Inter Press Service News Agency
Friday, April 20, 2018   00:13 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions

Maswali na Majibu
Kukabiliana na Unyanyapaa Dhidi ya Ushoga Ni Muhimu Katika Vita Dhidi ya UKIMWI
Rebecca Hanser

UMOJA WA MATAIFA, Januari 3 (IPS) - Wakati jumuiya ya kimataifa inaungana Desemba 1 kuadhimisha Siku ya UKIMWI Duniani, taarifa mpya kutoka Shirika la Kupambana na UKIMWI la Umoja wa Mataifa inaonyesha kuwa wakati kuna mafanikio makubwa katika kuzuia na kutibu VVU/UKIMWI, unyanyapaa, matumizi ya nguvu na ubaguzi dhidi ya jumuiya ya mashoga unaendelea

Michael Ighodaro, mwanaharakati wa haki za mashoga hivi karibuni alikutwa na VVU/UKIMWI, ni mfano halisi wa ukiukwaji endelevu wa haki za binadamu katika taifa lake la Nigeria.

Baada ya kuvamiwa kikatili na kupigwa na nyumba yake alimokuwa akiishi kuchomwa moto, Ighodaro alilazimika kukimbilia nchini Marekani. Kwa sasa anaishi mjini New York na anaendelea kufanya kazi kama mwanaharakati kuhamasisha kuhusu kuendelea kwa ghasia dhidi ya mashoga.

"Nchini Nigeria, ni kama nilikuwa naishi kwa mashambulizi. Huwezi kutembea mitaani kama unavyotaka na huwezi kutangaza waziwazi kuwa wewe ni shoga," aliiambia IPS.

Ighodaro alizungumza na mwandishi wa IPS katika Umoja wa Mataifa Rebecca Hanser kuhusu maisha yake na harakati zake nchini Nigeria akiwa kama shoga mwenye VVU na kazi yake kama mwanaharakati wa haki za mashoga.

Sehemu ya mahojiano inafuata.

Swali: Kutokana na kuzaliwa nchini Nigeria, nchi inayojulikana kwa kukosekana kwa uvumilivu kwa ushoga, unaweza kuelezea miaka yako ya ujana na imezekanaje kuweza kuishi katika mazingira haya?

Jibu: Niligundua kuwa mimi ni shoga nilipokuwa na miaka saba tu. Mama yangu aligundua nilikuwa tofauti na kaka zangu na dada zangu na alidhani nilikuwa mgonjwa hivyo alinipeleka kanisani na kwa waganga wa kienyeji ili kujua nilikuwa nasumbuliwa na nini.

Walipokuja kufahamu kuwa nilikuwa shoga, nilikuwa sijui hiyo ilikuwa ina maana gani, kwasababu nilikuwa bado mdogo sana. Mama alisema kuwa nilikuwa na mapepo na ilibidi nipatiwe tiba, na hivyo kunifanya kuamini ni jambo baya kuwa shoga na nilianza kuwa na hofu kulizungumzia jambo hilo.

Hata hivyo, haikunizuia nisiwe ambaye nilitakiwa kuwa. Katika umri wa miaka kumi na saba nilikuwa nimeanza kutongozana na wanaume. Wazazi wangu hawakunivumilia tena na hivyo walinifukuza niondoke nyumbani. Baba hakutaka kunilipia ada ya shule tena hivyo ilibidi niache shule ya sekondari. Katika umri kama huo, ilikuwa vigumu kuishi bila familia au makazi au marafiki. Nilikuwa na marafiki zangu mashoga tu, na hata hivyo nilikuwa mpweke sana.

Swali: Maisha yako yalifananaje nchini Nigeria baada ya kuondoka nyumbani kwenu?

Jibu: Wakati nilipoondoka nyumbani nilihisi kuwa huru na kufanya kila kitu nilichotaka. Nilikuwa na maisha ya kufanya ngono kwa kiasi kikubwa na hivyo kunipatia mawazo ya ukombozi na hatimaye kuanza kujitangaza. Kwa bahati mbaya, wakati huo sikujua chochote kuhusu matumizi ya kondomu, vilainishi au ngono salama. Mambo yangekuwa tofauti kama ningekuwa na taarifa za kutosha au elimu.

