Inter Press Service News Agency
Sunday, September 22, 2019   19:40 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions


TANZANIA – Mradi wa Pwani Wainua Maisha ya Wanawake Pangani na Bagamoyo
Na Marko Gideon

PANGANI, Desemba 5 (IPS) - Hali ya maisha ya wanawake katika vijiji kadhaa vya Pangani na Bagamoyo katika mwambao wa Bahari ya Hindi imeboreka kutokana na utekelezaji wa miaka mitatu wa mradi wa kuhifadhi mazingira ya Pwani (TCMP-Pwani).

Wakizungumza nyakati tofauti wakati wa ziara za ufuatialiaji wa shughuli za mradi huo katika wilaya hizo, wanawake mbalimbali kutoka vikundi vya kuweka na kukopa (Saccos), vikundi vya ufugaji wa nyuki, vikundi vya biashara, n.k. wamesema sasa wana uwezo mkubwa wa kusaidia familia zao kupitia shughuli zinazofadhiliwa na mradi huo.

Kwa mujibu wa taarifa ya hivi karibuni iliyotolewa katika kijiji cha Mkalamo juu ya maendeleo ya wananchi yaliyochangiwa na mradi wa TCMP-Pwani unaofadhiliwa na Shirika la Misaada ya Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) na kupata msaada wa kiufundi kutoka Chuo Kikuu cha Kisiwa cha Rhode, kuna jumla ya vikundi 18 vinavyoendesha shughuli za maendeleo katika kijiji hicho na vijiji vya jirani, ambavyo kwa pamoja huunganishwa na Saccos.

Vikundi hivyo ni pamoja na vikundi vya ufugaji wa ng’ombe, uelimishaji rika, ufugaji wa kuku, kilimo, ufugaji wa nyuki, ufugaji wa mbuzi na kikundu cha uhamasishaji wa matumizi ya majiko banifu.

Vikundi hivyo hupata mtaji wa kuendeshea shughuli zake kutoka Saccos ambayo ilianzishwa kwa msaada kutoka mradi wa Pwani ili kuanzisha shughuli mbadala ambazo zinaweza kutunza mazingira. Pia mradi hutoa mafunzo ya ujasiriamali ya jinsi ya kuendesha shughuli hizo endelevu na zisizoharibu mazingira kwa wanavikundi.

Suala la kipekee katika mradi huo, hata hivyo, ni kuona kuwa idadi kubwa ya wanaofaidika ni wanawake, jambo ambalo ni zuri katika kuleta maendeleo ya kibinadamu kwa familia za vijijini.

"Kutambuliwa kwa jukumu la wanawake katika maendeleo ya jamii za vijijini ni muhimu kwa maendeleo ya jamii hizo katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara," inasema ripoti ya Kituo cha Kiufundi katika Kilimo na Ushirikiano Vijijini (CTA). "Kutambua na kuunga mkono jukumu hili ni muhimu kwa maendeleo siyo ya wanawake tu na pia maendeleo ya kiuchumi katika maeneo ya vijijini." Umuhimu wa jukumu la wanawake kuleta maendeleo vijijini na hata kitaifa unatambuliwa pia na mashirika mengine ya kimataifa. "Tunajua, kutokana na tafiti za idadi ya watu, kuwa wakati wanawake wanapopata pesa, wana uwezo mkubwa wa kutumia katika chakula cha familia ikilinganishwa na wanaume," Carlos Seré, Mkuu wa Kuendeleza Mikakati katika Shirika la Kimataifa la Maendeleo ya Kilimo (IFAD), alisema hivi karibuni. Anaongeza, "wanawake wa kijijini wanapokuwa na uwezo wa kiuchumi na kijamii, wanakuwa nguvu muhimu ya kuleta mabadiliko".

Mabadiliko yanayosemwa na ofisa wa IFAD yanaonekana wazi katika kijiji cha Kwakibuyu, kitongozji cha Sakura wilayani Pangani ambapo mama Fidea Haule anajivunia kuleta mabadiliko katika familia yake kutokana na kupata mikopo kadhaa kutoka Saccos.

"Mimi ni mama wa watoto wanne. Nimekuwa nikikopa kutoka Saccos kuendeleza elimu ya watoto wangu toka wanaanza shule hadi sasa wengine wako Chuo Kikuu," anasema mama Haule.

