Inter Press Service News Agency
Tuesday, May 22, 2018   11:03 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions


Pamoja na Umaskini Visiwa vya Pasifiki Vyapata Mafanikio ya Kuzuia Vifo vya Watoto
Na Catherine Wilson

BRISBANE, Desemba 3 (IPS) - Visiwa vilivyopo katika Bahari ya Pasifiki vinapata mafanikio ya haraka katika kupunguza vifo vya watoto wachanga, pamoja na kuwa vingi kati ya visiwa hivyo vinakabiliwa na kazi kubwa ya kutokomeza umaskini na kuongeza ajira miongoni mwa vijana na idadi ya watu inayoongezeka kwa kasi.

Huku ikiwa imebakia miaka mitatu kufikia Malengo ya Maendeleo ya Milenia ya Umoja wa Mataifa (MDGs), mafanikio yanaonekana kuanza kupungua katika ukanda huo, kwa mujibu wa ripoti ya Jukwaa la Visiwa vya Pasifiki linalojulikana kwa kifupi chake cha Kiingereza kama (PIF), kikundi cha kikanda.

Habari njema, kwa mujibu wa ripoti ya PIF, ni kuwa kati ya mataifa 10 nje ya 14 katika visiwa hivyo ambayo yalifanyiwa utafiti, ikiwa ni pamoja na Vanuatu, Visiwa vya Marshall, Visiwa vya Cook na Tonga, yanapata mafanikio katika lengo namba nne (MDG4) ambalo linataka kupunguza vifo vya watoto wachanga.

Kuna mafanikio yanayotofautiana duniani kote katika kufikia malengo la MDGs, ambayo yalikubaliwa katika Tamko la Milenia la Umoja wa Mataifa la mwaka 2000 ambalo lilikubali kuufanya ‘utandawazi kushirikisha kikamilifu watu wote duniani pamoja na kuwa wa usawa.’

Ripoti ya Kikanda ya Mwaka 2012 kuhusu Ufuatiliaji wa MDG inakuja miaka mitatu baada ya nchi wanachama wa PIF kusaini mkataba wa kuimarisha uratibu wa rasilimali kuongeza mafanikio ya kimaendeleo.

Mafanikio na changamoto za muda mrefu ni ushahidi katika ngazi ya kanda hiyo. Melanesia, kisiwa chanye idadi kubwa ya wakazi katika wastani wa idadi ya watu zaidi ya milioni mbili, ambacho kinamilikiwa na taifa la Papua New Guinea (PNG), iko nyuma kufikia malengo. Kwa kulinganisha, Polynesia, ambayo inahusisha visiwa vya Cook, Niue, Samoa, Tonga na Tuvalu, ambayo ina wastani wa wakazi 62,000, iko katika nafasi ya kufikia malengo manne.

Visiwa vya Cook na Niue ni mataifa pekee ambayo yana uwezekano wa kufikia malengo yote nane ya MDGs.

Lengo namba moja (MDG 1) ambalo linataka kupunguza nusu ya idadi ya watu wanaoishi katika umaskini uliokithiri ifikapo mwaka 2015, linaonekana kuwa changamoto kubwa kwa ncho zote za ukanda wa Pasifiki.

Katika PNG, wastani wa asilimia 28 ya wakazi milioni saba wanaishi chini ya mstari wa umaskini, na hivyo kuonyesha kuwa hali imeboreka kwa kati ya asilimia tano hadi 10 tangu mwaka 1990. Sababu za msingi ni pamoja na wakazi kuishi maeneo ya ndanindani sana katika maeneo ya vijijini, rushwa, kiwango cha juu cha ghasia na janga la VVU.

Baadhi ya asilimia 23 ya wakazi wa kisiwa cha Tonga wanaishi chini ya mstari wa umaskini na familia kukabiliwa na ongezeko la ugumu wa maisha kutokana na madhara ya mtikisiko wa kifedha duniani, ukuaji mdogo wa kiuchumi na mfumuko wa bei.

Pia kuna tofauti katika ngazi ya kitaifa huku jamii za vijijini zikikabiliwa na kiwango cha juu cha umaskini katika mataifa ya Fiji, Palau, Samoa na Tonga, wakati kuna idadi kubwa ya idadi ya maskini mijini katika visiwa vya Solomon, Kiribati, Tuvalu na Vanuatu.

Umaskini siyo rahisi kupata fasili katika Visiwa vya Pasifiki ambako kiwango cha kipimo cha kipato cha chini ya dola moja kwa siku kinaweza kisiwe sahihi. Jamii za Pasifiki zina historia ndefu ya kuendesha kilimo cha kujikimu, kujitosheleza na kuwa na imani kubwa ya uwajibikaji katika ngazi ya familia ya ndugu wengi na jamii ambayo inaweza kufikia mahitaji ya wale wasiojiweza. Lakini hata katika vijiji, karne za desturi zinabadilika kwa kiwango tofauti hasa kutokana na madhara ya uchumi wa kifedha, kuongezeka kwa kasi kwa ukuaji wa miji na shinikizo la kitamaduni na kuingia kwa ustaarabu wa kisasa.

