Inter Press Service News Agency
Monday, June 18, 2018   10:49 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions


Wanawake Chachu ya Usalama wa Chakula
Busani Bafana

DES MOINES, Iowa, Marekani, Novemba 12 (IPS) - Katika kupitishwa kwa sera ya kuwekeza kwa wanawake – ambao ndiyo wakulima wengi wa mazao ya chakula duniani – Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon alisema usalama wa chakula hauwezi kufikiwa bila ya wanawake, na kuwa nchi zenye uhaba wa chakula duniani zinatakiwa viongozi wao kuwa na vipaumbele. "Watoto wa kike na wanawake katika jamii wana nafasi kubwa ya kukabiliana na njaa," Ban aliuambia mkutano wa viongozi wa dunia, watafiti, wakulima na watunga sera wakati wa uwasilishaji wa Tuzo ya Chakula Duniani mwaka 2012.

Mkutano wa viongozi wa dunia katika jimbo la katikati mwa Marekani la Iowa ulijadili mikakati ya kukuza uzalishaji wa chakula duniani umesema changamoto kubwa ya usalama wa chakula barani Afrika itahitaji kukusanya vichwa bora kabisa vya wanasayansi katika bara, ikiwa ni pamoja na vichwa vya wanawake wa bara hilo.

"Kukomesha njaa katika maisha yetu kunahitaji kuchanganya ubunifu wa wanasayansi na watafiti …kukomesha njaa pia kunatoa wito wa utawala bora duniani …Kukomesha njaa duniani kunaweza kufanyika na ni jambo sahihi kulifanya," Ban Ki-moon alisema katika sherehe za mwaka huu za Tuzo ya Chakula Duniani, tuzo ya kimataifa inayotolewa kutambua mchango wa watu mmoja mmoja ambao wamekuza maendeleo ya kibinadamu kwa kuleta ubora, wingi au upatikanaji wa chakula duniani.

Wito wa ushirikiano wa kimataifa katika kuleta uongozi wa usalama wa chakula wakati ambapo karibu watu bilioni moja wanalala njaa kwa mujibu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), Ban angekuwa anazungumzia kuhusu Wanawake wa Afrika katika Utafiti wa Kilimo na Maendeleo (AWARD).

Wiki hii, AWARD, iliadhimisha kufanya kazi kuongeza idadi ya wanawake watafiti na wanasayansi katika kilimo, na kupata karibu dola milioni 20 katika ufadhili mpya wa pamoja kati ya Bill & Melinda Gates Foundation na Shirika la Misaada ya Kimataifa la Marekani.

Msaada uliotangazwa katika Mjadala wa Borlaug, ulioandaliwa Okt. 17-19 huko Des Moines, Iowa, utaruhusu AWARD kuzindua awamu ya pili ya miaka mitano ya kuwapatia wanawake wanasayansi katika kilimo kwenye mataifa 11 Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, na kuongeza katika idadi ya mamia ya watafiti ambao wamekuwa wakisaidiwa tangu mwaka 2008.

Ni mmoja tu kati ya watafiti wanne barani Afrika ni wanawake, kwa mujibu wa utafiti wa AWARD wa mwaka 2008. Lakini hali inazidi kuwa mbaya: ni mmoja tu katika kila saba wanashika nafasi za uongozi katika taasisi za utafiti wa kilimo barani Afrika. Mwanzilishi wa AWARD Vicki Wilde alisema hii imewaacha wanawake kushindwa kuhudumiwa katika kilimo na hivyo kuwa katika nafasi duni zaidi ya kupambana na njaa.

"Inakuja kuwa siyo suala la kushangaza kwamba ni vigumu kufikia usalama wa chakula barani Afrika," Wilde aliiambia IPS. "Sehemu ya sababu ya jambo hilo kuwa gumu sana ni kwamba wakati nguvukazi ya wanawake katika kilimo ni kubwa zaidi barani Afrika, chini ya mmoja katika kila watu wanne katika utafiti wa kilimo ni wanawake, na hii imetufanya kuachwa katika mzunguko wa kuongeza thamani ya kilimo."

Wilde alisema wanawake hawakuwa katika utoaji wa maamuzi katika vipaumbele vya chakula. Aliongeza kuwa pamoja na kwamba kuwashirikisha siyo jibu la kila tatizo, itahakikisha maendeleo mazuri na ya kasi, na wakulima wadogo wadogo – ambao wengi wao ni wanawake barani Afrika – watahudumiwa vizuri zaidi kwa njia ya kuongeza uzalishaji wa chakula na kuongeza vipato vyao.

