Inter Press Service News Agency
Thursday, April 26, 2018   20:03 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions


Maswali na Majibu: "Kilimo Kidogo Kidogo Kinahitaji Kutambuliwa Kama Biashara"
Na Raúl Pierri

PUNTA DEL ESTE, Uruguay, Desemba 3 (IPS) - Mataifa yanayoendelea ya Kusini yanapaswa kuondokana na vikwazo ambavyo bado vinawakabili wakulima wadogo wadogo, kwasababu wakulima hao wana mchango mkubwa katika ukuaji wa kiuchumi, anasema Carlos Seré, Mkuu wa Kuendeleza Mikakati katika Shirika la Kimataifa la Maendeleo ya Kilimo (IFAD).

"Sera za taifa na kikanda zinapaswa kuondokana na ucheleweshwaji wa mpakani na vikwazo vya mara kwa mara vinavyowakabili wakulima wadogo wadogo," alisema mtaalam mwenye asili ya Uruguay, ambaye alisisitiza kuwa "Uwekezaji katika wakulima wadogo wadogo na maendeleo ya vijijini ni msingi wa ukuaji wa uchumi."

Katika mahojiano haya na IPS wakati wa Mkutano wa Pili wa Utafiti kwa Maendeleo ya Kilimo (GCARD2), Seré pia alijadili umuhimu wa kusaidia wanawake wapate kumiliki ardhi na kukabiliana na changamoto za kimazingira zinazowakabili wakulima wadogo wadogo.

Oktoba 29-Nov. 1 mkutano ulifanyika katika mji wa mapumziko nchini Uruguay wa Punta del Este ambao uliandaliwa na Jukwaa la Kimataifa la Utafiti wa Kilimo, kwa kushirikiana na Kundi cha Ushauri wa Utafiti wa Kilimo Duniani linalojulikana kwa kirefu chake cha Kiingereza kama CGIAR.

Sehemu ya mahojiano inafuata:

Q: Mkakati wa GCARD2 ni kusisitiza katika utafiti na ubunifu ili kuleta maendeleo. Je mapendekezo ya maarifa ya mababu zetu katika jamii – ambayo yameonyesha kuwa na ufanisi, kwa mfano, katika utafiti wa mbinu za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi katika ngazi ya jamii – yameachwa?

A: GCARD2 ni mkusanyaji wa wadau mbalimbali katika jukwaa moja ambalo linakuza ushirikiano katika utafiti kwa ajili ya maendeleo. Lengo ni kuleta ushirikiano kati ya taasisi zenye mafanikio makubwa katika utafiti katika nchi zilizoendelea, vituo vya kimataifa vya utafiti wa kilimo kama vile CGIAR, na mifumo ya kitaifa ya utafiti wa kilimo katika nchi zinazoendelea.

Utafiti wa kilimo katika nchi zinazoendelea unahusu pia vyombo katika ngazi ya taifa na jamii kama vile vyuo vikuu vya kilimo, mashirika ya kijamii, NGOs na mashirika ya wakulima, ikiwa ni pamoja na mashirika ya wazawa, kama washirika kamili katika mchakato wa utafiti.

GCARD2 inasisitiza katika jukumu la maendeleo shirikishi katika teknolojia ambalo linajijenga katika maarifa ya jamii na kuhusisha uelewa mzuri wa watu, imani zao, tamaduni zao na mambo mengine ya kijamii na kiuchumi ikiwa ni pamoja na mazingira ya kibaolojia na maumbile ya nchi.

Swali: Ni kwa jinsi gani wakulima maskini wanaweza kuanza kutumia teknolojia mpya na ni vigezo gani vinapaswa kutumika katika kuongoza sekta ya uwekezaji?

Jibu: Kwa utafiti kuhama kutoka maabara hadi kwenye eneo la kazi, unahitaji kuungwa mkono na mfumo wa ugani wenye nguvu na kuwezesha sera ambazo zinaunganisha matokeo ya utafiti na masoko ili kufaidisha umma na sekta binafsi.

Uamuzi au uchaguzi wa kutumia teknolojia mpya mara nyingi ni swala gumu kwa wakulima, hasa kutokana na kwamba wanashiriki katika kilimo kutokana na sababu mbalimbali kama vile kuzalisha kipato, kwa ajili ya matumizi yao ya chakula, kupunguza madhara yanayoweza kutokana na vyanzo vingine vya kipato (mfano ajira zisizokuwa rasmi), nakadhalika.

Uwekezaji katika maendeleo ya teknolojia mpya kwa ajili ya kutumiwa na wakulima wadogo wadogo kunahitaji kuongozwa na uelewa wa motisha na hatari zinazowakabili wakulima tofauti.

Hii inaleta haja ya kuegemea zaidi katika utafiti na jitihada za ubunifu ili kujenga teknolojia ambayo itasaidia wakulima kuongeza uzalishaji wao kwa njia ambayo itawawezesha kukabiliana vyema na mazingira magumu, uhaba wa maji na mabadiliko ya tabia nchi.

