Inter Press Service News Agency
Tuesday, May 22, 2018   10:56 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions

Maswali na Majibu
Utoaji wa Huduma za VVU Huanzia katika Elimu
Julia Kallas

UMOJA WA MATAIFA, Januari 3 (IPS) - Wakati Shorai Chitongo alipoanzisha shirika la "Ray of Hope", ambalo lilikuwa na kazi ya kusaidia wanawake walioepukana na vipigo vya majumbani mwaka 2005, aligundua kuwa robo tatu ya waliowahi kukabiliwa na unyanyasaji katika kundi hilo walikuwa na VVU.

"Wanawake kuongea na kujiamini kwa kiasi kikubwa ni muhimu katika kupambana na VVU/UKIMWI," Chitongo, kiongozi wa jamii ambaye anapambana kupatia uwezo na kulinda jamii nchini Zimbabwe na kiongozi wa kitaifa wa shirika la "Groots Zimbabwe Home-Based Care Alliance", aliiambia IPS. Unyanyasaji wa majumbani unaongeza moja kwa moja nafasi ya kupata maambukizi ya ngono ambayo yanafanya wanawake kuambukizwa VVU.

"Kama wanawake wanatoa sauti zao kiasi cha kutosha, wanakuwa na uwezo wa kujadili kuhusu kufanya ngono salama kama wapenzi sawa na wala siyo wanaokandamizwa," Chitongo alielezea.

Mwandishi wa habari wa IPS Julia Kallas alizungumza na Chitongo kuhusu uhusiano kati ya unyanyasaji wa kingono na VVU/UKIMWI na jinsi gani jitihada za wanawake katika ngazi ya chini kabisa katika jamii zinaweza kukuza huduma za VVU na kusaidia wagonjwa.

Swali: Mwaka 2005, kesi yako ya unyanyasaji majumbani ilivutia vyombo vya habari kitaifa na pia ulikuwa ukionewa huruma. Ni kitu gani kilikushawishi kuanzisha shirika la "Ray of Hope: kusaidia wanawake wenye VVU?

Jibu: Kuanzishwa kwa shirika la "Ray of Hope" kunaanzia mwaka 2005, wakati nilipoona makala ya video katika kipindi cha TV na kujifunza kuwa shirika la "Girl Child Network" lilikuwa likitoa mikopo kwa wanawake chini ya Mpango wa Maendeleo na Kuwezesha Jamii.

Kwa kuliona hili kama fursa pekee ya kujinasua na unyanyasaji wa majumbani, ambako nilidhani kumetokana na utegemezi wa kiuchumi kwa mume wangu, niliamua kuifuata GCN. Wafanyakazi wa shirika hilo walinipeleka kwa mwanamke anayeitwa Betty Makoni, wakati walipoona kesi yangu ilikuwa hatari sana kwa wao, kwa kuwa mume wangu alikuwa anatumia sana nguvu na hakufuata sheria.

Betty aliguswa sana na hadithi yangu na ya watoto wangu watatu, ambao waliishia mitaani wakati nilipokuwa najificha kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu katika nchi jirani ya Botswana. Hapo kabla, nilifuata mashirika kadhaa ya wanawake na watekelezaji wa sheria bila mafanikio na hivyo kupoteza matumaini. Hata ndugu zangu wa karibu waliogopa kunipatia hifadhi katika makazi yao. Lakini Betty alinipatia hifadhi katika eneo la kijijini la Mutasa.

Wakati naishi huko, mwanamke wa eneo hilo aliuawa kikatili na mume wake mbele ya macho ya watoto wake watatu; na kulikuwa na kesi ambazo hazikuripotiwa. Kwa msaada wa Betty nilipata hamasa kushawishi wanawake wengine waliopatwa na unyanyasaji wa majumbani kuanzisha kikundi cha kuwasaidia, ambacho kilitoa nafasi ya kuzungumza kuhusu matatizo yao wakiwa mbali na wanaume zao.

Matokeo yake ni kuongezeka kwa kasi kwa wanawake waliomiminika wakiwa na habari za kutisha kuhusu unyanyasaji. Wanawake walisafiri zaidi ya kilomita 30 wakiwa hawana viatu ili kuja kuelezea mizigo waliyokuwa nayo kwa miaka. Kitu kilichokua kikiumiza kwa wanawake hawa waliokuwa na matatizo ni kwamba hawakupatwa na unyanyasaji wa majumbani pekee lakini pia na watoto wao. Jambo la kusikitisha, watoto wao ni sababu kuu ambayo iliwafanya kunyamaza kimya bila kusema kitu katika uhusiano uliokuwa ukitishia maisha yao.

Mikutano hii ilibadili wanawake. Waligeuka kuwa wakimya na kuwa kikundi ambacho kilikuwa na nia ya kubadili maisha.

