Inter Press Service News Agency
Wednesday, April 25, 2018   23:30 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions


Ethiopia Yakandamiza Mashirika ya Haki za Binadamu
Ed McKenna

ADDIS ABABA, Desemba 4 (IPS) - Dunia ilipata dalili za kuchanganya mambo juu ya rikodi ya haki za binadamu ya Ethiopia wakati ilipochaguliwa wiki hiyo hiyo kuingia katika Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa huku shirika kubwa la misaada la Ujerumani likifunga ofisi yake likipinga mazingira kandamizi ya kisiasa."Kama kuhitimu kuingia katika UNHRC ni rikodi ya haki za binadamu ya nchi hiyo – basi Ethiopia isingefaa kuteuliwa …. Mazingira ya haki za binadamu nchini yanatisha," Endalkachew Molla, mkurugenzi wa Baraza la Haki za Binadamu(HRCO), ambalo limedumu kwa miaka mingi nchini Ethiopia aliiambia IPS.

Ethiopia, pamoja na nchi nyingine nne za Afrika - Kenya, Gabon, Côte d'Ivoire na Sierra Leone – zilichaguliwa Nov. 12 kuwa wanachama wa UNHRC kwa miaka mitatu kuanzia Jan. 1, 2013.

Katika wiki hiyo, moja ya mashirika makubwa ya kiraia yanayopigania haki za binadamu ya Ujerumani, Heinrich Böll Foundation (HBF), liliamua kufunga ofisi yake likipinga vikwazo dhidi ya haki za binadamu katika taifa hilo la Pembe ya Afrika. Kufungwa kwa shirika hilo kumeweka historia ya kuwahi kufungwa kwa shirika kubwa kama hilo nchini Ethiopia.

Likiwa na jina la mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel ambaye ni raia wa Ujerumani, Heinrich Böll Foundation ni NGO ambayo inakuza demokrasia na haki za binadamu, ikiwa na ofisi katika nchi 30 duniani.

"Lengo letu la kufanya kazi pamoja na washirika wa ndani kukuza demokrasia, usawa wa kijinsia na maendeleo endelevu, haliwezi kufikiwa tena. Kufungwa kwa ofisi ya Ethiopia ni ishara ya kupinga dhidi ya kukiukwa kwa haki za kiraia na uhuru wa kujieleza," alisema Barbara Unmüßig, mkurugenzi wa HBF, katika taarifa yake ya Nov. 7.

Unmüßig alikuwa akimaanisha sheria tata ya NGO iliyopitishwa mwaka 2009 inayojulikana kama "Charities and Societies Proclamation".

Sheria hii inaweka vizuizi vya kufanya kazi, kuendesha na kufadhiliwa kwa mashirika ya haki za binadamu nchini Ethiopia. Inazuia shirika lolote lile la haki za binadamu kupokea ufadhili wa zaidi ya asilimia 10 kutoka kwa vyanzo vya kigeni.

Kutokana na sheria hii, ofisi ya HBF, ambayo ilifunguliwa mwaka 2006, ililazimika kupunguza malengo yake katika kipindi cha miaka mitatu kutoka kukuza demokrasia na usawa wa kijinsia na kufanya zaidi kazi za mazingira ili kuendana na sheria mpya, kwa mujibu wa mkurugenzi mkazi Patrick Berg.

"Tuliruhusiwa kutoa mafunzo ya ufumaji kwa wanawake, lakini hatukuruhusiwa kuwasaidia kudai haki zao za kikatiba. Lengo letu ni kuhamasisha mjadala wa kisiasa unaohusisha wote – lakini sheria ya sasa inafanya jambo hilo kushindikana," Berg aliiambia IPS.

Kwa kuongeza, mwongozo wa karibuni juu ya sheria hiyo unasema kuwa kiasi cha juu cha asilimia 30 cha bajeti ya NGO kinaweza kutumika katika gharama za kiutawala. Berg alisoma maana ya gharama za utawala ni nini na alishangazwa kugundua kuwa fasili yake ilikuwa ya undani zaidi ya kile ambacho kingeweza kugharamiwa na shirika lake.

"Ghafla, kazi yetu ya kuzalisha na kusambaza taarifa na kutoa nafasi ya mjadala wa umma inaonekana kama kazi ya kiutawala. Hakuna jinsi ya kuendana na sheria hizi bila ya kubadili sisi ni akina nani. Hatuko tayari kufanya hilo," Berg alisema.

Mwaka 2009 HBF ilikubali kufanya kazi chini ya vikwazo vya sheria hiyo ikiwa na matumaini kuwa mapatano yangefikiwa na serikali ya Ethiopia kurejesha hali kama ilivyokuwa zamani. Hata hivyo, baada ya miaka mitatu ya mazungumzo yasiyokuwa na matunda, shirika hilo hatimaye liliamua kufunga ofisi.