Albert Cerelala, ofisa programu wa "Foundation of the Peoples of the South Pacific", asasi isiyokuwa ya kiserikali ya nchini Fiji, anaelezea umaskini kama "kukosekana kwa uwezo wa mtu na familia yake kufikia mahitaji ya lazima na kuishi katika maisha ya afya. Hii inaweza kuwa na maana kuwa wanakosa uwezo wa kuweka chakula mezani kutokana na sababu yoyote ile au wananyimwa fursa za kijamii na za kiuchumi."

"Inaweza pia kuwa wanakosa hisia za kujitambua wenyewe (katika ardhi au wakiwa kijijini) au mahali fulani, au kwamba mtu anakuwa hajaunganishwa na desturi yake au jamii," Cerelala aliiambia IPS.

Kwa upande wake PIF inazungumzia ‘umaskini wa fursa katika Viswa vya Pasifiki.

Mataifa yote ya visiwa vyenye wakazi milioni 10 na ongezeko la watu la 188,000 kwa mwaka yanakabiliwa na changamoto ya kuwa na ajira zenye maana huku suala la kuongezeka kwa vijana wasiokuwa na ajira likiwatia wasiwasi mkubwa. Ni katika Visiwa vya Cook na Niue pekee, ambako kiwango cha ajira ni asilimia 70 na asilimia 80, huku kisiwa cha Kiribati kikiwa na asilimia 44 na Samoa asilimia 30.

Wakati MDG7 – lengo linalotaka kuboreshwa kwa maisha ya wakazi wa makazi duni – halijaonekana sana katika ripoti, ongezeko la wakazi mijini limefikia kiwango cha juu cha asilimia 4.2 katika visiwa vya Solomon na Vanuatu.

Makazi yasiyopangwa ambayo yanakabiliwa na umilikaji wa ardhi usiokuwa na uhakika na nyumba duni, yanazidi kukua katika Melanesia kwani wakazi wengi wanatafuta ajira na huduma ambazo hazipatikani katika maeneo ya majimboni kwao. Wastani wa nusu ya wakazi katika mji mkuu wa PNG, Port Moresby, na asilimia 30 ya wakazi wa mjini katika Vanuatu wanaishi katika makazi yasiyopangwa.

Lakini katika mwelekeo chanya mataifa mengi ya Kisiwa cha Pasifiki yanatarajiwa kupunguza vifo vya watoto wachanga kwa theluthi mbili sanjari na lengo la MDG4.

"Hii inaweza kuhusishwa na mafanikio ya programu za kujenga uelewa zilizofanywa na mamlaka ya afya ya umma ya kikanda na kitaifa kuhamasisha chanjo na afya na matunzo bora ya watoto, wafanyakazi wenye mafunzo kwa ajili ya utekelezaji na kufuatilia afya za watoto," Gordon Nanau, mhadhiri wa masuala ya kimataifa, Chuo Kikuu cha Pasifiki Kusini, Fiji, alisema.

Nanau, ambaye ni mwanachama wa Mtandao wa Maendeleo ya Oceania, alisema msaada wa nchi na nchi na ule wa kimataifa pia ni muhimu katika kufikia MDG4.

Fiji ambayo ina wakazi 868,406 imepunguza vifo vya watoto wa chini ya umri wa miaka mitano kutoka asilimia 28 hadi 18 kwa watoto 1,000 wanaozaliwa wakiwa hai tangu mwaka 1990, jambo ambalo linahusishwa na utekelezaji wa mkakati wa pamoja wa kusimamia maradhi ya watoto na huduma bora za watoto hospitalini.

Katika kisiwa cha Tuvalu, kutokana na kiwango cha juu cha chanjo ya ugonjwa wa surua, kiwango cha vifo vya watoto chini ya miaka mitano kimepungua katika muongo uliopita kutoka 35 hadi 25 kwa watoto 1,000 wanaozaliwa wakiwa hai.

PIF ina imani kuwa kuongezeka kwa kasi kwa mafanikio ya ukanda huo ya kufikia malengo kabla ya mwaka 2015 kunategemea sana dhamira ya kisiasa.

Nanau alikubaliana, lakini aliongeza kuwa "hata kwa kuwepo kwa uongozi wa kisiasa wenye nia na kuboreshwa kwa utawala, usimamiaji wa fedha na rasilimali watu na uwezo wao" pia ni muhimu. (END/2012)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The element 'html' is used but not declared in the DTD/Schema.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>