"Katika bara la Afrika tunahitaji kizazi cha viongozi wapya ambao ni wabunifu, wanaoona mbali, wajasiriamali, wenye ujuzi mkubwa na wanaozingatia jinsia, na wanapaswa kujibu vipaumbele vya wakulima wadogo wadogo, ambao wengi wao ni wanawake," alisema.

AWARD, ilipendwa na mashirika mengi katika Mjadala wa Borlaug, kuwa ni mpango mzuri ambao mwaka huu umeshuhudia maombi 3,000 ya wanasayansi wanawake wa Afrika kuingia katika nafasi 320 za kuwa wanasayansi wa shirika. Wilde alisema shirika lake limetaka kupanua wigo wa vipaji vya watekeleaji wa sera za usalama wa chakula.

AWARD ni mpango wa kuendeleza ujuzi kwa kuimarisha ujuzi wa utafiti na uongozi kwa wanawake wa Afrika katika sayansi ya kilimo, kuwapatia uwezo wa kuchangia kiufanisi zaidi katika kutokomeza umaskini katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Unatoa ufadhili wa miaka miwili kupata mafunzo ya vitendo katika maeneo ya ushirikishwaji, ujuzi wa sayansi na maendeleo ya uongozi. Wanawake wa Afrika wanaofanya kazi katika maendeleo ya utafiti wa kilimo kutoka Ethiopia, Ghana, Kenya, Liberia, Malawi, Msumbiji, Nigeria, Rwanda, Tanzania, Uganda na Zambia, na ambao wamemaliza shahada za kwanza, za pili au hata sahada za udaktari katika fani zinazokubaliwa wanastahili ufadhili huo.

Mary Njenga, mtafiti katika AWARD kutoka Kenya, ni mwanamke mwenye maono yake ya kubadili sera na mitizamo ya majukumu ya wanawake katika usalama wa chakula.

Njenga, mwanasayansi wa mazingira ambaye anaunganisha kilimo na mazingira na masuala ya nishati, amejikita katika kuboresha usimamiaji wa maliasili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Amefanya hivi kwa kuingiza teknolojia kama zile ambazo ni rafiki kwa mazingira, nishati rahisi inayotokana na vumbi mkaa, vumbi la mbao na vitu vingine vinavyotokana na mimea katika jamii maskini.

"Naweza kufanya kazi na wanawake na kuja na teknolojia nzuri, lakini kama sina sauti ya watunga sera, teknolojia zangu zitabaki kwenye vitabu na hazitatumiwa," Njenga aliiambia IPS.

"Kwa kupitia mafunzo na mafunzo kwa vitendo katika AWARD, nimejifunza kushawishi maendeleo ya kisera kwa ajili ya kuleta mabadiliko kutokana na kuwa na mbinu za kuandika kwa makundi tofauti na kutumia njia tofauti za kuchapisha masuala yangu katika vyombo tofauti vya habari kufikia watu katika lugha wanayoweza kuelewa."

Njenga, mtafiti mwenye PhD katika Chuo Kikuu cha Nairobi anayefanya kazi kwa kushirikiana na World Agroforestry Centre (ICRAF), alikuwa anapenda kutengeneza nishati safi kuboresha kipato cha wanawake na kulinda afya zao na za watoto wao wakati huo huo wakilinda mazingira.

"Nina wasiwasi kuwa tunaweza kufikia hali ambapo katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara tutaweza kuzalisha chakula lakini tukashindwa kupika kutokana na kukosekana kwa nishati; na hivyo ni lazima kuweka kipaumbele katika nishati ya taka za wanyama na majumbani kwa ajili ya kupikia kama sehemu muhimu ya usalama wa chakula na lishe," Njenga alisema.

Mtafiti mwingine wa AWARD, Profesa Sheila Okoth wa Chuo Kikuu cha Nairobi, amechangia kwa kiasi kikubwa katika kupunguza njaa kupitia utafiti wake juu ya ufumbuzi wa kukabiliana na sumu, zinazotokana na kuvu katika mashamba ya Kenya.

"Nilibadilika sana kutokana na mafunzo na uelewa niliopata kutoka AWARD," alisema Okoth. "Hata sasa nina nia ya kusaidia kutatua tatizo la sumu ambazo zinafanya wakulima maskini kuwa maskini zaidi."

Okoth alianzisha maabara ya kwanza ya uzamili, kutokana na mafunzo yake ya sayansi ya juu ya miezi mitatu katika Chuo Kikuu cha Stellenbosch nchini Afrika Kusini, ambayo yalifadhiliwa na USAID kupitia AWARD (END/2012)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The element 'html' is used but not declared in the DTD/Schema.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>