Inter Press Service News Agency
Thursday, April 26, 2018   20:12 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions


Somaliland Yaibuka Kutoka Kwenye Uharibifu wa Somalia
Matthew Newsome

HARGEISA, Januari 3 (IPS) - Wakati Somalia ikianza kuibuka kutoka katika kukosekana kwa utulivu na machafuko, miaka 20 ya kiasi fulani cha amani na utulivu inaanza kulipa kwa jirani yake wa karibu Somaliland, kwani mwezi wa Novemba walisaini mkataba mkubwa wa kwanza wa kutafuta mafuta na gesi tangu ilipojitenga kutoka Somalia mwaka 1991. Kampuni yenye asili ya Uingereza na Uturuki ya Genel Energy ilipata leseni kutoka kwa serikali ya Somaliland mapema mwezi wa Novemba kutafuta na kujenga visima vya mafuta na gesi baada ya kuahidi kutumia karibu dola milioni 40 kwa ajili ya kazi za uchunguzi wa mafuta. Genel iliiambia IPS "Somaliland ina fursa ya kuvutia ya kijiolojia, na tunatazamia kuanza kufanya kazi katika ukanda huu."

Kampuni huru ya uchunguzi na uzalishaji wa mafuta na gesi imekuwa mwekezaji wa kwanza wa kigeni kuahidi kutumia kiasi kikubwa hicho cha mtaji katika sekta ya nishati nchini humo, baada ya uchunguzi wa kwanza kuonyesha "hifadhi kubwa za mafuta" ilisema taarifa ya Genel.

Genel Energy, ambayo hapo zamani iliongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa BP Tony Hayward, inatarajia kuanza uchunguzi wa mafuta na gesi kabla ya mwisho wa mwaka huu.

Nguvu kubwa ya uchumi wa taifa hilo la Pembe ya Afrika kwa asili umekuwa ni ufugaji mifugo. Kwa kuwa na idadi kubwa ya mifugo ambayo ni mara tatu ya idadi ya wakazi wapatao milioni 3.5, biashara ya mifugo inazalisha hadi asilimia 65 ya pato la taifa la nchini humo, Waziri wa Mpango wa Somaliland Dk. Saad Shire aliiambia IPS.

Kutokana na kuwa na bajeti ndogo ya taifa ya dola milioni 120, serikali ya Somaliland kwa sasa inaanza kupata mapato yanayohitajika zaidi kutoka wawekezaji binafsi wa kigeni kuanza maendeleo yake.

Hifadhi ya mafuta na gesi katika Somaliland ilivutia makampuni makubwa zaidi ya mafuta kama vile kampuni yenye makao yake nchini Afrika Kusini ya Ophir Energy, Jacka Resources Ltd ya Australia, na Petrosoma Ltd, kampuni ndogo ya kampuni yenye makao yake nchini Uingereza ya Prime Resources – ambazo zote hizo zilionyesha nia yake ya kuwekeza nchini humo.

Somaliland imeathirika kwa muda mrefu kutokana na kutokutambuliwa kimataifa kwa kipindi cha miaka 21 iliyopita. Kutokana na kutokutambuliwa kisheria imekuwa kikwazo cha kufikia matarajio yake ya kiuchumi – makampuni machache ya bima yamejiandaa kuwekea bima makampuni ya kigeni kuwekeza huko. Hapo kabla wawekezaji waliiona Somaliland kama iliyopooza kiuchumi.

Kutokana na sababu hizi nchi hiyo pia haikuweza kuhitimu kupata msaada wa kifedha kutoka Shirika la Fedha Ulimwenguni na Benki ya Dunia.

Hata hivyo, mwaka 2012 sekta binafsi katika Somaliland zilianza kupata mafanikio.

Mwanzo mwa mwaka, mkutano wa kwanza wa uwekezaji kati ya Uingereza na Somaliland ulifanyika kuchagiza ushirikiano wa kibiashara baina ya nchi hizo mbili. Na kiwanda cha soda aina ya Coca-Cola cha thamani ya dola milioni 17 kilianzishwa mwezi Mei na kampuni ya Djibouti na kuifanya kuwa kampuni kubwa zaidi binafsi ya uwekezaji nchini Somaliland tangu mwaka 1991. Wawekezaji waliona kuwa uamuzi wa Coca-Cola kuanza kufanya kazi katika ukanda huo kama mwanzo chanya wa mazingira tulivu ya biashara.

Bandari ya Somaliland ya Berbera pia inatarajia kuanza uwekezaji mkubwa katika miaka ijayo. Inaonekana kama tunu katika uchumi wa nchi. Ikiwa hapo awali ilijengwa na taifa la Urusi ya zamani wakati wa Vita Baridi, kwa sasa bandari hiyo inafanya kazi kama lango kuu la usafirishaji nje wa mifugo nchini humo. Kuna fursa kubwa kuwa kitovu cha usafirishaji nje wa mafuta na gesi kutoka nchi zisizokuwa na bandari za Afrika kama vile Ethiopia.