Sheria ya "Charities and Societies Proclamation" imekuwa mbaya mno kwa kuipatia serikali mwanya wa kuingilia, kuchunguza na kushiriki moja kwa moja katika usimamiaji na uendeshaji wa mashirika.

Kwa sasa kuna mashirika ya kiraia ya kimataifa karibu 3,000, na 400 kati ya haya yameshapewa onyo juu ya kuendesha shughuli zao kinyume na taratibu na kanuni za sheria hiyo.

Umuhimu wa kulinda haki za binadamu katika nchi kama Ethiopia ulisisitizwa na naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Eliasson, ambaye aliiambia IPS kuwa "nguzo nne muhimu za kipindi cha baada ya 2015 ya MDG ni amani duniani, maendeleo, utawala wa sheria na haki za binadamu; kama moja kati ya hisi nguzo itakuwa dhaifu mfumo mzima utakuwa dhaifu."

Msemaji wa serikali ya Ethiopia Bereket Simon alielezea IPS kuwa "lengo la sheria ya NGO ni kupunguza mambo ya nchi kuingiliwa na wageni, kuwezesha wananchi kushiriki katika maisha yao ya kisiasa." Kwa mujibu wa Bereket, uteuzi wa karibuni wa kuingia kwenye UNHRC "unaipatia serikali nguvu zaidi ya kuendeleza demokrasia na haki za binadamu Ethiopia."

Hata hivyo, Endalkachew ana imani kuwa kuzuia ushiriki wa mashirika ya haki za binadamu ya kigeni kunajenga mazingira ambayo hayaendani na Tamko la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa la mwaka 1948.

"Haki za binadmau hazina mipaka, ni za kila mtu. Ni ajenda ya binadamu wote. Ni kwa nini haki za binadamu nchini Ethiopia zisiwe na utaratibu kama huo usiokuwa na mipaka kama ilivyo kwa rasilimali kama kilimo na miundombinu?" aliuliza.

HRCO na shirika linaloongoza kupigania haki za wanawake la Ethiopian Women Lawyers Association (EWLA) – walifungiwa akaunti zao za benki Desemba mwaka 2009 baada ya kupata kiwango cha pesa kinachozidi kile cha sheria ya "Charities and Societies Proclamation", pamoja na ukweli kwamba fedha zake zote za kigeni zilipatikana kabla ya kupitishwa kwa sheria mwaka 2009.

EWLA imeshatoa misaada ya sheria ya bure kwa zaidi ya wanawake 17,000. Mwaka 2011, lilisitisha rasmi shughuli zake.

Oktoba mwaka huu, mashirika ya Amnesty International na Human Rights Watch yalipinga uamuzi wa mahakama kuu ya Ethiopia kukubali kuzuiliwa kwa mali zenye thamani ya dola 500,000 za HRCO.

Uwezo wa kuendesha shughuli wa HRCO umeshapunguzwa kwa kiasi kikubwa tangu sheria hiyo mwaka 2009. Wamepunguza matawi yao kutoka 12 hadi matatu, kutoka wafanyakazi 60 hadi 12 na ilibidi kufunga ofisi kadhaa nchini humo. Wigo wa kutoa misaada ya sheria kwa waathirika wa haki za binadamu umekandamizwa kabisa.

"Tunaweza kuendelea kuwa shirika la haki za binadamu lakini lisilokuwa na rasilimali," Endalkachew alisema.

Kwa mujibu wa Endelkachew, kuzorota kwa haki za binadmau nchini kunatokana na ghasia zinazotokana na chaguzi za mwaka 2005, wakati idadi kubwa ya watu walipigia kura upinzani.

"Machoni mwa chama tawala NGOs nyingi na waandishi wa habari walionekana kama kusaidia upinzani, hivyo waliamini kuwa lazima wafanye kitu kuzuia shughuli zao."

Baada ya matukio haya, serikali ilianzisha sheria ikiwa ni pamoja na ile ya 2009 ya "Charities and Societies Proclamation".

Kama sababu ya kuiteua Ethiopia kuingia katika UNHRC ni kuhamasisha serikali mpya kuboresha rikodi zake za haki za binadamu chini ya uangalizi wa jumuiya ya kimataifa hapo Enadalkachew anaamini "kuna sababu ya kuwa na matumaini kuhusu mustakabali wa baadaye wa haki za binadamu nchini Ethiopia." (END/2012)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The element 'html' is used but not declared in the DTD/Schema.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>