Inter Press Service News Agency
Thursday, April 26, 2018   10:41 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions


Wakulima Wabeba Matumaini ya Amani na Maendeleo katika Kongo ya DRC
Na Taylor Toeka Kakala

GOMA, Kongo ya DRC, Novemba 27 (IPS) - Ng’omne wa maziwa wanachungwa tena katika vilima vya kijani katika jimbo la Kivu ya Kaskazini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Miaka ishirini iliyopita, kuibuka kwa vita vya kikabila kulisambaratisha kabisa mkoa huo, na kurejeshwa kwa shamba la Lushebere kunaweza kuonekana kama dalili na uthibitisho wa amani tete.

Likiwa limeanzishwa katika miaka ya 1960 na mtumishi wa dini Carbonel, shamba la Lushebere lililazimika kufungwa mwaka 1993 wakati mapigano makali ya kikabila yalipoanza mwezi Machi mwaka huo katika eneo la Ntoto, katika jimbo la Walikale, kabla ya kuenea katika maeneo mengine ya Kivu Kaskazini: Masisi na Rutshuru, ikiwa ni pamoja na Kalehe, katika jimbo la Kivu ya Kusini.

Nyumba, mashamba na shule, vituo vya afya na masoko na makanisa vilichomwa moto, na mifugo ilichinjwa au kuchukuliwa na wanamgambo. Mameneja wa shamba walilazimishwa kuachana na shughuli zao wakati familia nyingi zilikimbia Masisi kwenda katika mji mkuu wa jimbo, Goma, au kuingia katika nchi jirani za Rwanda na Burundi.

Wakati wa miaka kumi ya kufungwa kwa shamba hilo, miti aina ya mikaratusi ilikatwa na kuuzwa ili kulipia mishahara ya wafanyakazi ambao walibakia nyuma kulinda mali zao.

Katika ukanda huo, ambako mkaa ni chanzo cha kipekee cha nishati, ukataji haramu wa miti unazidi kuongezeka, hata katika mbuga za wanyama.

"Kaya tisa kati ya kumi hutumia mkaa kwa ajili ya kuongeza joto katika nyumba zao na kupikia," alisema Emmanuel de Mérode, mkurugenzi wa Taasisi ya Utunzaji wa Mazingira wa Asili Kongo.

"Tangu mwaka 2003, tumeshapanda miti 20,000 ya mikaratusi ili kuchukua nafasi ya ile iliyokatwa na kuuzwa," Padre Diogène Harerimana, mkurugenzi wa shamba hilo, aliiambia IPS.

Shamba la hekta 558 lilianza kufanya kazi tena mwaka 2003 kutokana na mchango wa euro 33,000 kutoka shirika la Saint Ave-Goma Entraide (SAGE), chama ambacho kiliundwa nchini Ufaransa mwaka 2002 kusaidia kujenga amani miongoni mwa vikundi vya kikabila vya Masisi kupitia shughuli za pamoja za kiuchumi.

Fedha ziliwafikia wakulima kwa njia ya vifaa ambavyo vilikuwa vimeshanunuliwa. SAGE pia imelipatia shamba chumba cha baridi kwa ajili ya kuhifadhia mazao yake ya maziwa na gari aina ya 4×4 kusafirisha mazao kwenda katika soko la Goma.

Mwezi Julai, shamba lilipokea msaada mwingine wa euro 61,000, wakati huu kutoka Rotary Club ya Vannes, mji wa magharibi mwa Ufaransa, na kutoka shirika la Rotary International. Fedha hizi zimesaidia kusambaza vifaa vipya vya kugandishia na kufungia maziwa.

Fundi kutoka kampuni ya Ulaya ambayo iliuza mashine hiyo kwa Lushebere alitembelea shamba kutoa mafunzo kwa wafanyakazi juu ya jinsi ya kuhifadhi vifaa hivyo. "Kwa sasa tunafanya kazi kwa kujitegemea," alisema Harerimana.

Kwa kuwa na vifaa vipya, shamba kwa sasa linafunga maziwa katika paketi za lita moja ambayo huuzwa kwa dola moja kila paketi, pamoja na kuwa mazao ya kila siku bado hayawezi kuzidi lita 50.

"Wakazi wa Goma na wafanyakazi wa mashirika ya misaada katika eneo lenye ukubwa wa mzunguko wa kilomita 20 (la Lushebere) wanazidi kuzoea aina hii ya maziwa," alisema Harerimana.

Ng’ombe wa shamba la Lushebere kwa sasa wanafikia 420, kidogo zaidi ikilinganishwa na jumla ya ng’ombe 2,000 waliokuwa nao mwaka 1990. Shamba pia lilikuwa na wafanyakazi 1,000 miaka 20 iliyopita. Leo hii linaajiri wafanyakazi 60, huku wakipatiwa mishahara ya kila mwezi ya kati ya dola 25 na 130.

Lakini tangu mwezi Julai, shamba limeweza kuongeza uzalishaji wa siagi kutoka kilo tano hadi kilo 35 kwa kila siku.

"Kwa sasa, maziwa yetu yanapimwa kwanza kuangalia kuwepo kwa bakteria kabla hayajaingizwa katika matenki makubwa na kuandaliwa kwa siagi," alisema Harerimana.

Vipande vya siagi huuzwa kwa dola tano kwa kilo, ikilinganishwa na dola tatu kwa kilo kwa siagi iliyozalishwa mahali pengine – lakini walaji wakuu wanavutiwa kulipia kiasi kikubwa kutokana na ubora wa maziwa yetu ambayo yameondolewa mafuta.

"Mara nyingi kichache ni kinyemi, na kinyemi ni kichache," alisema Jacques Bonana, mmoja wa wateja wa shamba hilo. Bonana anafanya kazi katika shirika la kibinadamu katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Lushebere.

Watu wengi wanakubaliana kuwa maziwa yetu ni bora katika kanda, alisema Charles Balume, mmiliki wa mgahawa mjini Goma.

Akiongea na IPS katika Francophonie Village mjini Kinshasa, mji mkuu wa DRC, katikati mwa Oktba, Carly Kasivita Nzanzu, waziri wa jimbo wa kilimo na maendeleo ya kijijini katika Kivu ya Kusini, alisema "Kiwanda hiki kipya kitaleta maendeleo ya kweli ya kiuchumi na kijamii katika mkoa wa Lushebere na katika Kivu ya Kaskazini yote."

Katika mkoa huu, ambako watu hawaaminiani na wanajamii wamezoea kuzurula ovyo, Monsignor Théophile Kaboy, askofu wa Goma, hafichi wasiwasi wake.

Anahofia kurejea kwa wanamgambo kutoka Ntoto: Raïa Mutomboki (neno lenye maana ya "tunasafisha watu wasiokuwa wazawa) ambao mara nyingi wanapigana na Nyatura (neno lenye maana ya "futilia na kung’oa wanaojiona kuwa ni wazawa" kwa lugha ya Kinyarwanda). Kila kikundi cha wanamgambo kinasaidiwa na wanasiasa fulani. (END/2012)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The element 'html' is used but not declared in the DTD/Schema.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>