Inter Press Service News Agency
Wednesday, April 25, 2018   07:55 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions


Wanamazingira Watoa Wito kwa Waganda Kutokula Sokwe
Na Henry Wasswa

MKOA WA ALBERTINE RIFT, Uganda, Novemba 16 (IPS) - Wanamazingira wanaofanya jitihada za kulinda idadi ya sokwe inayobakia nchini Uganda wameonyesha wasiwasi wao kwa watu wanaozunguka hifadhi za wanyama pori magharibi mwa nchi hiyo kutokana na kuendelea kula sokwe. "Kwa sasa kuna suala gumu la ulaji wa nyama ya porini. Hatujawahi kudhani kuwa Waganda walikuwa wakila nyama ya sokwe lakini tunaanza kuona kuwa nyani na sokwe wanaliwa. Hii inashangaza. Tishio kwa maisha ya wanyama hawa imeendelea kuongezeka," kwa mujibu wa Lily Ajarova ambaye anaendesha Hifadhi ya Sokwe ya Ngamba, iliyopo katika kisiwa cha Ngamba katika Ziwa Victoria katika mkoa wa Albertine Rift.

Hifadhi hiyo, ambayo inakaliwa na jumla ya sokwe 48 waliookolewa kutoka mikononi mwa watu, ilianzishwa kwa msaada wa Taasisi ya Jane Goodall na inasimamiwa na asasi ya Chimpanzee Sanctuary and Wildlife Conservation Trust.

Miongo iliyopita, mamia kwa maelfu ya sokwe walizurua katika misitu minene ya kitropiki ambayo kwa wakati huo ilifunika sehemu kubwa ya ardhi ya mkoa wa Albertine Rift nchini Uganda. Eneo hilo ni pamoja na upande wa magharibi mwa Bonde la Ufa la Afrika Mshariki kutoka kaskazini magharibi mwa Uganda hadi upande wa kusini magharibi, mpakani mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Lakini kwa mujibu wa Mfuko wa Hifadhi ya Wanyamapori Ulimwenguni, sokwe tayari wamshatoweka katika nchi nne za Kiafrika, na wanakaribia kutoweka kabisa katika nchi nyingine ningi kutokana na matumizi makubwa ya misitu kwa kukata miti na uwindaji wa sokwe hao kwa ajili ya nyama pori. Kwa sasa kuna wastani wa sokwe 5,000 nchin Uganda, wanasema maofisa wa hifadhi ya mazingira.

Wengi wa sokwe wanaosalia nchini humo wanahifadhiwa katika hifadhi kubwa sita za wanyama na misitu katika mkoa wa Albertine Rift, wakati wengine wamezingirwa katika misitu inayomilikiwa na watu binafsi.

Ajarova aliiambia IPS kuwa pamoja na kwamba timu yake ya wanamazingira iligundua hapo kabla kuwa watu wanakula nyama ya sokwe magharibi mwa Uganda miaka miwili iliyopita, wale wanaoshiriki katika vitendo hivyo wengi wao walikuwa ni wahamiaji au wakimbizi kutoka nchi jirani ya DRC. Ilikuwa mara chache mno kwa wenyeji wa Afrika Mashariki kula nyama ya sokwe, alisema.

"Kuna maeneo mengine mengi ya dunia ambapo nyama ya sokwe inaliwa lakini hii haijawahi kutokea nchini Uganda. Tulianza kushuhudia jambo hili wakati huo. Limekuwa likikua polepole na sisi wenyewe tumepata upepo wa jambo hilo tulipokuwa katika kazi za uwandani miaka miwili iliyiopita," alisema, akiongeza kuwa kwa sasa "ni tatizo linaloibukia."

Kuwasili kwa hivi karibuni kwa wahamiaji kutoka DRC kubadili wakazi wa maeneo hayo na kuathiri utamaduni wa wazawa, alisema. Mwezi Julai Waziri wa Misaada ya Dharula, Kujiandaa na Majnga na Wakimbizi Musa Ecweru alisema kuwa Uganda ilikuwa ikijitahidi kulisha idadi kubw aya wakimbizi wanaokimbia kutoka nchi jirani ya DRC. Kuna wastani wa wakimbizi wa Kongo 16,000 magharibi mwa Uganda.