Nilijigundua kuwa na VVU nikiwa na umri wa miaka 23. Huo pia ni wakati ambapo niligundua kilichowaua baadhi ya marafiki zangu mashoga wa karibu nchini Nigeria. Jambo hilo liliniumiza sana na kuniamsha.

Nchini Nigeria, ilikuwa kama naishi na ghasia. Katika mitaa huwezi kutembea na huwezi kuzungumzia ushoga waziwazi. Unatakiwa kusema ukweli kama unataka kupata kitu. Lakini nchini Nigeria unatakiwa kuzungumza kwa kuzunguka sana hadi wakati mwingine unaanza kuamini uongo wako.

Swali: Kuna mafanikio yamepatikana katika kuzuia VVU, lakini unyanyapaa na matumizi ya nguvu na ubaguzi unaendelea. Una mawazo gani katika hali kama hii?

Jibu: Watu mashoga siyo tu kwamba wananyanyapawa barani Afrika lakini katika dunia nzima. Hali mbaya zaidi inatokana na kwamba tunanyanyapawa hata katika jamii zetu wenyewe. Katika jumuiya ya mashoga, wanachama wanapambana zaidi kuwa na sheria za ushoga, kupambana na haki za mashoga na mikakati ya kuzuia maambukizi ya VVU, lakini kwa kiasi wanawasahau mashoga wanaoishi na VVU.

Wanashindwa kuzungumza kinagaubaga juu ya mashoga wenye VVU, kwasababu unapaswa kukumbuka kuwa mtu shoga anayeishi na VVU ni tofauti na shoga ambaye hana VVU. Haya ni mambo mawili tofauti.

Swali: Wewe pia ni mwanaharakati maarufu wa haki za mashoga katika Afrika na sasa hapa katika Umoja wa Mataifa. Ni ujumbe gani unautoa kupitia kazi yako?

Jibu: Kuna mashirika mengi ninayofanyia kazi, hata katika Afrika, kama vile ICARE, ambalo linasaidiwa na shirika la Haki ya Afya na Kujamiiana kwa Wanaume wa Afrika (AMSHR). Pia hivi karibuni nilianzisha shirika hapa Marekani linalojulikana kama "African MSM Plus". Linajikita katika kutoa ushauri nasaha na kusaidia wanaume mashoga wenye VVU.

Mimi pia ni mpiga debe wa shirika la IRM. IRMA ni shirika linalofanya kazi ya utafiti wa vimelea vinavyowapata watu wanaoshiriki ngono kinyume cha maumbile. Katika Afrika mimi pia nashiriki katika mpango wa watu wanaofanya ngono za jinsia tofauti unaojulikana kama Mind Builders.

Kwa bahati mbaya, mashirika haya katika bara la Afrika yanapaswa kufanya kazi ya "msingi" kwasababu hakuna uvumilivu kwa vituo vya jamii za mashoga. Inabidi tujifiche, jambo ambalo ni vigumu kwasababu pia tunafanya kazi ya kutembeleana. Lakini tunafanya kazi hii kwasababu ni muhimu. Hatukupaswa kuangalia tu changamoto za mbeleni kwetu badala ya kuangalia mafanikio yetu.

Ujumbe wangu ni mfupi na wenye nguvu: bakia kuwa wewe, kwasababu huwezi kuwazuia watu kufikiria tofauti.

Swali: Katika suala la matumizi ya nguvu na ubaguzi, nini ni kitu kibaya zaidi ambacho kimejitokeza kwako?

Jibu: Usiku ule ambao nilipigwa na kushambuliwa – naukumbuka kichwani mwangu. Kila ninapofunga macho yangu, naweza kuona watu ambao walinifanyia hilo. Najaribu kusahau, lakini kila usiku nikiwa usingizini nawaona mbele yangu, wakinitukana. Inaumiza, lakini ni jambo ambalo inabidi kuishi nalo katika maisha yangu yote. (END/2013)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The element 'html' is used but not declared in the DTD/Schema.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>