Anasema kabla hajajiunga na Saccos alikuwa mkulima mdogo mdogo ambaye aliwalea watoto wake kwa shida kwa kutegemea kilimo cha mihogo, mahindi na ufuta na kipato kidogo cha mume wake ambaye ana mashine ya kushona nguo.

Lakini baada ya kuwa na fursa ya kukopa kutoka Saccos ameweza kupanua shughuli zake za kilimo hadi kufikia ekari 12, ameweza pia kujikita katika ufugaji wa nyuki ambapo ana uwezo wa kuvuna zaidi ya lita 200 katika kila msimu wa mavuno. Lita moja ya asali kwa sasa inauzwa shs 8000 kijijini hapo.

"Kutokana na shughuli hizi nimeweza kuongeza mtaji wangu katika Saccos kiasi kwamba naweza kukopa wakati wowote kiasi ambacho kinaweza kusaidia familia," anasema.

Anasema anakumbuka mkopo wa mwisho kukopa ni wa shs 900,000 ambao aliutumia kumnunulia mtoto wake anayesoma Uhandisi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kompyuta ndogo aina ya laptop kwa ajili ya kuendelea vizuri na masomo yake.

Mama Haule pia hutumia pesa anazopata kutokana na Saccos kununulia watoto wake wengine sare za shule na kuwalipia ada na matumizi mengine ya nyumbani. Hadi sasa watoto wake watatu kati ya wanne wana ngazi ya elimu ya juu na mmoja bado yupo sekondari.

Saccos ya Sakura ambayo hujulikana kama "Songambele" ilianzishwa Januari mwaka 2008 ikiwa na wanachama 20 na mtaji wa sh. 200,000 ikiwa ni hisa shilingi 140,000 na michango shilingi 60,000.

Hadi kufikia Juni mwaka huo, Saccos ilikuwa imeshafikia wanachama 44 huku idadi ya wanawake na wanaume ikilingana. Mtaji pia ulifikia zaidi ya 600,000. Ni mwezi huo ambapo mradi wa Pwani ulisaidia kujasiliwa kwa Saccos na kuiongozea mtaji wa shs 1,000,000 na kuingia nao mkataba wa kuanzisha shughuli za utunzaji wa mazingira.

Hadi sasa Saccos imeshatoa mikopo 202 yenye thamani ya shs 87,000,000 ambayo imefaidisha wanawake 30.

Saccos ya "Tunza Mazingira" ya kijiji cha Ushongo kata ya Mwera wilayani Pangani nayo ina historia ya kufaidisha wanawake. Ikiwa imeanzishwa Januari 2012 na kuwa na mtaji wa zaidi ya shs 2,500,000 imeshatoa mikopo kwa wanawake 13 na wanaume 3 tu. Wanawake waliokopa katika Saccos hiyo huendesha shughuli mbalimbali za kujiingizia kipato ikiwa ni pamoja na kilimo cha mwani, uchuuzi wa samaki, mama lishe, ususi na kulipia ada watoto wao wanaokwenda shule.

Katika Saccos ya Mkalamo, jumla ya wanawake 14 wamefaidika na mikopo yenye thamani ya zaidi ya shs 8,000,000 huku wanawake 17 wakiwa miongoni wa wanachama waliofadika na mikopo yenye thamani ya shs 11,000,000 katika Saccos ya kijiji cha Saadani wilayani Bagamoyo.

Saccos ya UWAMKE (Umoja wa Wanawake Mkange) katika wilaya ya Bagamoyo ilianza Juni 2011 na hadi sasa ina jumla ya wanachama 69 ambapo kati ya hao, wanawake ni 63 na wanaume 6. Hadi sasa idadi hiyo kubwa ya wanawake imeshafaidika na mikopo yenye thamani ya zaidi ya shs 9,000,000.

"Saccos ni mkombozi wa kweli wa wanawake vijijini. Haya nayaona kama mafanikio mengi na makubwa katika maisha yangu. Nimeshakopa mara nyingi na naendelea kukopa. Nimesomesha watoto hadi wamefikia Chuo Kikuu. Nashukuru sana kwa faida kubwa niliyopata," anasema mama Haule. (END/2012)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The download of the specified resource has failed.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>