Inter Press Service News Agency
Thursday, June 21, 2018   09:54 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions

Maswali na Majibu
Jinsi Ufadhili wa Kiubunifu Unavyokabiliana na VVU/UKIMWI
Julia Kallas

UMOJA WA MATAIFA, Januari 3 (IPS) - Katika Siku ya Ukimwi Duniani, ukweli kwamba idadi ya watoto wanaoambukizwa VVU inazidi kupungua ni habari njema kwa UNITAID, Mfuko wa Manunuzi ya Madawa uliopo chini ya Shirika la Fedha Duniani. Lakini UNITAID inatambua pia kuwa ina kazi kiasi gani kuhudumia watoto ambao tayari wameshaambukizwa na ugonjwa huo. Philippe Douste-Blazy, wa Ufaransa, ni mshauri maalum ambaye anaikuza UNITAID na vyanzo vingine vya ufadhili wa kiubunifu kwa ajili ya kufikia Malengo ya Maendeleo ya Milenia ya Umoja wa Mataifa(MDGs).

"Kuna baadhi ya mafanikio yamefikiwa lakini bado kuna kazi kubwa ya kufanywa na jumuiya ya kimataifa,'' Douste-Blazy aliiambia IPS akizungumzia juu ya mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI. "Kwa bahati mbaya hatuna fedha za kutosha kufikia MDGs ifikapo mwaka 2015,'' aliongeza.

Douste-Blazy aliongea na mwandishi wa IPS katika Umoja wa Mataifa Julia Kallas kuhusu maendeleo ambayo yamepatikana katika kuzuia maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto lakini pia juu ya ni jinsi gani jumuiya ya kimataifa inaendelea kutoa tiba ya VVU kwa watoto katika nchi zinazoendelea. Sehemu ya mahojiano inafuata.

Swali: Hali ya ufadhili wa tiba ya VVU kwa watoto katika nchi zinazoendelea ikoje kwa sasa?

Jibu: Watoto wapatao milioni 3.3 wanaishi na VVU leo hii. Kwa bahati mbaya hatuna fedha za kutosha kufikia Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs) kwa ujumla wake na hasa malengo yanayohusiana na afya – VVU, kifua kikuu na malaria.

Ni lazima kutafuta ufadhili kwa sasa kwasababu kwa hali ya kiuchumi ya sasa, tutaona kupungua kwa kiasi kikubwa kwa misaada ya maendeleo (ODA). Itakuwa vigumu kwa nchi zote kusaidia. Hatuwezi kuomba serikali ya Ugiriki, kwa mfano, kuchangia dola bilioni 3 kwa ajili ya nchi zinazoendelea kwasababu tunaona ongezeko la umaskini miongoni mwa wananchi wao wenyewe. Hivyo tutakuja kuona ongezeko la vifo vya watoto wadogo.

Inabidi kujenga ufadhili wa kiubunifu kwa ajili ya maendeleo. Kwa mfano, UNITAID imeweka kodi ndogo katika tiketi za ndege. Ufadhili wa namna hii unasaidia kukabiliana na VVU miongoni mwa watoto.

Ni mara chache sana watoto wanaweza kuzaliwa wakiwa na VVU katika nchi zilizoendelea kwasababu mama wanaoishi na VVU wanapatiwa tiba wakati wa ujauzito ambayo inahakikisha kuwa watoto wao wanazaliwa wakiwa hawana VVU. Hata hivyo, bado watoto zaidi ya 1,000 wanazaliwa wakiwa na VVU kila siku – ambapo asilimia 99 wanatoka bara la Afrika na ni asilimia 28 tu wanapatiwa tiba.

Tumetathmini ni makampuni gani yalivutiwa na kuzalisha madawa ya kupunguza makali. Ufadhili wetu wa muda mrefu ulipatia wasambazaji motisha kutengeneza madawa ambayo ni rafiki kwa watoto na hivyo tukaweza kununua madawa hayo kwa kipindi cha miaka mitano. Wasambazaji wengi wa madawa yanayotengenezwa kwa ruhusa kutoka kwa makampuni ya asili waliingia katika soko na hivyo kushusha bei ya vidonge kwa asilimia 70.

Kabla ya hapo, hakuna mtoto aliyetibiwa na madawa ya kurefusha maisha ambayo ni ya vipindi maalum, lakini kwa kutumia madawa ya watu wazima, ambayo walitumia mara 18 kwa siku. Lakini sasa wanatumia vidonge viwili tu kwa siku, watoto wanaweza kutibika.

