU, wataweza kuishawishi Hispania," kwani serikali ya Hispania, pia, ina uwezekano wa kufaidika na mradi huo.

Kukosekana kwa uratibu

Lakini kukataa kwa Hispania ni mfano mmojawapo tu wa vikwazo vikubwa vya uratibu wa kisiasa, kiufundi na kifedha ambavyo mradi unapaswa kuvikabili.

Moja ya dalili ya ugumu huu ulikuja mwishoni mwa Oktoba, wakati shirika kubwa la simu la Kijerumani la Siemens lilipotangaza kujiondoa kwake katika umoja huo, pamoja na kuwa mwanachama mwanzilishi wa DII mwaka 2009.

Hatua hii imetafsiriwa kwa kiasi kikubwa kuwa uthibitisho kuwa mradi wa Desertec unashindwa.

Kwa mujibu wa Friedrich Fuehr, mwanachama mwanzilishi wa bodi ya wakurugenzi katika Mfuko wa Desertec, DII "imekuwa ikifuatilia mkakati mbaya".

Fuehr aliiambia IPS kuwa wajibu mkubwa wa DII tangu mwaka 2009 ni kuwa na mkakati wa kisiasa ambao utaweza kusababisha kuepukana na matatizo yote ya uratibu wa kimataifa na kutatua masuala makubwa ya jinsi gani ruzuku na kodi zingeweza kutekelezwa.

Fuehr, mwanasheria mwenye hadhi kubwa wa Kijerumani na mshauri mtaalam wa biashara, alisema kuwa "umoja wa makampuni yenye nguvu ya binafsi kama vile Benki ya Deutsche, UniCredit, RWE na SCHOTT Solar itaweza kuanzisha katika kipindi cha miaka mitatu mkakati wa kisiasa unaohitaji kuufanya mpango wa Desertec kuwa wa kweli".

"Lakini bado tunasubiri mkakati huu," Fuehr alisema. "Badala yake, DII imejikita zaidi katika hatua zake zote katika kuzindua mradi mmoja wa mfano katika eneo la Ouarzazate."

Fuehr alilaumu kuwa mapinduzi ya nishati ambayo dunia inayahitaji ili kukabiliana na uhalisia wa kuongezeka kwa joto ulimwenguni "tayari unajitokeza. Lakini Desertec haijashiriki katika mpango huo". (END/2013)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The element 'html' is used but not declared in the DTD/Schema.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>