Swali: Kuna miradi kama ya "Vijiji vya Milenia" ambayo inasaidia wakulima wadogo katika fani mbalimbali na wameweza kuongeza mazao yao. Hata hivyo, bado wanakabiliwa na ugumu wa vifaa katika kufikia masoko na kuhakikisha kuwa ongezeko hili litatafsiriwa katika mapato makubwa zaidi. Jambo hili linaweza kutatuliwa kwa njia gani?

Jibu: Wakati wakulima wadogo katika nchi zinazoendelea wanapoongeza uzalishaji, kwa kuanzia, inaweza kuleta mchango mkubwa katika usalama wa chakula katika jamii na kitaifa na maendeleo ya kiuchumi – kama wana uwezo, wanaweza kuhakikisha kuwa chakula cha ziada kinatosheleza, kinaleta usalama kutoka katika shamba la mkulima hadi kwenye soko.

Kwa wakulima kuwa na fedha zaidi, tunaweza kuanza kuona mabadiliko halisi katika ulimwengu unaoendelea. Uwekezaji katika kilimo kidogo kidogo na maendeleo vijijini ni msingi wa ukuaji wa kiuchumi.

Kama tunataka masoko ya kikanda kufanya kazi, kama tunataka kuhakikisha kuwa nchi zinazoendelea zinakuwa na usalama wa chakula na kiuchumi, ni lazima kubadili miundombinu yetu na jinsi tunavyoendesha biashara.

Barabara, upatikanaji wa umeme tulivu, nishati na maji ya bomba, na utawala bora ni mambo ya msingi katika kufanya mazingira ya biashara kuvutia. Katika nchi zinazoendelea kilimo kidogo kidogo kinapaswa kuonekana kama biashara.

Sera za kitaifa na kikanda zinahitaji kuondokana na ucheleweshwaji wa mpakani na vikwazo vya kisheria vinavyowakabili wakulima wadogo, ili kuwafanya kuwa rahisi kusafirisha mazao kutoka nchi moja hadi nyingine.

Swali: Ni jinsi gani mipango ya kutoa pembejeo na mafunzo kwa wakulima wadogo wadogo katika nchi za Kusini imefanikiwa, wakati ruzuku za kaskazini na vikwazo vya biashara vya kimataifa vinaendelea kuwepo?

Jibu: Mapendekezo au mipango ya kutoa pembejeo na mafunzo kwa wakulima lazima kuwa sehemu ya mipango mipana ya kusaidia wakulima kupata maendeleo katika nchi zinazoendelea – huku kukiwa na ongezeko la fursa za kufikia masoko.

Hata hivyo, wakati tunatambua kuna uharibifu wa masoko na kuna vikwazo vya biashara huria, bei ndogo za chakula duniani katika siku za zamani ziliathiri vibaya motisha katika kilimo na utekelezaji kwa sasa umebadilika kwa kasi.

Bei za juu lazima zije na fursa za usambazaji. Tunahitaji mfumo kamili wa kuchagiza ukuaji wa sekta ya kilimo na katika sekta nyingine za vijijini ambazo zinaweza kutoa fursa mpya za kiujasiriliamali na ajira.

Swali: Wanawake ni msingi wa familia katika dunia inayoendelea, lakini mara nyingi sheria na desturi za nchi zinawanyima kumiliki ardhi. Ni nini kinafanyika katika suala hili?

Jibu: Usawa wa jinsia ni suala la haki za binadamu za msingi na za thamani, lakini kwa sasa inazidi pia kueleweka wazi kuwa linakuwa suala la kuendesha ufanisi wa kiuchumi katika kilimo.

Wanawake wana majukumu makubwa katika nyanja zote za kiimo na mifumo ya chakula katika nchi zinazoendelea.

Wanawake mara nyingi ni wakulima katika nchi zinazoendelea. Kuwapatia wanawake usawa katika umilikaji wa ardhi, pembejeo na rasilimali nyingine za kilimo sawa na wanaume kunaweza kuongeza uzalishaji katika mashamba yao hadi kufikia asilimia 30 na kunaweza kupunguza idadi ya watu wanaokabiliwa na njaa duniani kwa watu milioni 100 hadi 150.

Tunajua, kutokana na tafiti za idadi ya watu, kuwa wakati wanawake wanapopata pesa, wana uwezo mkubwa wa kutumia katika chakula cha familia ikilinganishwa na wanaume. Wanawake wa kijijini wanapokuwa na uwezo wa kiuchumi na kijamii, wanakuwa nguvu muhimu ya kuleta mabadiliko. Linapokuja suala la kumiliki ardhi, hii inaweza kutafsiriwa kuwa mfumo unaozingatia jinsia katika taasisi zinazoongozwa na jamii.

Kwa hiyo shughuli ambazo zina faida katika upatikanaji wa ardhi, kujengea uwezo wanawake kujua haki zao na uwezo wa kuzidai, kusaidia wanawake wa kijijini kuwa na vitambulisho ili waweze kudai haki zao za ardhi ni masuala muhimu sana ya taasisi za uwezeshaji, wakati mifumo ya teknolojia inapaswa kuzingatia kuokoa muda na nguvu wanazotumia wanawake. (END/2012)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The element 'html' is used but not declared in the DTD/Schema.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>