Swali: Siku ya Ukimwi Duniani ni Desemba 1. Je tunapaswa kusherehekea mafanikio makubwa?

Jibu: Ndiyo. Tunaweza kuona kumekuwepo na baadhi ya mafanikio, lakini bado kuna kazi kubwa ya kufanywa na jumuiya ya kimataifa. Kwa mara ya kwanza zaidi ya asilimia 50 ya wagonjwa milioni 15 ambao wanahitaji madawa ya kurefusha maisha wanayapata.

Ni mafanikio makubwa pia kwamba tuna maambukizi milioni 7 ya VVU ambayo yamepungua duniani, hasa katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara. Kwa bahati mbaya katika Ulaya Mashariki, katika nchi za Russia na Indonesia, maambukizi yanaongezeka.

Swali: Unaweza kuzungumzia juu ya manedeleo ya dozi ya mseto ya tatu – kwa – moja katika kukabiliana na UKIMWI kwa watoto?

Jibu: Tangu kuundwa kwake UNITAID imekuwa ikifanya kazi ya kukabiliana na VVU kwa watoto kwa kujenga soko la madawa bora ya kupambana na VVU kwa watoto. Kabla ya hapo, hakukuwa na motisha kwa makampuni ya madawa kuwekeza katika madawa yanayofaa kwa watoto. Tiba ya VVU kwa watoto katika nchi za kipato cha chini ilikuwa imeandaliwa kwa watu wazima – ambayo ilienda hadi dozi 18 kwa siku.

Kwa hiyo dawa ya mseto ya dozi tatu-kwa moja ya kupambana na UKIMWI kwa watoto ni ugunduzi mkubwa sana, kutoka dozi 18 kwa siku hadi vidonge viwili kwa siku. Ni mafanikio makubwa. Kila mwaka UNITAID inafadhili tiba kwa zaidi ya watu 100,000. Na sasa ni wakati wa kufuatilia kazi zetu za kukabiliana na VVU kwa watoto.

Swali: Je ajenda ya maendeleo endelevu baada ya mwaka 2015 inapaswa kuzungumzia nini kuhusu VVU/UKIMWI, na ni nini kinatakiwa kufanyika kuleta ufanisi zaidi?

Jibu: Hatuwezi kuendelea kama hatuna fedha. Kila mkuu wa nchi, mkuu wa serikali au mbunge anasema tutakuja kufikia malengo ya MDGs. Siyo kweli.

Ili kukabiliana na VVU tunahitaji mambo matatu. Kwanza kuzuia. Tunahitaji kusaidia kuzuia miongoni mwa watu walioko katika hatari kubwa ya kuambukizwa kama vile makahaba na watu wanaofanya mapenzi ya jinsia moja wasiweze kuambukizwa. Pili, lazima kuhakikisha kuwa kuna upatikanaji wa tiba kwa wote. Ni asilimia 54 tu ya watu wazima na asilimia 28 ya watoto wadogo wanapata tiba leo hii.

Mwisho, tunahitaji kutafuta pesa kufikia malengo ya MDGs – tunahitaji ufadhili wa kiubunifu zaidi. Kwa kutumia UNITAID, tumethibitisha kuwa hili linawezekana.

Swali: Unaweza kuzungumzia zaidi kuhusu kodi ya dola moja kwenye ndege ambayo ilibuniwa na wewe mwenyewe, rais wa zamani wa Brazili Lula na rais wa zamani wa Ufaransa Chirac? Nini kinahitajika kuwezesha nchi nyingi zaidi kushiriki katika mradi huu?

Jibu: Mfumo wa ufadhili wa UNITAID unajikita katika kodi ya mshikamano ya tiketi ya ndege. Kila Mmarekani ambaye anasafiri kwenda Ufaransa analipia dola moja zaidi kusaidia mpango huu. Jambo hilo linatumika katika nchi nyingine 15. Katika kipindi cha miaka mitano tulikusanya dola bilioni 2.5, na ni ufadhili ambao unatabirika na endelevu.

Kwa msafiri, hasikii maumivu – watu ambao wana uwezo wa kulipia tiketi ya ndege wanaweza kutoa dola moja zaidi kwa urahisi mkubwa. Hata haifikii bei ya kikombe cha kahawa. Kwa ufadhili huu tunasaidia kukabiliana na VVU kwa watoto wachanga. Watoto nane kati ya 10 wanatibiwa kutokana na mfumo huu. Tunafanya kazi kushawishi nchi nyingi zaidi kuwa sehemu ya mpango huu. (END/2013)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The element 'html' is used but not declared in the DTD/Schema.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>