Inter Press Service News Agency
Tuesday, June 19, 2018   19:22 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions


Maswali na Majibu: Onyesho la Nyota Wanaoendesha Harakati
Becky Bergdahl

UMOJA WA MATAIFA, Novemba 27 (IPS) - Anzisha mjadala wa kidunia unaoangalia sababu kwa nini umaskini unaendelea kuwepo – na tumia sinema. Mpango mkubwa wa "Kwa nini Umaskini" unaleta pamoja watengenezaji filamu maarufu nane na wengine 30 wenye vipaji vya filamu zinazofundisha masuala mbalimbali ya umaskini, kama vile jinsia na kukosekana kwa usawa, ubaguzi na misaada na biashara.

Kuanzia Novemba 25 hadi 30, filamu zitarushwa duniani kote kupitia mashirika ya utangazaji ya kitaifa 62 kupitia duniani kote, na kufikia watu milioni 500. Mjadala wa mtandaoni kuhusu mada hii utafuata.

"Kwa nini Umaskini" ilizinduliwa katika Umoja wa Mataifa Sep. 27, na inaendeshwa na shirika la Steps, lenye makao yake nchini Denmark na Afrika Kusini. Ajenda siyo kutafuta pesa au kushinikiza hata ufumbuzi mmoja tu wa umaskini duniani – nia ni kuchochea mijadala kuhusu maeneo ya umaskini kadri inavyowezekana.

Mtengezaji wa filamu wa Sweden Bosse Lindquist anatumia eneo la misaada ya kiutu katika mchango wake, katika filamu yenye jina la "Tupatieni Fedha". Alizungumza na mwandishi wa IPS Becky Bergdahl kuhusu filamu, na lengo lake ni kuangalia wanasanaa mamilionea Bob Geldof na Bono, ambaye alitumia miaka mingi akitetea watu maskini duniani.

Sehemu ya mahojiano inafuata.

Swali: Umekujaje na wazo la filamu?

Jibu: Nilikaribishwa na BBC, SVT na wahariri wengine kuangalia masuala ya misaada na maendeleo. Baada ya kuangalia ulimwengu wa matajiri na watu maarufu, nilikubali kuwa Bob Geldof, ambaye kwa njia nyingi alianza kuingia katika watu maarufu katika kupambana na umaskini, alikuwa ni mwanasanaa wa muda mrefu.

Amekuwa mwanaharakati tangu mwaka wa 1984, wakati huo akitafuta pesa za waathirika wa njaa, halafu baadaye kufanyia kazi suala la mabadiliko ya mfumo. Pia ilikuja kuwa wazi mapema kuwa Bono alijiunga naye katika kupambana na umaskini miaka ya 90, na watu hawa wakashirikiana na wengine wengi na mashirika, na sasa wameshapata mafanikio makubwa.

Swali: Je matamasha na kampeni za wanasanaa kama Bono na Geldof yalisaidia maskini?

Jibu: Ndiyo. Kwa kusema hili, pia ni muhimu kutaja kuwa hakuna tafiti za kisayansi kuonyesha matokeo halisi ya kampeni hiyo. Pia suala zima la matokeo ya jumla ya misaada ya maendeleo katika maendeleo ya kiuchumi ya Afrika. Haya ni masuala magumu mno, ikitegemeana na sababu nyingi.

Hata hivyo bado ni wazi kuwa Bono na Geldof walikuwa na jukumu kubwa mno katika kufutwa kwa madeni ya mataifa ya Afrika na mataifa tajiri mwaka 2005. Pia, Bono na Geldof walimsaidia Rais (George W.) Bush kuanzisha mpango wa PEPFAR (Mpango wa Rais wa Marekani wa Kupambana na Dharula ya UKIMWI), na kufanya dunia iliyoendelea kuanza kufadhili GAVI (Mpango wa Chanjo ya UKIMWI Duniani), miradi miwili ambayo kwa pamoja imefadhili sehemu kubwa ya madawa ya kuokoa maisha ambayo kwa sasa yanafikia Waafrika milioni nane waliaoambukizwa na VVU.

Swali: Je, nyota na tajiri mzungu anaweza kuwa msemaji wa Mwafrika mweusi maskini?

Jibu: Bono na Geldof wamekuwa watetezi maarufu wakifanya kazi kuongezwa kwa rasilimali kwa maskini barani Afrika, ikiwa ni pamoja na kubadilika kwa mfumo wa kimataifa, kufikia kuwa na sheria muhimu inayohusu misaada ya uwazi. Lakini wasemaji – hapana! Kazi hii lazima ifanywe na Waafrika wenyewe.

Swali: Je ni kwa kiasi gani kazi za mwanasanaa-mwanaharakati zinafanywa kwa ajili ya kuongeza umaarufu wa mtu mmoja mmoja, na ni kwa kiasi gani inafanyika kusaidia wengine?

Jibu: Ni watu maarufu wachache sana ambao wanashiriki katika kazi za misaada kuongeza umaarufu wao wenyewe. Bado sijathibitisha hilo kwa Bono au Bob Geldof wakifanya hivi. Lakini kwa hakika, utetezi wao wa kweli hauna madhara kwa majina yao makubwa na uuzaji wa rikodi zao.

Swali: Mataifa tajiri 20 duniani yanatumia asilimia 80 ya rasilimali. Baadhi ya watu wanaishi katika maisha ya anasa, wengine wanazidi kuwa na njaa. Inawezekana kuwa na usawa wa kidunia – bila ya kusaidiwa na nyota hawa?

Jibu: Tunapaswa kufanya kazi katika dunia ambayo ni ya usawa zaidi na ya haki. Hakuna kitu kingine kinaweza kuwa cha haki. Pia hii ni njia pekee kama tunataka kufanya dunia kuwa na amani zaidi na salama. Nadhani kuwa suala hili ni muhimu kwa kila mtu kuja pamoja na kupambana na uharibifu wa mazingira na kuongezeka kwa joto duniani.

Swali: Na tutafikiaje hili?

Jibu: Mapambano yamefanyika katika majukwaa kadhaa. Moja ya mapambano muhimu ni kuhusu kutungwa kwa sheria ambayo itapambana na rushwa na wizi katika biashara kati ya nchi zenye madini au rasilimali za kilimo na wanunuzi katika nchi tajiri.

Mapambano mengine makubwa ni kuhusu kumpatia kila mtoto elimu. Mapambano ya tatu ni wazi kuwa yanahusu kuhakikisha kuwa wanawake wana fursa sawa kama wanaume katika dunia.

Swali: Una maoni gani juu ya dhana ya "mtego wa misaada", dhana ambayo inasema kuwa nchi maskini zinakuwa tegemezi kwa misaada ya kigeni?

Jibu: Siyo nchi maskini sana zinazozidi kuwa tegemezi, ni maofisa wa serikali ambao wanazidi kuwa tegemezi. Kuna aina fulani ya rushwa katika kuhamisha fedha nyingi, na kuna hatari kwa watu kudanganyika na hili.

Lakini ukweli kwamba kuna "mtego wa misaada" hata kama upo hauwezi kuwa sababu ya kuachana na misaada yote. Pamoja na kuwa ni sababu kubwa mno kudai uwazi kuhusu jinsi gani misaada inatolewa na kusambazwa, kwa kuwa na mbinu zilizojengwa ndani mwa wapokeaji wenyewe kufuatilia jinsi gani fedha zinatolewa (END/2012)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The element 'html' is used but not declared in the DTD/Schema.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>