"Tupo eneo la kimkakati – Berbera ipo katika eneo la pitio la meli – meli 30,000 zinapitia katika bandari yetu kila mwaka zikitoka Ulaya, Mashariki ya Kati na Asia. Tunaweza kuendeleza Berbera na kuwa bandari kubwa kama ilivyo kwa Singapore – huku ikiwa na mageti ya makontena, maeneo ya kuhifadhia bidhaa, mitambo ya kusafishia mafuta, na huduma zinazohusiana na biashara za baharini," Shire alisema.

Meneja wa bandari hiyo, Ali Omar Mohamed, ana matumaini kuhusu uwezekano wa kupanua bandari hiyo ili kuifanya kuwa kitovu cha biashara kati ya Afrika na Mashariki ya Kati.

"Bandari hii inaweza kuwa kubwa na yenye mafanikio kama ya Djibouti. Ni suala la muda tu kabla ya kuvutia wawekezaji kuifanya kuwa ya kisasa na kuipanua ili kwamba tunaweza kuongeza uwezo tunaohitaji kufikia mahitaji kamili ya kiuchumi," aliiambia IPS.

Shire ana matumaini kuwa kama Somaliland inakuwa na muundo mzuri wa kibiashara unaotambulika kisheria, na kuwa na hatua bora za kiusalama kuongeza imani ya wawekezaji binafsi, itavutia wawekezaji kuibadili nchi na kuwa ya demokrasia yenye kustawi kama ilivyo Singapore. "Tuna utulivu na bandari, tuna kile ambacho wawekezaji wanakitafuta. Kama Singapore inaweza kufanya hivyo, nadhani na sisi tunaweza," alisema.

Kukosekana kwa bima kwa ajili ya wawekezaji ni kikwazo kikubwa zaidi cha maendeleo nchini kwa mujibu wa J. Peter Pham wa Kituo cha Afrika cha Michael S. Ansari, ambacho kilianzishwa kusaidia kuleta mageuzi ya sera za Marekani na Ulaya katika bara la Afrika.

"Bila ya kutambuliwa kimataifa na kupata fedha kutoka taasisi za kimataifa, wananchi wa Somaliland watakabiliwa na vikwazo vikubwa vya kufikia maendeleo ya kiuchumi ambavyo vitaendelea kuwepo hata kukiwepo utulivu wa kisisa na utawala wa kidemokrasia," aliiambia IPS.

"Siyo suala la kupata tu misaada ya kimaendeleo na mikopo ya kimataifa, lakini pia kuwa na mfumo wa kisheria ambapo washirika wa sekta binafsi watapata bima na kuwa na uhakika wa vitega uchumi vyao," alisema.

Kwa mujibu wa Pham, Somaliland haitakuwa katika nafasi ya kufaidika kikamilifu na rasilimali zake ilizojaaliwa kama itaendelea kukataliwa kuwa na hadhi ya taifa linalojitegemea.

"Fursa za maliasili nchini Somaliland – ikiwa ni pamoja na mafuta na gesi, madini na uvuvi – haziwezi kutumika kama hakuna azimio la kuifanya nchi kuwa huru na inayojitegemea."

Kuendelea kuhitajika kwa uwekezaji wa kigeni kulionyeshwa katika mpango wa maendeleo wa taifa wa 2012 hadi 2016 ambao uliandaliwa na serikali Desemba 2011. Unaelezea haja ya kuwepo kwa uwekezaji katika miundombinu ya nchini humo kama vile barabara na maeneo ya kutupia taka. Jumla ya mtaji unaohitajika kufadhili mpango huo ni dola bilioni 1.19.

Kwa mujibu wa Shire, kiasi kikubwa cha uwekezaji huu kinatarajiwa kutoka kwa vyanzo vya kigeni ikiwa ni pamoja na misaada ya wafadhili na wawekezaji wa kigeni.

Hata hivyo, kuna hatari kuwa bila ya kuwepo kutambuliwa na jumuiya ya kimataifa, maendeleo yatakwenda taratibu mno na inaweza kusababisha sehemu ya wakazi kushawishiwa na kuwa rahisi kujiunga na vikundi vya kigaidi kama Al-Qaeda wa Somalia ambao wanahusishwa na kikundi cha Al-Shabaab.

Kwa mujibu wa Pham, kushindwa kwa jumuiya ya kimataifa kutafutia ufumbuzi suala la utaifa wa Somaliland kunaifanya nchi hiyo kuwa katika hatari halisi na kuifanya kuwa rahisi kushawishiwa na vikundi vya kigaidi vya Kiislam.

"Kitu ambacho jumuiya ya kimataifa inahitaji ni kuelewa kuwa kama hakuna litakalofanyika kuinasua Somaliland kutoka katika mtego ambao imefungwa, mambo hayataweza kwenda vizuri.

"Idadi kubwa ya wakazi vijana ambao matarajio yao ya maisha ni madogo kutokana na vikwazo vya maendeleo ya kiuchumi wanaweza kujikuta wakikubaliana na sauti ambazo ni tofauti mno na zile za viongozi wenye maono ambao wameijenga Somaliland kutoka kwenye uharibifu wa Somalia ya zamani," alisema. (END/2013)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The element 'html' is used but not declared in the DTD/Schema.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>