Inter Press Service News Agency
Thursday, June 21, 2018   09:53 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions


Maswali na Majibu: Kuonyesha Mazuri, Mabaya na Kukosekana kwa Uhuru wa Habari
Na Stanley Kwenda

JOHANNESBURG, Novemba 26 (IPS) - Mwandishi Stanley Kwenda akizungumza na PANSY TLAKULA, Msimamizi Maalum wa Uhuru wa Habari na Upatikanaji wa Habari wa Umoja wa Afrika Pansy Tlakula, Msimamizi Maalum wa Uhuru wa Habari na Upatikanaji wa Habari wa Umoja wa Afrika, amefanya kazi ya kutosha ya kutafutia ufumbuzi kuendelea kwa udhalilishaji wa waandishi wa habari nchini Gambia.

Akiwa katika jukumu lake kama kamishina wa Tume ya Afrika kuhusu Haki za Binadamu, amewahi kutoa wito mara kadhaa kwa serikali ya taifa hilo la Afrika Magharibi kuheshimu haki ya kujieleza.

"Nimeandika barua kadhaa kwa serikali juu ya kukamatwa kwa hivi karibuni kwa waandishi wa habari – serikali kwa sasa imechoka na barua zangu. Tumefanya kila linalowezekana kuonyesha tatizo la Gambia na mataifa mengine ya Afrika," aliiambia IPS.

Lakini haijatosha kuzuia ukandamizaji wa vyombo vya habari nchini Gambia.

Mwezi Septemba, serikali ilikamata waandishi wa habari wawili na kufungia magazeti yao, The Standard na The Daily News, kutokana na kuandika habari nyingi za upinzani unaotokana na serikali kuwanyonga wafungwa tisa.

Mwezi Juni, waziri wa zamani wa Habari na Mawasiliano nchini humo Amadou Scattred Janneh na wengine watatu walikamatwa kutokana na kuchapisha na kusambaza fulani ambazo zilitoa wito wa kukomeshwa kwa udikteta nchini Gambia.

Janneh, ambaye pia ni raia wa Marekani, ameshitakiwa kwa kosa la uhaini na kufungwa kifungo cha maisha lakini aliachiliwa huru baada ya mwanaharakati wa haki za binadamu wa Marekani Mchungaji Jesse Jackson kuingilia kati.

Tlakula alisema kuwa Tume ya Haki za Binadamu Afrika ilipeleka kesi ya Janneh kwenye Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi.

"Lakini kwa bahati mbaya Gambia haijaridhia itifaki inayounda Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na hivyo kushindwa kuwapeleka mahakamani," alisema.

Lakini kushindwa kwa Gambia hakujaondoa nia ya Tlakula ya kuhakikisha kuwa uhuru wa habari unakuwepo katika bara. Hivi karibuni, alichukua hatua kali za kuhimiza serikali za Kiafrika kuanzisha vyombo huru vya kusimamia uhuru wa habari, akisema kuwa wanasiasa na serikali hawatakiwi kumiliki vyombo vya habari.

Tlakula, ambaye ni wakili wa Mahakama Kuu ya Afrika Kusini, mjumbe wa zamani wa Tume ya Haki za Binadamu Afrika Kusini na mwenyekiti wa sasa wa Tume Huru ya Uchaguzi, anataka kuona mazingira ya kisheria barani Afrika ambayo yanaruhusu uhuru wa waandishi wa kufanya kazi zao.

Sehemu ya mahojiano inafuata:

Swali: Ni jukumu gani ambalo waandishi wanapaswa kulitekeleza barani Afrika?

Jibu: Waandishi wa habari wanatakiwa kuanika rushwa, uhalifu na mambo yote mabaya kuhusu bara hili, lakini pia tunatakiwa kuonyesha mambo mazuri ya bara letu kwani hapa ndiyo nyumbani kwetu.

Hatuwezi kuonyesha ubaya tu wa bara letu kwa dunia. Tunatakiwa kubeba sifa yetu na kutoa habari zetu wenyewe na wala siyo kutegemea kutolewa na watu wengine.

