Inter Press Service News Agency
Monday, June 18, 2018   10:55 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions


Ili Kupunguza Umaskini Afrika – Muelimishe Mtoto wa Kike - Reduce
Blain Biset

ADDIS ABABA, Novemba 12 (IPS) - Wakati muongo uliopita idadi ya nyongeza ya watoto milioni 52 katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara waliandikishwa katika shule za msingi, huku idadi ya watoto wa kike ikiongezeka kutoka asilimia 54 hadi asilimia 74, idadi kubwa ya watoto hao wa kike – milioni 16 – bado wanaendelea kunyimwa elimu.

Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya shirika la Plan International yenye jina la "Progress and Obstacles to Girls’ Education in Africa" yaani Mafanikio na Vikwazo vya Elimu ya Watoto wa Kike Barani Afrika iliyotolewa mjini Addis Ababa, Ethiopia Okt. 11 – siku ya kwanza ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike.

Ripoti inasema kuwa kujiandikisha shule katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kunabakia kuwa katika idadi ya chini zaidi duniani, huku watoto wa kiume wakiwa na fursa zaidi ya kuandikishwa ikilinganishwa na watoto wa kike.

Inaonya kuwa kama hali haitabadilika mara moja, Lengo la Maendeleo ya Milenia la kutoa elimu ya msingi kwa wote ifikapo mwaka 2015 halitafikiwa. (MDGs ni mlolongo wa malengo ya maendeleo juu ya maendeleo na kupambana na umaskini ambayo yalikubaliwa na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa mwaka 2000.)

Luther Anukur, naibu mkurugenzi wa kanda ya Afrika Mashariki na Kusini wa Plan International, aliiambia IPS kuwa utamaduni ulikuwa moja ya sababu kuu za tatizo: "Tunapaswa kushirikiana na wanajamii kujadili suala la watoto wa kike ambao hawaendi shule."

Sababu kadhaa zinazuia watoto wa kike wasiende shule, kama vile gharama za elimu, unyanyasaji mashuleni, au familia kupendelea kupeleka shule watoto wa kiume badala ya watoto wa kike.

Ripoti inasema kuwa wakati nchi nyingi katika bara zina sera za kitaifa zinazohakikisha elimu ya msingi ya bure, ukweli halisi ni kwamba watoto wa kike na wazazi wao ni tofauti sana.

"Wakati ada zinaweza kuwa zimesitishwa, shule nyingi zinaendelea kutoa aina nyingine za ada, kama vile kujisajili kufanya mitihani. Hii pia inaongeza katika gharama za sare za shule, vitabu, usafiri, madaftari na kalamu na gharama nyingine za elimu ambazo hazionekani, na hivyo kufanya kumpeleka mtoto shule kuwa suala kubwa la kifedha kwa familia," inasema ripoti hiyo.

Ndoa za mapema na kupata mimba ni sababu nyingi muhimu ya msingi inayofanya watoto wa kike kuacha shule. Nchini Uganda, Guinea-Bissau na Liberia, karibu asilimia 60 ya watoto wanaosoma shule waliacha masomo yao kutokana na kupata mimba, kwa mujibu wa ripoti. Na katika nchi kama Niger, Chad na Mali, watoto wawili kati ya watatu wanaolewa kabla ya miaka 18.

Isabel* ni mtoto mwenye umri wa miaka 19 kutoka Msumbiji ambaye ameolewa mara mbili, na hivi karibuni alilazimishwa na familia yake kuolewa mara ya tatu tena na mwanaume mzee. Hana elimu na hivyo anategemea zaidi familia yake.

"Walinionya kuwa kama nikishindwa kutekeleza maneno yao, wangenifukuza na watoto wangu wawili. Kwasababu sina ajira, nililazimika kukabiliana na changamoto hii," aliiambia Plan International.

Latifa* mwenye umri wa miaka kumi na tano kutoka Ethiopia aliweza kuhimili vishindo vya familia yake wakati baba yake wa kambo alitaka aolewe kwa mwanaume mwenye umri wa miaka 40 ambaye ni askari. Haikuwa rahisi kwa Latifa kukabiliana na changamoto ya familia yake kwani alibughudhiwa sana. Aliiambia Plan International: "Hali ilipozidi kuwa mbaya kuweza kuihimili, nilikimbia kwenda kuishi na shangazi yangu kilomita 60 kutoka nyumbani kwetu." Hata hivyo kupata ada ya shule limekuwa tatizo kubwa, lakini kutokana na kuwa na ajira ya muda mfupi katika saluni anaweza kulipia ada hiyo.

Lakini watoto wengi wa kike kama Latifa mara nyingi huishia katika mahusiano ya kingono kuweza kulipia ada zao za shule au kununua mahitaji ya msingi lakini ambayo hawana uwezo wa kuyanunua kama vile sabuni, chakula na nguo, kwa mujibu wa ripoti hiyo.

Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike inalenga katika kusaidia watu kama Isabel na Latifa, lakini watoto wa kiume na wanaume pia wanapaswa kutekeleza sehemu yao, Anukur alisema. "Uamuzi kama mtoto wa kike aende shule au asiende unaamuliwa na wanaume. Hivyo tutalenga familia kupeleka watoto wao shule, ili wawe mifano ya kuigwa katika jamii."

Wakati Afrika ni maskini, serikali zinatumia sababu hii mara nyingine kutokana na kushindwa kwao kubeba wajibu juu ya hali kama hii, Anukur alisema. Alisema kuwa bara hili halina uhaba wa rasilimali.

"Suala la msingi ni jinsi gani rasilimali hizi zinagawanywa vizuri na kutumiwa. Utawala ni suala kubwa barani Afrika; ni muhimu kuwa serikali zinajitolea kuleta mabadiliko."

Profesa Jean-Pierre Onvehoun Ezin, wa Tume ya Rasilimali Watu, Sayansi na Teknolojia ya Umoja wa Afrika (AU), aliiambia IPS kuwa shirika lake lina nia ya kuhakikisha kuwa watoto wa kike barani Afrika wanakua katika mazingira salama huku wakiwa na fursa za kufikia mustakabali wao kamili.

"Kutokana na kwamba wana umri mdogo na ni wanawake, watoto wa kike wanakandamizwa kuliko kundi jingine lolote lile, wananyonywa na kunyanyaswa." Aliongeza kuwa ili kuhakikisha watoto wa kike wanafikia fursa zao kamili "siyo suala la kuwa na dhamira tu moyoni, lakini ufumbuzi mkubwa zaidi tunaojua ni kuondokana na umaskinki."

Ezin aliiambia IPS kuwa wakati sera zilikuwa bora katika karatasi, kuzitekeleza kunazidi kubakia kuwa kikwazo katika bara zima.

"Kama shirika au taasisi pekee, unaweza kuzungumza mambo mengi na kwa sauti kubwa, lakini huwezi kuleta mabadiliko mwenyewe."

Kamishina wa AU ana imani kuwa elimu ya msingi ni jukumu la nchi husika. "Mashirika ya kiraia, mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na serikali wanapaswa kufanya kazi pamoja kutekeleza sera za elimu," alisema. (END/2012)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The element 'html' is used but not declared in the DTD/Schema.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>