"Kuna wakimbizi wengi mno wa Kikongo katika eneo hilo na inawezekana wamesdhawishi wakazi wenyeji kula nyani na sokwe," Ajarova alisema. "Hii haikuwa sehemu ya utamaduni wa Waganda siku za zamani, lakini sasa linakuwa suala kubwa. Tumegundua kuwa tabia hiyo sasa ni kubwa katika ukanda mzima wa magharibi. Hali imezidi karibu katika vijiji vyote tulivyotembelea.

"Mara kw amara tuliona wanakijiji wakiwa wamebeba nyani waliowaua, na mara chache, wakiwa wamebaba sokwe," Ajarova alisema.

Maofisa pia wana imani kuwa watu wamenza kula sokwe kwasabau mkoa wa Albertine Rift una umaskin mkubwa na wengi wa watu wake wanategemea zaidi rasilimali za msituni kwa ajili ya kuishi, kwani hawawezi kumudu kununua nyama.

"Watu ni maskini sana, ni maskini kutokana na kuwa mkoa huu una maendeleo duni kabisa. Mara nyingi wanategemea rasilimali za msituni, ikiwa ni pamoja na kula nyama ya porini, na hili linaweza kuwalazimisha kuanza kula nyama ya sokwe," Ajarova alisema.

Wataalam sasa wana wasiwasi mweleko huo mpya unaweza kusababisha kulipuka kwa ugonjwa wa Ebola, ugonjwa wa kutokwa na damu nyingi na ambao unaua mara moja, ambao unaaminika kuambukizwa kutoka wanyama kwenda kwa binadamu pale wanapogusana.

"Hili ni tatizo kubwa sana. Nyama yoyote ile inayoliwa inapaswa kupitia kwa mkaguzi wa mifugo, hata kama inatoka porini. Watu wanaokula sokwe wana hatari ya kuambukizwa magonjwa yanayoambukizwa kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu, ikiwa ni pamoja na Ebola," alisema Andrew Seguya, mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Wanyamapori Uganda.

"Hakuna hata kabila moja la Uganda ambalo wana asili ya kula nyama ya sokwe, lakini kuna wakimbizi wengi wa Kongo katika eneo hilo na inawezekana Wakongo hao wameeneza tabia hiyo kwa wakazi wenyeji," alisema.

"Ebola inaenezwa kupitia kugusana moja kwa moja na imaanika kuwa sokwe hawa ndiyo wanaobeba virusi vya ugonjwa na kuambukiza wanadamu kwa njia nyingine nyingi, ikiwa ni pamoja na kugusa kkinyesi cha mnyama. Pia kuna kundi la wasomi ambalo lina imani kuwa UKIMWI umetokana na sokwe," Seguya, ambaye ni mtaalama wa upusuaji wa wanyama, aliiambia IPS.

Wilaya ya magharibi ya Kibaale, katika mkoa wa Albertine Rift, ulikumbwa na gonjwa ambalo liliaminika kuwa ni la Ebola mwezi Julai. Maofisa wa afya bado hawajathibitisha kuwa ilikuwa ni ugonjwa wa Ebola. Lakini kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari watu 17.

Wakati huo huo, Ajarova alisema jitihada zinafanyika kubadili mitizamo ya watu juu ya suala zima la kula nyama ya sokwe kupitia vipindi vya elimu maalum na kuanzisha miradi ya ufugaji wa wanyama miongoni mwa wanakijiji.

"Tunawaambia watu waache kula nyama ya sokwe, tunawapatia taarifa kuwa ni hatari mno kwa afya zao kwani watapata magonmjwa kama vile ugonjwa wa Ebola. Huu ni ujumbe muhimu katika programu zetu za elimu," alisema.

"Pia tunatumia redio za masafa ya FM kufikisha ujumbe wetu kwa jamii. Redio hizi huwafikia watu wengi kwa wakati mmoja," Ajarova alisema. (END/2012)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The element 'html' is used but not declared in the DTD/Schema.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>