Katika moja ya mikutano yetu, tuligundua kuwa robo tatu ya wanawake hao katika kikundi, ambacho kilikuwa na wanachama zaidi ya 100, walikuwa wanaishi na VVU na kuwa karibu wanachama wote wako katika kazi za kutunza wagonjwa wa Ukimwi katika ngazi za chini au za kati. Ndipo tukakubaliana kuwa kila mpango ambao tutakwenda kutekeleza unatakiwa kuingiza suala la VVU/UKIMWI.

Swali: Kama mwakilishi wa watoaji huduma katika jamii na kama kiongozi wa "Groots Zimbabwe Home-Based Care Alliance", unaamini nini kinahitajika kuboresha upatikanaji wa teknolojia ya habari katika kuzuia VVU, ifikapo mwaka 2015?

Jibu: Kinachohitajika ni kuanzishwa kwa sera za makusudi katika ngazi ya kitaifa kupatia wanawake upatikanaji wa teknolojia ya habari inayostahili kueneza taarifa za VVU/UKIMWI. Kuanzisha vituo vya habari katika ngazi za vijijini na nje ya miji kungesaidia kuwapatia wanawake fursa ya kupata habari hizo. Watu pia wanapaswa kujikusanya katika vikundi na kutaka kutumia kompyuta na vifaa vingine vya TEHAMA.

Taarifa za VVU/UKIMWI zinatakiwa kukatiza katika makundi yote ya wanawake: kisiasa, kijamii, kiuchumi, kidini na kitamaduni. Elimu katika nchi yetu inapaswa kulenga katika kukuza maarifa ya kupata habari zinazofaa kukabiliana na VVU/UKIMWI, hasa katika maeneo ya vijijini ambako watu wenye elimu ni wachache.

Swali: Ni ujumbe gani unataka kufikisha kwa jumuiya ya kimataifa katika Siku ya Ukimwi Duniani?

Jibu: Wakati dunia ikikubali na kuamini kuwa VVU/UKIMMWI ni tatizo la wote, pia wanatakiwa kutambua kuwa baadhi ya makundi katika jamii yana nafasi kubwa ya kuupata ugonjwa huo kutokana na mazingira ya kijamii, kiuchumi na kitamaduni. Jinsi mtu anavyokuwa hana uwezo kitamaduni, kijamii na kiuchumi, ndivyo jinsi anavyokuwa rahisi kuambukizwa.

Kwa sasa dunia inapaswa kuelekeza nguvu katika kukabiliana na kukosekana kwa usawa kijamii katika misingi ya jinsia, kidini na kiuchumi ili kila mmoja awe na fursa sawa ya njia ambazo zinatumika kukabiliana na VVU/UKIMWI.

Swali: Je kuna uhusiano wa karibu kati ya VVU/UKIMWI na unyanyasaji wa majumbani nchini Zimbabwe?

Jibu: Ndiyo. Wanawake wenye VVU wana hatari kubwa ya kukabiliana na kila aina ya unyanyasaji wa majumbani. Hali inazidi kuwa mbaya wanapokuwa wagonjwa sana kwasababu waume zao wanawatelekeza au wanawarejesha kwa ndugu zao kupata matunzo huko au kusubiri kufa, lakini mara nyingi ndugu zao wasingependa kuwapokea.

Kwa kuongeza, wanawake wanalaumiwa mara nyingi kuwa ndiyo walioleta VVU nyumbani, kwa hiyo wanatelekezwa kabisa, wananyanyapawa, wanaachwa kwa nguvu na katika baadhi ya matukio wanatupiliwa mbali. Wanawake wenye VVU pia wanakabiliwa na unyanyasaji wanapojadili suala la ngono salama au kutumia kinga wanapojamiiana na wapenzi wao.

Suala la lishe kwa wanawake wenye VVU mara nyingi linasababisha mgogoro na kutokuelewana, jambo ambalo linapelekea unyanyasaji wa kupigwa, na uamuzi wao wa kuacha kuzaa watoto unasababisha kupigwa pia.

Swali: Nini kifanyike kusaidia wanawake kuwa na chaguo la kufanya ngono salama na kuvunja mila za kukubali tu ngono kutoka kwa wanaume?

Jibu: Maarifa huleta nguvu, kuwa na uwezo wa kujieleza na kujiamini. Ni muhimu kwa makusudi kabisa kuelekeza nguvu katika kupatia wanawake uwezo kupitia elimu ili wanawake waweze kukabiliana na matatizo yao kwa kujiamini. Kama wanawake hawatatambua haki zao, wataendelea na tatizo la kukubaliana na wanaume katika kutatua tatizo.

Kwa kuongeza, kutungwa kwa sera zinazotoa fursa sawa kijamii na kiuchumi bila kujali jinsia kutajenga nguvu ya kuzungumza ya wanawake. Wanaume wana faida ya kuwa na nguvu, lakini kama wanawake watapatiwa fursa sawa ya kuwa na nguvu hawatakubaliana na kila kitu wanachotaka wanaume. (END/2013)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The element 'html' is used but not declared in the DTD/Schema.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>