Swali: Mataifa kadhaa barani Afrika hayana sheria za kukuza haki ya habari. Katika ngazi ya bara ungependa suala hilo kusukumwa ili kuwa na haki ya kupata habari katika bara?

Jibu: Tumesukuma suala hilo kwa kiasi. Tumeandaa sheria ya mfano kuhusu upatikanaji wa habari Afrika. Tulianza mchakato wa kuandaa sheria hiyo katika mataifa matano ya Afrika na sasa tuna mataifa 10 ambayo yana sheria ya upatikanaji wa habari.

Mataifa zaidi sasa yana miswaada ya sheria ya upatikanaji wa habari ambayo inasubiri kupelekwa bungeni. Tuna matumaini kuwa sheria hii ya mfano itasukuma mipango ya upatikanaji wa sheria kwasababu tunadhani hatupaswi tu kukosoa nchi, lakini kuwasaidia kufikia uhuru wa habari. Bila ya kuwa na uhuru habari, haki nyingine zote hazitafikiwa.

Swali: Zimbabwe imewahi kuwa na sifa mbaya sana ya uhuru wa habari barani Afrika siku za nyuma. Wakati sasa ikiandaa rasimu ya katiba mpya, ushauri wako ni nini kwa nchi hiyo?

Jibu: Katiba mpya haitatua matatizo yote. Hata baada ya katiba mpya, bado tutaendelea kuwa na sheria ambazo zinakandamiza uhuru wa kujieleza kama vile Sheria ya Upatikanaji wa Habari na Kulinda Siri za Mtu Binafsi, Sheria ya Utulivu wa Uma na Usalama, na sheria nyingine nyingi ambazo haziendani na sheria nyingine za kikanda na kimataifa ambazo Zimbabwe imeridhia.

Sheria hizo zinaendelea kubakia kuwa chanzo cha wasiwasi kwetu sisi lakini tuna matumaini kuwa kutokana na katiba mpya, sheria hizi zitafanyiwa marekebisho ili kuzingatia katiba.

Mara tu katiba mpya itakapopitishwa, sheria hizi inabidi zirekebishwe upya au kuandikwa upya. Kama siyo hivyo, zinaweza kupingwa mahakamani. Katiba mpya ni hatua katika mwelekeo mzuri, pamoja na kwamba sheria zinapaswa kuzingatia katiba.

Swali: Je tunapata mafanikio yoyote katika suala zima la uhuru wa habari katika bara?

Jibu: Ndiyo tunapata mafanikio kwa kuhamasisha baadhi ya nchi kupitisha sheria za kukuza uhuru wa habari. Kwa sasa tuna kampeni yenye lengo la kuondoa suala la kashfa katika makosa ya jinai.

Awamu ya kwanza ya kampeni hii ni kubainisha ni wapi sheria hizi za kashfa zinapatikana kwasababu pale ambapo zipo zina faida kubwa kwa uhuru wa kujieleza. Tunaendesha kampeni ya majaribio nchini Zambia na Botswana.

Swali: Unashughulikaje na kuongezeka kwa hoja kwa baadhi ya nchi kuwa kusita kwao kupitisha sheria za uhuru wa kujieleza kunatokana na masuala ya usalama wa taifa?

Jibu: Hii inasababisha swala muhimu kuhusu haja ya kuchora mstari unaoonyesha mpaka kati ya habari zilizopo na kupatikana katika hali ambayo haiwezi kuathiri usalama wa taifa. Ni suala kubwa na tunajaribu kuweka miongozo ya upatikanaji wa habari na usalama wa taifa. Ni suala linaloikabili dunia nzima, na kazi hiyo ni endelevu.

Swali: Unaonaje kwa Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma kufuta kesi yake dhidi ya mwandishi na mchoraji wa katuni Jonathan Zapiro, ambaye alimfungulia mashitaka na kutaka kulipwa maelfu ya dola dhidi ya katuni ambayo ilimuonyesha akijiandaa kumbaka mwanamke huku akisaidiana na wafuasi wake serikalini na chama chake cha siasa?

Jibu: Nina furaha kubwa. Ni ushindi kwa uhuru wa kujieleza na uandishi wa habari barani Afrika. (END/2012)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The element 'html' is used but not declared in the DTD/Schema.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>